Mwanafunzi aliyepotea akutwa Mbinga Mkoani Ruvuma


MWANAFUNZI wa kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya St. Anthony Mbagala, mkoani Dar es Salaam, Franco Donald Kisongo (18),(pichani) aliyepotea jijini humo Machi 18 mwaka huu, amepatikana Mbinga mkoani Ruvuma.

Kijana huyo aliyekuwa mgeni jijini Dar es Salaam alipotea siku nne tu tangu ajiunge na shule hiyo kuanza masomo ya kidato cha tano.

 Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika familia ya Franco, kijana huyo alifika kwao Mbinga mkoani Ruvuma Machi 23, akiwa peke yake.

Inadaiwa kuwa, baada ya kufika kwao, alisema kuwa hajui alifikaje huko akiwa ametumia takribani siku sita njiani kutoka Dar es Salaam.



Machi 18 asubuhi, Franco aliwaaga wanafunzi wenzake kuwa alikuwa anakwenda kwa shangazi yake, Adela Kisongo, Kariakoo jijini humo, hakufika huko, pia hakurudi shule, na haikufahamika alikuwa amekwenda wapi.

 Walimu na walezi wa kijana huyo, walitoa taarifa Polisi, na wakatumia RB namba 3343/2012 ya kituo cha Msimbazi kumtafuta.

Wazazi na wanafamilia ya Franco wanawashukuru wote ambao kwa namna moja au nyingine walishiriki kumtafuta kijana huyo, aksanteni.

Kampeni Za CHADEMA Udiwani Songea Leo


Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ruvuma Joseph Fuime akinada sera za chama hicho kwenye kampeni za uchaguzi zinazoendelea kata ya Lizaboni
Mbunge wa Vitimaalum na Mjumbe wa Kamati kuu ya Chadema Taifa Chiku Abwalo akiwahutubia wananchi wa Kata ya Lizaboni waliofika kwenye viwanja vya Sokoni kusikiliza mkutano huo.
Picha kwa hisani ya mjengwa blog

WAUZA MBOLEA FEKI WAKAMATWA SONGEA



Wafanyabishara wa mbolea waliokamatwa na jeshi la polisi mkoani Ruvuma jana kwa tuhuma za kuuza  chumvi walioiweka katika mifuko ya mbolea na kuwauzia wananchi kama mbolea aina ya SA, kutoka kushoto Abdilai Abdala(42) Yasin Gawaza(48) Festo Sanga(25) na Ajda Halfan(36) wakiwa katika kituo kikuu cha polisi mjini songea.
PICHA NA MUHIDIN AMRI.
Kwa hisani ya Michuzi Blog

Wanafunzi wa shule ya sekondari St Benedictine wafanya mdahalo wa kujiepusha na ukimwi


Kaimu mkurugenzi wa halmshauri ya wilaya Namtumbo Constatino Mushi kushoto akimfariji mwanafunzi wa kidato cha 3 shule ya sekondari Runa wilayani humo Abdul Ngonyani aliyevunjika mkono wake wa kulia kufuatia gari walilokuwa wakisafiria kupinduka na kusababisha kifo cha mwanafunzi mmoja na wengine kujeruhiwa,katika ni baba mzazi Abdul Mang'inyuka,
Mwezeshaji wa mafunzo ya ukimwi kutoka idara ya maendeleo ya jamii ya halmshauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Pees Kamugisha akitoa mada wakati wa mdahalo wa wazi juu ya maambukizi mapya ya ukimwi kwa wanafunzi wa shule ya sekondari  st benedictine hanga, uliofanyika jana shuleni hapo,
Mwenyekiti wa kamati ya kudhibiti ukimwi ya halmshauri ya wilaya ya namtumbo ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa halmshauri hiyo Kassim Ntara akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya St Benedictine Hanga wakatri wa mdahalo wa siku moja juu ya kujikinga na maambikizi mapya ya ukimwi uliofanyika jana shuleni hapo,
Wanafunzi wa shule ya sekondari St Benedictine Hanga wilayani Namtumbo,wakiiangalia chini jana wakati wa mdahalo juu ya masuala ya ugonjwa wa ukimwi ulioendeshwa na idara ya maendeleo ya jamii ya halmshauri ya wilaya ya Namtumbo kupitia mpango wake wa elimu ya ukimwi mashuleni uliofanyika shuleni hapo,
Wanafunzi wa shule ya sekondari St Benedictine Hanga wilayani Namtumbo wakimsikiliza mwezeshaji wa masuala ya ukimwi kutoka idara ya maendeleo ya jamii ya wilaya hiyo Peres Kamugisha hayupo pichani wakati wa mdahalo wa siku moja juu ya namna ya kujiepusha na maambukizi mapya ya ukimwi uliofanyika shuleni hapo jana.
PICHA NA MUHIDIN AMRI
Kwa hisani ya Michuzi Blog 

Welcome to Ruvuma Region Tanzania


Along with Mtwara region Ruvuma is the Southern most part of Tanzania Mainland. The region lies between latitudes 9 0 35' and 11 0 45' South of the equator and between longitudes 34 0 35' and 38 0 10' East of Greenwich . It borders the Republic of Mozambique to the South and shares Lake Nyasa with the Malawi Republic to the West. Mtwara Region is to the East. To the North East is Lindi region and in the north the region borders with Morogoro and Iringa regions.

SURFACE AREA AND ADMINISTRATIVE UNITS

Ruvuma region has a total surface area of 67,372 sq. kms. Of this area the water area comprises 3,582 sq. kms. The water area is dominated by some 2,979 sq. kms of Lake Nyasa . Hence, the 603 sq kms of water are scattered throughout the rest of the region. This leaves a land area of some 63,790 sq. kms. The subdivision of the total surface area.
Source: Tanzania Regions Site
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa