Mbambabay wapata boti mpya

UMOJA wa wakazi wa wilaya mpya ya Nyasa, mkoani Ruvuma, waishio jijini Dar es salaam, umetoa msaada wa boti moja yenye thamani ya sh milioni 16 kwa wananchi wa Mbambabay wilayani humo kwa ajili ya kuendeshea shughuli za uvuvi wa kisasa.
Boti hiyo ilikabidhiwa mwishoni mwa wiki na mwenyekiti wa umoja huo Cassian Njowoka, kwa mkuu wa wilaya ya Nyasa Ernest Kahindi ili litolewe kwa kikundi kimojawapo ambacho kinajishughulisha na shughuli ya uvuvi kwa madai kwamba mapato yatakayopatikana yaweze kununulia boti nyingine ambayo itagawiwa kwa kikundi kingine.
Njowoka alisema kuwa lengo la chama chao ni kuhakikisha kila kikundi cha uvuvi kinapata boti ya kisasa kwa lengo la kuongeza ufanisi katika shughuli zao tofauti na ilivyo sasa ambapo wanaendesha uvuvi wa hatari wa kutumia mitumbwi ambayo wakati wa dhoruba inashindwa kuhimili na kusababisha maafa kwa wavuvi.
Alisema mpango wa chama hicho ni kuhamasishana juu ya kuwekeza wilayani humo na kusaidia nyanja mbalimbali ikiwemo vikundi vya vijana wanaofanya shughuli ya uvuvi, kilimo kwa kugawa miche ya kahawa kwa kila mwananchi ambaye ana shamba ili waondokane na dhana ya kutegemea uvuvi peke yake.
Njowoka aliendelea kusema kuwa endapo wananchi hao watalitumia boti hilo ipasavyo na kurejesha mapato kwa uaminifu walao kila wanapofikisha shilingi milioni saba, watakuwa tayari kusaidia tena boti moja kwa ajili ya kuviwezesha vikundi vingine.
Aidha chama hicho kina mikakati mbalimbali katika kuboresha sekta ya elimu wilayani humo ikiwa ni pamoja na kuanzisha Shule ya Sekondari ya Wasichana Lituhi ambayo itakuwa na kidato cha kwanza hadi cha sita.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Ernest Kahindi, alikipongeza chama hicho kwa msaada wake na kusema kwamba ni cha kizalendo na kwamba wilaya itajenga karakana ya boti ili wakazi wa mwambao mwa Ziwa Nyasa wapate fursa ya kutengeneza na kujifunza juu ya uvuvi wa kisasa.
Imeandikwa na Julius Konala, Ruvuma
Source: Tanzania Daima

POLISI RUVUMA WAKAMATA MENO YA TEMBO WILAYANI TUNDURU



Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki akiangalia pembe zilizokamatwa
——————————————–
JESHI la polisi mkoani Ruvuma kwa mara nyingine limefanikiwa kukamata nyara za serikali katika wilaya ya Tunduru tukio ambalo limetokea Julai 21 mwaka huu majira ya saa 11:40 alfajiri lililotanguliwa na tukio jingine lililotokea Juni 26 mwaka huu ambapo jumla ya meno 18 ya tembo yalikamatwa wilayani humo kwa ushirikiano wa jeshi la polisi na idara ya wanyamapori pamoja na wananchi wanaotoa taarifa za siri kwa vyombo hivyo vya ulinzi na usalama.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki amesema kuwa sik hiyo ya tukio askari polisi waliokuwa doria walifanya upekuzi kwenye mabasi yaliyokuwa yakianza safari alfajiri katika kituo kikuu cha mabasi cha mjini Tunduru ambapo katika basi moja lenye namba za usajili T315ABS aina ya Scania mali ya kampuni ya WAHIDA  walifanikiwa kukamata sanduku moja likiwa na nguo pamoja na vipande 21 vya meno ya tembo
Amesema kuwa vipande hivyo vya meno ya tembo vilikuwa na uzito wa kilogramu 34.45 na thamani yake ikiwa ni dola za kimarekani 189,475 sawa na fedha za kitanzania shilingi 30,316,000na mkia mmoja wa tembo na walipoendelea kufuatilia katika mizigo hiyo walibaini kuwepo kwa tiketi moja ya kusafiria  abiria ikiwa na namba zilizofutwafutwa na walipofuatilia kwenye kitabu cha tiketi waligundua kuwa tiketi hiyo ilikuwa imesajiliwa kwa jina moja tu
Na askari walipoendelea kufuatilia ilionekana abiria mwenye tiketi hiyo na mizigo hiyo iliyotiliwa mashaka aliamua kuitelekeza mizigo yake baada ya kuwaona askari polisi wakiwa kwenye upekuzi wa mabasi na hivyo mtu huyo hakuweza kufahamika na jitihada za polisi kwa kushirikiana na wananchi za kumtafuta zinaendelea ili aweze kufikishwa mahakamani .
Aidha kamanda Nsimeki ameendelea kuwaomba wananchi na raia wema kuendelea kutoa ushirikiano mwema kwa jeshi la polisi katika harakati za kuzuia biashara hiyo haramu inayoendelea kuhujumu uchumi wa taifa.
Katika tukio jingine lililotokea katika kijiji cha Langiro wilayani Mbinga mkoani Ruvuma  kamanda Nsimeki amesema tukio hilo lililotokea Julai 22 mwaka huu majira ya saa 7 usiku ambapo  mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Peter Kapinga(19) aliuawa baada ya kupigwa na mti kichwani na watuhumiwa wa tukio hilo ni Ingo Kapinga na Elias Kapinga ambapo chanzo niugomvi uliotokea kwenye disko na  ugomvi wao huo  ulisababisha kifo kwa sababu ya wivu wa kimapenzi ulioanzia kwenye muziki huo amba baada ya tukio hilo mtuhumiwa mmoja Inigo Kapinga alitoroka na mwenzake Elias Kapinga(14) alikamtwa na anahojiwa na polisikuhusina na tukio hilo.
Habari kwa hisani ya demashonews.blogspot.com

SHUJAA WA TANZANIA ALIYEFIA DARFUR RODNEY NDUNGURU AZIKWA KWAO SONGEA


 Asikari wa JWTZ wakiwa wamebeba mwili wa Rodney Ndunguru
Aliye kaa katikati ni mama wa marehemu Rodney Ndunguru
 Askari wakiwa wamebeba mwili wa marehemu Rodney Ndunguru wakati wakielekea  katika makaburi ya Mjimwema
 Umati wa watu uliojitokeza katika mazishi ya Rodney Ndunguru katika makaburi ya  mjimwema jana
 Mwili wa Rodney Ndunguru ukiingizwa katika kaburi
 Mama wa marehemu Rodney Ndunguru akiweka taji katika kaburi la mwanaye
---------------------------------------
Na Cresensia Kapinga,Songea.


SIMANZI ,Vilio,majonzi  vimetawala wakati wa mazishi ya askari wa Jeshi la Wananchi Rodney Ndunguru wa kikosi cha makomando cha 92 KJ Ngerengere mkoani Morogoro ambapo mamia ya wakazi wa Mkoa wa Ruvuma wakiwemo askari wa Jeshi la wananchi ambao walihudhuria mazishi yaliyofanyika jana kwenye makaburi ya Mjimwema Manispaa ya Songea.

Katika mazishi hayo ambayo yaliongozwa na Paroko wa kanisa katoriki jimbo kuu la Songea parokia ya Mjimwema padre Noel Duwe ambaye wakati  akiendesha ibada ya mazishi aliwaonya Watanzania kutochezea amani  na kwamba utulivu walionao watanzania unahitajika kulindwa kwa namna ya aina yeyote na si vinginevyo.

Padre Due alisema kuwa kwa wale wote wanaotaka kuchezea amani na utulivu tulionao wanapaswa kukemewa kwa nguvu zote kwa kuwa watanzania hatujazoea vurugu wala umwagaji wa damu jambo ambalo lilionekana kuvuta hisia kwa watu waliofika kuomboleza msiba hu.

Aidha Padri Due alimfagilia waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano Mizengo Pinda kwa kauli yake aliyoitoa Bungeni kuwa kuwa jeshi la Polisi lihakikishe kuwa linawadhibiti watu wanaoleta fujo kwa kupiga na kwamba kauli yenye agizo hilo inapaswa kuungwa mkono kwa nguvu zote badala ya kuibeza kwa kuwa hivi sasa watu wengi wamekuwa wakidharau vyombo vya Dola  wakizani kuwa serikali haipo.
Kwa upande wake  Kaimu wa Brigedi ya kanda ya kusini Kanari George Msongole alieleza kuwa taarifa ya kifo cha Rodney ilipokelewa muda mfupi baada ya kifo chake na kuwa Jeshi la wananachi linaungana  na familia ya marehemu katika majonzi na msiba mzito.

Kwa upande wake msemaji wa Familia ya Marehemu Rodney Ndunguru amesema kuwa  familia imepata pengo kubwa kwa kuondokewa na kijana wao ,na ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuisaidia  ili waweze kujengewa nyumba ambayo itwasaidia kwa kuishi mama yake mzazi na mjane.
Alisema kuwa Rodney Ndunguru amefariki akiwa na miaka takribani miaka saba kazini na akiwa na umri wa miaka 28 ambapo kimsingi kifo chake kimeacha pengo kubwa katika famila kwani katika uhai wake ilikuwa farja kwa ndugu na jamaa.
Rodney Ndungu amezikwa saa 10:45 jioni kwenye makaburi ya mjimwema ambako mamia ya wakazi ya mkoa wa Ruvuma walihudhulia akiwemo mwakilishi wa mkoa wa Ruvuma Saidi Mwambungu ambaye ni katibu tawala ya wilaya ya songea Joseph Kapinga na kwamba mazishi yaliendeshwa kijeshi ambapo askari wote walikuwa wamevaa sare huku wakifunga vitambaa vyeusi kwenye mikono yao. 

habari kwa hisani ya demashonews.blogspot.com

Barabara ya Songea, Tunduru-Mtwara kuanza kujengwa

MKOA wa Ruvuma utakuwa na fursa nyingi za kiuchumi na maendeleo mara baada ya kufunguka kwamtandao wa barabara ndani yakipindi kifupi kijacho ambapo  kilometa 1,500  za kutoka Songea, Tunduru hadi Mtwara zitakuwa zimejengwa kwa kiwango cha lami kwa kipindi cha kuanza mwaka huu wafedha wa 2013/14.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, Mizengo Pinda wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma,katika mkutano wahadhara wakati akiwa katika ziara ya siku nane ya kukagua shughuli za maendeleo za mkoa huo.

Pinda amesema kwasasa mkoa huo unamiradi mingi ya barabara ambayo ipo katika hatuaza mwisho za upembuzi wa kina na hivyo muda si mrefu ujezi wa barabara hizo utaanza.

Amesema barabaraya Songea hadi Namtumbo ambayo ni ya kilometa 73 kwa sasa ipo katika hatua ya mwisho kabisa ya umaliziaji baada ya kuweka lami na  ndani ya miezi michache itakabidhiwa kwa serikali.

Aidha Pinda amesema kwamba, Mkoa wa Ruvuma pia utaungani shwana Mkoawa Mtwara kwa ujenzi wa barabara ya Tunduru hadi Mangaka yakilometa 140, ambapo fedha zake zipo tayari ambazo zinato kaufadhili kutoka benki yamaendeleo ya Afrika na ujenzi wake utaanza mwezi ujao wa Agosti.

OCD MBINGA ALALAMIKIWA NA ASKARI

      
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEivD3fZqaty8yE_pL8Pvs2kK8PVIJ_ToW83JGmb4vzSmY6H61XqLI1Xdita4Lv-gMiNCBSgQbNi841xShX_SmPYCo7XCmwYnX9T3YKtQkLCzzOc_BS8jE35dWPYruGRPYTimHC_FD8HDpI/s1600/Police1.jpg

Na Muhidin Amri–Mbinga
BAADHI ya askari polisi wa kituo kikuu  Mbinga mjini,wamemtuhumu mkuu wa polisi wa wilaya hiyo(OCD)Jastine Joseph kuwa ni mtu anayetumia madaraka yake vibaya kwa kuendesha manyanyaso dhidi ya askari wa vyeo vya chini na kumuomba Mkuu wa jeshi ilo Said Mwema kumuondoa haraka kabla ya hali haijawa mbaya zaidi.
 
Wakizungumza na mtandao huu  kwa masharti ya kutotajwa majina yao,askari hao wamelalamika kuwa OCD wao amekuwa akitoa lugha za dharau na hata  zisizopendeza kwao hali inayowavunja moyo wa kazi askari wengine katika wilaya hiyo.
 
Walisema,iwapo jeshi litashindwa kumuhamisha Jastine kunaweza kutokea maafa makubwa kwani hawatoweza kuvumilia vitendo vinavyofanywa na afisa huyo hasa ukizingatia kuwa na wao ni watu wakubwa tena wenye familia kama yeye hivyo kitendo cha kuwatolea lugha za kiuni ni sawa na kuwadhalilisha.
 
Aidha wameshauri hata maafisa wengine katika wilaya hiyo wanatakiwa kuondoka kwani wameshaaka Mbinga kwa muda mrefu hivyo ni vema kupelekwa katika maeneo mengine ya nchi ili wakapate changamoto mpya za utendaji wa kazi, na kuendelea kuwepo katika wilaya hiyo ni tatizo kubwa kwani wameshafahamika na watu wengine hali inayowafanya kushindwa kuchukua maamuzi sahihi.
 
Wamesema ocd wao ni mtu hasiyetaka ushauri kutoka kwa mwingine hata kwa maafisa wenzake jambo linalomfanya kutengwa na kujikuta na yuko pekee yake au na wale askari wa kabila lake tu jambo lililowafanya askari kuwepo katika makundi hasa baada ya kufika Jastine kitu ambacho siku za nyuma hakikuwepo na askari wote walikuwa ndugu moja wakiishi na kusaidiana tofauti na sasa.

“huyu mkuu wetu ni tatizo kubwa,sijui hata mtu aliyempendekeza kuwa OCD ametumia kigezo gani,hafai kabisa yeye  kazi yake ni majungu tu na sio vinginevyo”alisema mmoja wa askari hao.
 
Kwa upande wake Jastine alikanusha tuhuma hizo na kuziita kuwa ni unafiki unaofanywa na askari wachache waliozoea kula rushwa kila mara hasa kwa waendesha pikipiki jambo ambalo yeye hataki kusikia katika uongozi wake.
“hizo tuhuma sio za kweli,zinafanywa na baadhi ya askari wngu hasa wale wala rushwa,nimeshaelekeza wakikamata pikipiki waje na faini hapa au mmiliki wake sio kuleta pikipiki hatuna eneo la kupaki kwani hizi tulizonazo ni nyingi na hatuna sehemu ya kuzipeleka”alisema.
 
Naye Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki alikiri kuwepo kwa malalamiko  ya askari wa vyeo vya chini dhidi ya OCDwao na kuhaidia kuwa atashughulikia tuhuma hizo ili kupata ukweli wa jambo ilo.
“sisi hatufanyi mambo kwa kukurupuka tu lazima tufanye uchunguzi  ili tujiridhishe,unajua ukishakuwa kiongozi unatakiwa kuwa makini  hasa  katika maamuzi ili usifanye mambo kwa kumuonea mtu lazima utende haki kila wakati”alisema RPC

Dawa ya waharibifu wa mazingira Ruvuma imeiva

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu amesema mtu yoyote atakaye haribu vyanzo vya maji au kutumia Maji ovyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu ameya sema hayo wakati wadau mbalimbali wa Bonde la Mto Ruvuma na Pwani ya Kusini kujadili jinsi ya kukabiliana na Majanga yanayo sababisha kiwango cha maji kushuka.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu amesema kiwango cha uharibifu wa mazingira katika mkoa wa Ruvuma una zidi kuongezeka kwa watu kilima katika vyanzo vya maji pamoja na kutumia maji bila kibali cha Maafisa wa Bonde la mto Ruvuma , watu hao wakibainika wata kamatwa na kufikishwa kwenye vyombo kisheria

 Afisa wa Maji Katika Bonde la Mto Ruvuma na Pwani ya Kusini.  Masaru Razaro Msengi amesma kiwango cha maji katika Mito na hata upatikanaji  wa Mvua mkoani Ruvuma umepungua kutoka milimita 1200 za mwaka 2010  hadi kufikia milimita 600 kwa mwaka 2013 hii ina tokana uharibifu wa mazingiza.

Mwenyekiti wa Halimashauri ya wilaya ya Nyasa Odo Mwisho katika kukabiliana na upungufu wa mvua ha sa baada ya wananchi kugeuza makaazi katika milima ya Lingistone na kusababisha uharibifu wa Mazingira amewataka wananchi hao kuondoka mara moja katika milima hiyo

 Mkoa waRuvumaumekabiliwanaUharibifuwa Mazingira Kwananchi kuvamia vyanzo vya Maji na kuvigeuza vya kilimo cha Mabondeni na Wenginekuchoma Moto ili kuwinda wanyama wa dogo kama sungura.

Vijana watakiwa kuendelezwa

VIJANA wanatakiwa kuendelezwa katika fani zao za kitaaluma na shughuli wanazopenda kuzifanya katika maisha yao ili waweze kujipatia maendeleo. Wito huo, umetolewa jana na Mratibu wa Mradi wa Shirila la Resteless Development mkoani Ruvuma, wakati akiwakaribisha vijana kutoka vyuo mbalimbali kwenye mdahalo uliyoandaliwa na shirika hilo huku.
Mdahalo huo, ulikuwa na mada ya vijana wanajitambuaje na wasaidiwaje ili waweze kukabiliana na changamoto zinazo wakabili katika maisha yao.

Alisema ili vijana waweze kumudu kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika maisha, ni lazima sekta za umma na za watu binafsi ziweze kutoa misaada ya kielimu ya kukabiliana na changamoto hizo.

Alisema kufuatia shirika hilo ambalo linafanya kazi na vijana katika nchi 11 ulimwenguni,limebaini vijana wengi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hasa za upande wa ajira, pindi wanapohitimu elimu zao.

Kwa upande wa watoa mada, Lawrence Ambokile alisema vijana wengi wanakata tamaa maisha kwa sababu hawajapewa elimu ya kujitambua.

Alisema jamii, inawategemea vijana kutoka vyuo vikuu hivyo inatakiwa iwalinde na kuwapa mawazo mazuri ambayo yatakuwa msingi wa maisha yao.

CHANZO: MTANZANIA GAZETI

Watoto Ruvuma waomba kutunzwa

WATOTO mkoani Ruvuma wanaoishi katika mazingira magumu wametoa wito kwa kampuni na jamii kutowasahau kutunzwa na kuwatembelea. Kauli hiyo waliitoa mjini hapa hivi karibuni katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kwa mwaka 2013 baada ya kutembelewa na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania.


Watoto hao waliomba wadau kuiga mfano wa Vodacom Tanzania kwa kuwa itakuwa changamoto kwao kuweza kutimiza yale yanayotarajiwa kutoka kwao na hatimaye kuwa Watanzania wenye ari ya kuleta maendeleo na mafanikio chanya katika Taifa.

Wafanyakazi hao walifika hapo kwa lengo la kuwaona na kuwafariji na kutoa msaada wa kilo 100 za mahindi, sabuni na mafuta ya kujipaka pamoja na viburudisho kwa watoto wanaolelewa katika kituo hicho chenye watoto 64.

Akizungumza katika makabidhiano ya msaada hiyo, Meneja wa Vodacom Ruvuma, Michael Kipuyo, alisema wameona ni kipindi kizuri kuwakumbuka watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwa ajili ya kuwasaidia nao wajisikie ni sehemu ya jamii inawajali.

“Vodacom tunajali wateja wetu wa sasa na wale wa baadaye kwa kuwa kwa kusaidia watoto hawa tunasaidia jamii na Serikali kulea watoto watakaouja kuwa ni nguvu kazi ya Taifa hapo baadaye katika mazingira ya amani na hatimaye kuwafanya wajisikie kuwa ni sehemu ya jamii,” alisema Kipuyo.

Watoto hao waliwashukuru wafanyakazi hao kwa kuwakumbuka katika kipindi hiki ambapo Afrika inaadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika na kuwakumbuka wale waliofariki katika kudai haki zao kule Afrika ya Kusini mwaka 1976.

Waliomba wadau kuiga mfano wa Vodacom Tanzania kwa kuwa itakuwa changamoto kuwa Watanzania wenye ari ya kuleta maendeleo na mafanikio chanya katika Taifa.

CHANZO: GAZETI LA MTANZANIA
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa