Ofisi ya CCM Mbinga yachomwa Moto.


1
Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga Anastasia Amasi akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambao hawapo pichani.
2
 Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga Anastasia Amasi akionyesha sehemu iliyoanzia moto kuwaka na kukamata pazia.
4
Kama unavyoona katika picha hapo ni ndani ya ofisi baada ya moto kuwaka.
5
Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga Anastasia Amasi anayeonekana katika picha akitoa  maelezo kwa nje ambapo walimwaga mafuta aina ya petroli dirishani na kuwasha moto.
6
 Huu ni mlango uliomwagiwa mafuta katika upenyo kisha kuwashamoto ambao haukuleta madhara kama walivyo kusudiwa na wachomaji.
Watu wasiojulikana wamechoma moto jengo la ofisi ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma tukio lililotokea Juni 21 mwaka huu majira ya usiku pamoja mlinzi wa ofisi hizo kuwepo katika eneo hilo la ofisi mpaka majira ya saa 12 asubhi  na hakuweza kutambua kutokea kwa kitendo hicho kilichofanywa na watu wasiojulikana usiku huo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga Anastasia Amasi amesema kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Juni 21 mwaka huu ambapo watu wasiojulikana walichoma moto moja ya jengo la ofisi za chama hicho wilayani humo  moto ambao ulielekelezwa katika chumba cha ofisi ya katibu ambapo walivunja vioo na kuchoma moto mapazia lakini kabla hawajachoma vitu vilivyokuwemo ndani walikimbia na kuacha dumu lililokutwa likiwa na mafuta aina ya petroli.
Alisema kuwa mpaka sasa hakuna hisia zozote zinazohusiana na tukio hilo ingawa uongozi wa chama cha mapinduzi wilayani humo umeshatoa taarifa kwenye vyombo ya ulinzi na usalama ambavyo vinaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Katika hatua nyingine hali ya sintofahamu imejitokeza katika uchaguzi wa viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga baada ya halmashauri hiyo kugawanywa na kuzaliwa kwa halmashauri mpya ya wilaya Nyasa kwa kuibuka kwa vitendo vya hujuma vinavyodaiwa kufanywa dhidi ya  mgombea mmoja wa nafasi ya mwenyekiti jina lake kuenguliwa katika mazingira ya kutatanisha na kuzua maswali mengi miongoni mwa madiwani wa halmashauri pamoja na wananchi na kutaka uchaguzi huo usifanyike mpaka majina yote matatu ya wagombea yawepo.
Mmoja wa wananchi wa halmashauri hiyo ya wilaya ya Mbinga ambaye pia ni katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi  wa kata ya Mbinga mjini Monika John alisema kuwa hizo ni dalili za kuwepo kwa njama za wazi za kupanga safu ya uongozi ambao siyo chaguo la walio wengi bali ni chaguo la baadhi ya viongozi wa halmashauri hiyo kwa masilahi yao.
Akizungumzia hali hiyo katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mbinga alisema kuwa uteuzi wa wagombea wa nafasi hizo hufanywa kwa kuzingatia kanuni za chama na wenye jukumu la mwisho  la uteuzi ni uongozi wa chama ngazi ya mkoa  na yeye si msemaji wa maamuzi ya ngazi mkoa ingawa amepokea tarifa ya kusitishwa kwa uchaguzi huo mpaka taarifa nyingine itakapotolewa na ofisi ya chama ngazi ya mkoa.
Picha na Habari kwa hisani ya www.demashonews.blogspot.com

JESHI LA POLISI SONGEA LAKAMATA MENO 18 TEMBO NA NOTI BANDIA



Kamanda wa Polisi Mkoa wa 
Ruvuma Deudedit Nsimeki
 akiwa ameshika noti za bandia 
ambazo zilikamatwa wakati wa 
kuuza mahindi katika soko la 
Sodeko Manispaa ya Songea
Haya  ndio meno ya tembo 
ambayo yamekamatwa katika 
kijijicha Hanga yakiwa meno
 18 ambayo yalikuwa 
yakisafirishwa kwenda Dar es salaam
Kweli watu  hawana huruma
 hayo ni meno ya tembo
 wadogo ambao walikuwa 
wakitegemewa kuwa watakuwa
 rasilimali ya taifa lakini
 masikini wawindaji haramu
 wamekatisha maisha ya tembo hao
Noti bandia zilizokamatwa 
Manispaa ya Songea katika
 soko la Sodeko, kwa mujibu wa
 kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma 
Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma 
limefanikiwa kukamata Vipande
18 vya Meno ya Tembo vikiwa 
kwenye Mfuko wa Salfeti. 
Kamanda wa Polisi Mkoa 
wa Ruvuma Deusdedit Nsmeki 
amefanikisha kukamatwa kwa meno
 ya Tembo vipande 18 vikiwa 
kwenye Mfuko wa Salfeti maeneo 
ya Hanga Misheni wilaya ya Namtumbo


PICHA NA SONGEA HABARI

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa