SANGA KUWANIA UENYEKITI CCM


na Stephano Chitete, Songea
KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Golden Sanga (Sanga One), ametangaza nia ya kugombea uenyekiti wa chama hicho wilaya ya Songea katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Septemba mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi mjini hapa, Sanga alisema ameamua kugombea nafasi hiyo, ili kurudisha heshima ya chama hicho mjini hapa.
Alisema kila kukicha mvuto wa chama hicho miongoni mwa jamii umekuwa ukipungua kutokana na matendo maovu yasiyokuwa ya kimaadili yanayofanywa na viongozi wake ambayo yamekuwa yakiwakatisha tamaa wananchi na wanachama wa chama hicho.
Alieleza kuwa hali hiyo imesababisha kata 6 kati ya 21 kuchukuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika uchaguzi mkuu mwaka 2010.
Alieleza zaidi kuwa amejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na viongozi wenzake watakaochaguliwa kushika nafasi mbalimbali ndani ya chama kukijenga chama na kuleta ushindi stahiki katika uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2015.
Chanzo: Tanzania Daima



ASKARI WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI MKOANI RUVUMA WAKUTANA

Askofu mkuu wa jimbo la mbinga mkoani Ruvuma John Ndimbo akizungumza wakati wa kikao cha siku moja cha kwa askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Ruvuma kilichofanyikas jana mjini mbinga kilicholengo kuwakumbusha wajibu wao askari hao baada ya kulalamikiwa na jamii juu ya kujihusisha na vitendo vya rushwa kunakosababisha kutokea ajali za barabarani mara kwa mara hapa nchini,katikati ni kamanda wa polisi wa cmkoa huo kamishina msaidizi wa polisi Deusidedit Nsimeki na kulia mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai(Rco) Revocutus Malimi.
Kaimu kamanda wa taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa(Takukuru) wa mkoa wa Ruvuma Hamisi Kidulani akizungumza jana wakati wa kikao cha siku mkoja kwa askari wa kikosi cha usalama barabarani wa mkoa huo,ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka askari hao kupunghuza malalamiko ya wananchi juu ya kujihusisha kwaio na vitendo vya rushwa vinavyopelekea kupindisha sheria za barabarani na kusababisha ajali nyingi hapa nchini.
Kamanda wa poisi mkoani Ruvuma kamishina msaidsizi wa poisi Deusidedit Nsimeki akizungumza na maafisa na askari wa kikosi cha usalama barabarani wa mkoa huo jana mjini wilayani mbinga,katika kikao cha siku moja cha kukumbushana wajibu wao hasa baada ya jamii kuwalalamikia askari hao kutokana na vitendo vya rushwa,kushoto mkuu wa wilaya ya mbinga Senyi Ngaga na kulia mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai(Rco) Revocutus Malimi.
Mmoja wa askari wa kikosi cha usalama bara barani mkoani Ruvuma aliyefahamika kwa jina moja la staff sajent Lilanga akichangia hoja wakjati wa kikao cha siku moja cha kukumbushana wajibu wa kazi kwa askari hao kilichoitishwa na kamanda wa polisi mkoani humo Deusidedit Nsimeki hayupo pichani kilichofanyika jana wilayani mbinga.
Mkuu wa wilaya ya mbinga mkoani Ruvuma,Senyi Ngaga akifungua kikao cha siku moja cha kazi kwa maafisa na askari wa usalama barabarani wa mkoa wa Ruvuma kilichofanyika jjana wilayani humo,kulia kamanda wa polisi mkoani Ruvuma kamishina msaidizi wa polisi Deusdedit Nsimeki.
baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi mkoani Ruvuma wakimsikiliza kamanda wa polisi wa mkoa huo Deusdedit Nsimeki (hayupo pichani) jana wakati wa kikao cha kazi cha siku moja juu ya wajibu kikosi hicho0 hasa baada ya kutuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa vinavyosababisha kuongezeka kwa ajali nyingi hapa nchini.Picha na Muhidin Amri wa Globu ya Jamii,Ruvuma.
Kwa hisani ya Michuzi blog

Local communities in Ruvuma Region urged to embrace Mkuju River Uranium Project





The Mantra Tanzania Community Relations Manager Benard Mihayo (right) stresses a point to the Ruvuma Region District Commissioners who were on a familiarilization tour at the Mkuju River Uranium Project site in Namtumbo District, Ruvuma Region at the weekend.

The Mantra Tanzania Geological Officer Roy Namgera (in white head gear) explains a point to Ruvuma Region District Commissioners who were on a familiarilization tour at the Mkuju River Uranium Project site in Namtumbo District, Ruvuma Region at the weekend. Second from the right (in red cap) is the Namtumbo District Commissioner Abdallah Lutavi
Namtumbo District Commissioner Abdallah Lutavi (in front) leads other Ruvuma Region District Commissioners to the Mkuju River Uranium Project site in Namtumbo District, Ruvuma Region at the weekend. The DCs had gone for a one-day familiarilization tour at the project.

=====  =======  ======= ======

WITH just a few weeks gone after the UNESCO World Heritage Committee accepted Tanzania's request to make changes to the territory of the Selous Game Reserve to pave way for uranium mining, the five District Commissioners within Ruvuma Region have called upon local communities to embrace opportunities that may come by when the project starts.

The UNESCO committee at a meeting in St Petersburg in the Russian Federation that started June 24 to 6 July 2012, committee unanimously approved Tanzania's request to modify the boundary of the game reserve by 0.8 per cent which means that about 200 square kilometers to the south of the Selous, where uranium deposits are found, will also be excluded.

Speaking during a visit to the $400 million Mkuju River uranium mine development project in Namtumbo District, Ruvuma Region at the weekend, the DCs urged locals not to listen to rumors that the project poses a threat to their lives. The Namtumbo District Commissioner Abdallah Lutavi said the project is expected to benefit the whole region in terms of poverty alleviation through jobs that will be created when the project begins.

“Local communities should embrace opportunities that may come by since the project will create a win-win situation. We are sure the good relations between Mantra Tanzania and local communities will persevere,” he said. The Mbinga District Commissioner Senyi  Ngaga said the mineral does not cause any harm in its raw-form urging that the minerals will not be processed in the country but exported.

Earlier the Mantra Tanzania Community relations Manager Benard Mihayo said there is still a challenge for the company to offer jobs to local communities as per the company’s policy since many of them do not have the necessary academic qualifications. “All semi-skilled laborers will come from surrounding communities surrounding the project.  We expect 500 permanent staff and the project will create many jobs in-directly,” he said 

The Mantra Tanzania Geological Officer Roy Namgera the project has life-span of 15 years but the company is still undertaking a research to determine where the project’s life span can take longer. The proposed uranium mine on the Selous Game reserve will give the Tanzanian coffers an annual gross turnover of at least $250 million for 15 years. 

Pinda: Jifunzeni kutoka kwa wawekezaji


Na Amon Mtega, Songea
WANANCHI wa Kijiji cha Lipokela, Kata ya Mbingamhalule wilayani Songea, wametakiwa kuacha kuwa watazamaji kwa wawekezaji na kufurahia fursa zao bali wafanye kazi ya kujifunza kutoka kwao.
Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipotembelea shamba la kilimo cha kahawa la wawekezaji wa Kampuni ya Avivu Tanzania Ltd, lenye ukubwa wa ekari 1,934 lililopo kijijini wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani Ruvuma.

Alisema kunufaika na wawekezaji waliopo, inatakiwa kushikamana nao zaidi kwa lengo la kujifunza namna ya utendaji kazi na hatimaye uchumi utakuwa kwa wote bila kuacha pengo kubwa kati ya mwekezaji na mwananchi mzawa.

“Msipofanya kazi hiyo ya kujifunza changamoto nyingi zitakuwa zinawakabili hasa suala la kipato ambacho huwa kinafikia mahali pakulaumiana kuwa mnaonewa kumbe si kweli bali ni uzembe wa kutokuwa tayari kupata mafunzo kutoka kwa wawekezaji,” alisema Pinda.

Alisema anapenda shamba hilo la wawekezaji liwe pia shamba darasa kwa wakulima wa kijiji hicho na vijiji vya jirani, kwa ajili ya kupata mafunzo hayo kirahisi zaidi na kwa uhakika.

Kwa upande wake, Meneja wa Shamba hilo, Medappa Genepaphy, alisema kampuni hiyo imeweza kutoa ajira kwa watu 5,000.

Alisema wameandaa miche ya kahawa itakayopandwa katika shamba hilo pamoja na kila mkulima wa kijiji hicho atapanda ekari moja ya kahawa katika shamba lake.

Aidha, alisema kampuni hiyo itasaidiana na wananchi katika huduma za kijamii ikiwamo ujenzi wa kituo cha afya na kutoa kompyuta katika shule na hatimaye wanafunzi waweze kupata elimu iliyo bora zaidi.
Chanzo: Mtanzania

Mbinga kutumia ziwa Nyasa kuongeza mapato


Mussa Mwangoka, Mbinga-Ruvuma yetu

UONGOZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma umejiwekea  mikakati  kamambe  ya kuongeza makusanyo ya halmashauri hiyo katika mwaka ujao wa fedha kwa kutumia vyema rasilimali zinazotokana na ziwa Nyasa na kuaanisha   vyanzo kadhaa vya kukusanya kodi.

 Akizungumza katika kikao cha pamoja baina Kamati ya Fedha  na Wataalamu wa Halmashauri hiyo katika ziara yao ya siku nne mkoani Rukwa, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo , Oddo Kiliani Mwisho alisema kuwa  wametumia muda mwingi kujifunza katika eneo la Ziwa Tanganyika mkoani Rukwa  na kubaini dosari kadhaa zilizokuwa zikisababisha kupungua kwa pato la halmashari yao.

 “Baada ya  kufanya  ziara  mkoni Rukwa hususani  katika maeneo  ya  mwambao  mwa  Ziwa Tanganyika tumebaini  dosari  kadha wa kadhaa  ambazo   zimekuwa  zikisababisha  kupungua  kwa pato  katika  Halmashauri  yetu  ya Mbinga” alisema Mwisho

Kwa mujibu  wa  Mwisho ufuatia ziara yao mkoani Rukwa wamebaini kuwa kuna vyanzo vingi vya mapato ambavyo wamekuwa wakivipoteza kwenye Ziwa Nyasa hivyo watatumia maarifa waliyoyapata na kuweka mikakati ya kuboresha ukusanyaji wa mapato kwenye ziwa hilo kama zinavyonufaika Halmashauri za Wilaya ya Sumbawanga na Nkasi kwenye Ziwa Tanganyika.

 Alisema  licha ya kuwa  Halmashauri hiyo ya Mbinga  imeweza kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato kufikia zaidi ya  Sh bilioni 1.8 katika mwaka huu wa fedha unaokwisha lakini bado wanayo nafasi ya kuongeza pato la halmshauri hiyo iwapo watatumia fursa zilizopo kwenye  Ziwa  Nyasa.



 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa