MGAWO WA MAJI WAIKUMBA SONGEA



na Julius Konala, Ruvuma
MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira katika Manispaa ya Songea (SOUWASA) imetangaza kuwapo mgawo mkali wa maji kati ya Agosti na Novemba mwaka huu kutokana na upungufu wa maji katika vyanzo vya mtiririko vilivyopo milima ya Matogoro mjini hapa.
Mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Francis Kapongo, alibainisha hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na akasema kuwa uzalishaji umepungua kutoka meta za ujazo 9,700 hadi kufikia 7,000 kwa siku.
Alisema kutokana na takwimu za vipimo vya maji kwenye mito inatarajiwa maji ghafi yataendelea kupungua na huenda yakapungua zaidi ifikapo Septemba hadi Novemba na kukadiriwa maji hayo kupatikana kwa viwango vya meta za ujazo 5,400 kwa siku, ambayo ni sawa na asilimia 56 ya mahitaji halisi.
''Hali hii imetokana na mvua zilizonyesha mwaka huu kuwa chache, jambo ambalo limesababisha ukame katika vyanzo vinavyotegemewa kutiririsha maji kuelekea kwenye tanki kubwa linalosambaza, kupungua na kupelekea kuwepo kwa mgawo,” alisema Kapongo.
Kutokana na hali hiyo, aliwataka wakazi wa Manispaa ya Songea kuwa wavumilivu katika kipindi hicho na kwamba watahakikisha watapata maji kulingana na ratiba ya mgawo na si vinginevyo hadi hapo mabadiliko ya hali ya hewa yatakapotengamaa.
Pamoja na hayo alisema chanzo cha akiba cha Luhira ambacho kilikuwa kinazalisha meta za ujazo 12,800 kimepungua na kufikia uzalishaji wa meta za ujazo 3,200.


UKISTAAJABU YA MUSSA....NI KWELI YAMETOKEA KIJANA AFUNGA NDOA NA MAMA YAKE MZAZI BAADA YA BABA YAKE KUFARIKI

 Mke na Mume, Bi Condorada Ngonyani (70) na Bw. Joseph Mapunda, ambao ni Mama na Mwanawe, wakiwa nje ya nyumba ya Mganga, wakati walipofikishwa kwa suala hilo la Mama Mzazi na Mwanawe kufunga ndoa.
************************************
 Na Mwandishi Wetu, Namtumbo Ruvuma
MARA kadhaa kumekuwa kukijitokeza matukio mbalimbali ya kustaajabisha, kusikitisha na kutisha na mengine yakihisiwa kuwa ni imani za kishirikina, ambapo mengi ya matukio hayo ambayo hutokea si kwingine ni hapa hapa nchini kwetu, huwaacha watu hoi na maswali mengi yasiyokuwa na majibu.

Kwa mara nyingine tena tukio la kushangaza na kutoaminika kama ni kweli ambalo huwezi hisi kuwa ni la imani za kishirikina, kwani wahusika wote wamefanya hivyo kwa malengo na kuweka wazi sababu za kufanya hivyo japo si sahihi kwa itikadi za kidini, mila na destuli za mtanzania.

Tukio hili ni Mama Condorada Ngonyani (70) mkazi wa mkoani Ruvuma, ambaye aliamua kufunga ndoa na mtoto wake wa tatu wa  kiume wa kimzaa na kuishi naye kinyumba kama mke na mume, ambapo wameonekana wao kama wao kuwa wapo sahihi na kuwashangaa wanadam, majirani zao na Jamii kwa ujumla kuingilia mapenzi yao.

Wananchi wapatao 400, wa mkoa wa Ruvuma walijitokeza kushuhudia kimbwanga hii wakati uongozi wa Serikali ya Mtaa walipoamua kuwafuatilia na kuwahoji na kuitisha mkutano wa wanakijiji na kuwaweka hadharani, ambapo Wananchi wa Mkoa wa huo wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Maendelo ya Jamii, Jinsia na watoto, kufuatilia kwa karibu suala hilo na kuwaondoa hofu wananchi kama kuna sheria inayomruhusu Mtoto na Mama Mzazi kuweza kuishi kindoa.

Alipohojiwa Mama huyo, Condorada Ngonyani, anasealisema kuwa mara tu baada ya kufariki mume wake, Mzee Mapunda, yeye aliamua kumchagua mtoto wake huyo Joseph Mapunda, ili amrithi baba yake katika kuumiliki mwili wake kama ambavyo alikuwa akifanya Baba yake mzazi, ili kuondokana na tamaa na vishawishi wa kiulimwengu.

Alisema kuwa baada ya uteuzi huo walifunga ndoa ya kimila japo kuna baadhi ya wanafamilia hawakufurahishwa na tukio ama jambo hilo, lakini yeye aliamua kufunga masikio na kuamua kuvunja amri ya sita na mtoto wake huyo wa kumzaa.

Tukio kama hili ni mara ya kwanza kutokea kwa mkoa wa Ruvuma na hata kwa Tanzania nzima, ambapo wakaazi wa Ruvuma wamekuwa wakibaki na maswali mengi juu ya tukio hilo na kuhoji Jamii sasa inaelekea wapi kwa baadhi ya Watanzania kuibomoa wenyewe mila na desturi zetu.

Kwa upande wake, Joseph Mapunda, yeye anasema kuwa upendo na mahaba anayoyapata kutoka kwa mkewe huyo ambaye ni mama yake mzazi, hajawahi kuyapata kokote na kusema kuwa wanapendana sana na wanaheshimiana kama mke na mume.

Josepha amehiji kulikoni wanadam kuwafuatilia katika mapenzi yao na kusema kuwa ''hawa watu wanaotufuatilia hadi leo hii kutuweka hadharani namna hii, wanataka nini kwetu?''.

Wananchi hao waliofurika kwa Mganga wa Jadi Flora Ndembo, wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma, wameiomba Serikali kuingilia kati suala hilo na kuchukua hatua kisheria ili iwe fundisho kwa wanatanzani wengine wenye akili kama hizo za kuharibu mila na desturi za kitanzania kirahisi kama hivyo. Picha na Songea Habari
 Bi. Condorada Ngonyani. ''Nawashangaa wanadam kuingilia mapenzi yangu, mtuache''.
 Bwana, Joseph Mapunda, ''Wananchi mtatutakia nini na mapenzi yetu''?

‘DOSARI ZA SENSA ZINATOKANA NA AHADI HEWA ZA SERIKALI’


Mwandishi wetu, Songea-Ruvuma Yetu
 
Wananchi walioshiriki zoezi la Sensa Mkoani Ruvuma wameiomba Serikali kuacha kutoa ahadi ambazo hazitekelezeki kwa kuwa ni moja ya mambo yanayopunguza imani ya wananchi kwa serikali yao hasa katika mambo muhimu kama sense.

Wakiongea kwa nyakati tofauti wakati wa Zoezi la Sensa la kuhesabu watu ambalo linaendelea kufanyika Mkoani Ruvuma wamesema ahadi nyingi zisizotekelezeka ndiyo kero kubwa kwa wananchi.
 
Maruzuku Mohamed Mkaazi wa Manspaa ya Songea amesema ili Serikali iweze kufanya kazi vizuri inapaswa kuwa na Kamati ya kufuatilia ahadi zinazotolewa na Viongozi ili kupunguza tabia ya viongozi kutoa ahadi hewa kila mara.

“Ahadi zimekuwa nyingi kiasi hata wananchi wanashangaa kuona kila kiongozi akitoa ahadi ya kuleta kitu Fulani halafu hawatekelezi ni vizuri kuunda kamati ya kufutilia ahadi za viongozi”
 
 
Vijana walioshiriki Sensa ya watu na Makazi wamesema Serikali ijitahidi kuwapatia ajira Vijana ndipo atakapoona umuhimu wa Sensa.

Vijana wamesema toka tupate uhuru kasi ya ongezeko la watu ni kubwa kutoka watu milioni 9 kabla ya uhuru hadi kufikia watu milioni 40 lakini pamoja na kasi hiyo walio wengi ni vijana na kwamba sensa ni lazima iwajali vijana hao.
 
Blogszamikoa

MAZUNGUMZO TANZANIA, MALAWI YAKWAMA


na Aron Msigwa
WAKATI mazungumzo ya mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa baina ya Serikali za Tanzania na Malawi yakishindwa kupata suluhu, Malawi imetakiwa kusitisha shughuli za utafiti kipindi hiki cha kutafuta muafaka.
Hayo yamebainishwa katika mkutano wa wataalamu na viongozi kutoka serikali za nchi hizo baada ya kushindwa kufikia muafaka uliokusudiwa kuhusu eneo halali la mpaka unaozitenganisha.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha kikao cha usuluhishi kilichohusisha  timu za wataalamu na viongozi wa wizara husika wa nchi hizo kilichomalizika juzi usiku mjini Lilongwe, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe, alisema Tanzania bado ina amini katika mazungumzo ili kufikia muafaka.
Alisema kuwa pamoja na sababu mbalimbali zilizotolewa na Malawi juu ya umiliki wa eneo lote la Ziwa Nyasa, msimamo wa Tanzania uko wazi  kwa kuzingatia vielelezo vya historia vilivyoachwa na wakoloni na sheria za kimataifa kuhusu mpaka kuwa katikati ya ziwa hilo.
Membe alisema kuwa licha ya Serikali ya Malawi kuonesha kila dalili za kukwamisha mazungumzo hayo yaliyoanza kupitia vikao mbalimbali nchini humo, viongozi wa  nchi hizo  kupitia mkutano wa kutafuta suluhu uliomalizika juzi usiku wameamua kuunda timu za wataalamu.
“Licha ya kuwasilisha vielelezo kuonesha uhalali wa mpaka, hatukuweza kufikia muafaka, tumefika mahali pa kuhitaji msaada tuzitume tume za nchi zetu zitoe mapendekezo ya nini kifanyike, maana kuna kila dalili kwamba sisi wenyewe tutashindwa kuendelea zaidi,” alisema.
Alisema kuwa wataalamu kutoka Malawi na Tanzana watakutana Septemba jijini Dar es Salaam ili waweze kutoa mapendekezo ya namna bora ya kuwapata wasuluhishi wa mgogoro huo pamoja na faida na hasara ya njia watakazozipendekeza.
Membe aliongeza kuwa, timu za wataalamu zitakazoundwa zitatoa mapendekezo ambayo yatapelekwa kwa marais wa nchi hizo katika kuelekea hatua ya pili ya utatuzi wa mgogoro huo, ikiwemo kumtafuta msuluhishi au kwenda kwenye mahakama ya kimataifa.
Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Ephraimu Chiume, alisisitiza kuwa licha ya mgogoro huo kuhitaji busara zaidi, bado serikali yake inaamini kuwa mpaka kati yake na Tanzania uko upande wa mashariki mwa Ziwa Nyasa na unatenganishwa na ardhi ya Tanzania.
Alisema kutokana na unyeti wa suala lenyewe na eneo hilo pamoja na historia ya nchi yake, anapenda kuona ufumbuzi ukipatikana haraka ili wananchi wa nchi mbili waweze kuendelea na shughuli zao bila hofu yoyote.
“Ni matumaini yangu mkutano wa Dar es Salaam utakaofanyika Septemba utazaa matunda ili suala hili lipatiwe ufumbuzi, na ikiwezekana tupate msaada wa sheria za kimataifa kwa sababu suala hili liko kisheria zaidi,” alisema Chiume.
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo uliongozwa na Waziri Membe na makatibu wakuu, Patrick Lutabanzibwa (Ardhi), John Haule (Mambo ya Nje) Waziri wa Ardhi, Prof. Anna Tibaijuka na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Patrick Tsere.
Chanzo: Tanzania Daima

MTOTO AFANYA MAPENZI NA MAMA YAKE KWA MIAKA 10, WENYEWE WAISHI KAMA MKE NA MUME

Mwandishi wetu, Ruvuma Yetu 
Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Maendelo ya Jamii, Jinsia na watoto kuingilia kama kuna sheria inayomruhusu Mtoto na Mama yake mzazi kuweza kuishi kindoa.
Hayo yamebainika katika Kijiji cha Namabengo Wilaya ya Namtumbo baada ya Joseph Mapunda kuweza kuishi na Mama yake kindoa kwa miaka 10 mfululizo.
Joseph Mapunda amesema ameweza kuishi kindoa na Mama yake Mzazi baada ya yeye kukubaliana wenyewe yeye na mama yake mzazi kuishi kindoa kama mke na mume.
Alipoulizwa mama anayefahamika kwa jina la Kondrada Ngonyani alikiri kuwa kweli wameishi kindoa kwa miaka 10 na anampenda Mume wake ambaye ni Mtoto wake Joseph Mapunda.
Umati wa watu uliofurika kwa Mganga wa Jadi Flora Ndembo, Namabengo wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma watu wapatao 400 wameomba Serikali ichukue mkondo wa Sheria kuvunja ndoa hiyo.
Kwa Mkoa wa Ruvuma hii ni mara ya kwanza mtoto wa kiume kutembea na mama yake mzazi.
Blogzamikoa

MWANASHERIA WA CCM ACHUKUA FOMU


 Na Amon Mtega, Songea
MWANASHERIA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka makao makuu Dodoma, Glorious Luoga, amejitosa kuchukua fomu ya kuwania ujumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC).

Luoga anawania nafasi hiyo kupitia Wilaya ya Songea vijijini mkoani Ruvuma, huku akiwataka wananchi mkoani hapa kuona umuhimu wa kujitokeza kuchangia shughuli za maendeleo.

Hayo aliyasema juzi wakati akichukuwa fomu ya kugombea nafasi hiyo katika Ofisi ya Katibu wa CCM Wilaya ya Songea Vijijini.

Luoga alisema, kila mwananchi ana wajibu wa kimsingi kuhakikisha kuwa, anachangia shughuli za maendeleo katika eneo analoishi na kuachana na tabia ya kupenda kuchangia harusi.

Alisema wilaya hiyo imekuwa na changamoto nyingi ikiwemo shule za sekondari za kata ambazo nyingi zimekuwa hazina maabara, walimu, vitabu pamoja na madawati.

“Lengo langu la kuchukuwa fomu nikuja kuunga mkono jitihada zilizofanywa na wezee wangu pamoja na Serikali ukizingatia wilaya yetu inachangamoto nyingi.

“Hizi changamoto utatuzi wake sio lazima zikasemewe bungeni kwani mkongojo wa wazee hupokelewa na vijana,” alisema Luoga.

Luoga alisema CCM bado inanguvu kubwa na mfumo wake ni mzuri wa kupambana na vyama vingine vya siasa ambavyo vimekuwa vikijitahidi kujaribu kutaka kukichafua lakini watu wengi wenye uelewa wamekuwa wakikiamini.

Luoga alisema mfumo wa kujivua gamba katika chama hicho ulikuwa na lengo la kukisafisha chama na si vinginevyo, kama baadhi ya vyama vya upinzani vinavyodai kuwa kumejaa mafisadi.
Chanzo: Mtanzania

WATAKIWA KULIPIA UPIMAJI ARDHI

na Stephano Mango, Songea
HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea, Mkoa wa Ruvuma, imewataka wananchi waliopimiwa ardhi yao katika Kata ya Mshangano kwa kutumia Kampuni ya Ardhi Plan, kulipia gharama za upimaji ili wengine waweze kuuziwa maeneo hayo na kuyaendeleza.
Wito huo ulitolewa jana na Diwani wa Kata ya Mshangano, Faustini Mhagama, wakati akiwahutubia mamia ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katani humo.
Mhagama alisema kuwa mradi ulioibuliwa na wananchi wa kata hiyo wa kurasimishiwa ardhi yao umekamilika kwa viwanja 18,000 kupimwa na hivyo wananchi wanapaswa kuvilipia haraka ili viweze kugawiwa Septemba 3, mwaka huu.
Alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutawapa fursa wananchi kuweza kuishi kwenye maeneo yaliyopimwa, pia watatumia maeneo hayo kwa kupata mkopo na kuendesha miradi mbalimbali ya kiuchumi.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mshangano, alisema kuwa gharama za mradi huo zinatolewa na wananchi wenyewe kwa kutoa ardhi badala ya kusubiri.
Chanzo: Tanzania Daima
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa