MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA (PSPF) : TARATIBU WA KULIPA MICHANGO KWENYE MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI (PSS)



MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA
(PSPF)

TARATIBU WA KULIPA MICHANGO KWENYE MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI (PSS)
Mfuko wa Pensheni wa (PSPF) unapenda kuwataarifu wanachama wake wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari juu ya mabadiliko ya akaunti za malipo kama ifuatavyo:-
1.    JINA LA AKAUNTI: PSPF SUPPLEMENTARY SCHEME
2.    JINA LA BENKI: CRDB
·         Akaunti na. 0150237443000 kwa fedha za kitanzania
·         Akaunti na. 0250237443000 kwa Fedha ya kigeni (Dola)
·          
3.    JINA LA BENKI: NMB
·         Akaunti na. 20110006364 kwa fedha za kitanzania
Pia unaweza kuwasilisha michango yako kwa kutumia mitandao ya simu.
MUHIMU: Kumbuka kutaja namba yako ya uanachama kila unapolipa michango benki au kwa njia ya simu.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu na. 0783 481 344  au 0758 500 701.
“KARIBUNI WOTE MJIUNGE NA PSPF”
Mkurugenzi Mkuu

Serikali yakipongeza Chuo cha St. Joseph

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa amekipongeza Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph, tawi la Songea, mkoani Ruvuma, kwa kufundisha masomo ya sayansi kwa kuwa itapunguza uhaba wa wataalamu wa kada hiyo.
Dk. Kawambwa alisema hayo mjini hapa jana wakati wa mahafali ya nne ya chuo hicho yaliyohudhuriwa na viongozi wa vyama vya siasa, serikali, wazazi wa wahitimu na wananchi mbalimbali.
Alieleza kuwa anathamini mchango unaotolewa na chuo hicho kwa kuwa nchi yoyote haipati maendeleo bila wataalamu wa sayansi hivyo ameuomba uongozi wa chuo hicho kuongeza udahili wa wanafunzi hao.
Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho Tanzania, Dk. Arul Raj, alimwomba waziri huyo kuangalia uwezekano wa serikali kutoa mikopo kwa wanafunzi wa stashahada badala ya mikopo hiyo kutolewa kwa wanafunzi wa shahada peke yake kwa vile baadhi yao wanashindwa kumudu gharama za masomo.
Naye Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Joseph Mkirikiti, aliwataka wazazi kuwahimiza vijana wao kujiunga na chuo hicho ili wapate ujuzi utakaowawezesha kujiajiri na kulifanya taifa lipige hatua ya maendeleo tofauti na ilivyo sasa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chuo hicho Askofu John Ndimbo wa Jimbo Katoliki Mbinga ameipongeza serikali kwa ushirikiano katika ufanisi wa chuo hicho kwa madai kwamba bila ya kupata ushirikiano huo wasingefanikiwa.
Katika mahafali ya chuo hicho kilichoanzishwa mwaka 2004 wahitimu 96 wa masomo ya sayansi ya kompyuta walitunukiwa vyeti.
Chanzo: Tanzania Daima

Mabishano yatawala kikao cha kupanga Bei ya korosho



Ruvuma
Mkutano wa Wadau wa Korosho umetangaza bei ya korosho kwa msimu wa mwaka 2013/14 kwa Sh. 1,000 kwa kilo kwa daraja la kwanza na daraja la pili Sh. 800 baada ya wadau kubishana na wabunge.

Bei ilitangazwa rasmi kuanza kwa msimu wa ununuzi wa zao hilo kuanzia mwezi huu katika mkutano huo uliohudhuliwa na wadau hao wakiwamo wabunge wa mikoa ya  kusini .
Wadau hao walipinga bei hiyo na kupendekeza korosho kuuzwa kwa Sh, 1,200 na kupingwa vikali na wakulima.

Kikao hicho kilichowashirikisha wanasiasa hususani wabunge wakionekana kupigia debe bei ya Sh. 1,200, huku wakulima  wakihofia  endapo korosho itauzwa kwa bei hiyo huenda wakajikuta katika wakati mugumu kwa kushindwa kulipwa fedha zao kama ilivyokuwa kwa msimu uliopita.

Mkulima wa korosho wa Kijiji cha Maundo Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara, Abdul Chinemba, alisema bei iliyopitishwa mwaka jana imewasababishia baadhi yao kukosa malipo yao hadi sasa huku akishauri korosho kuuzwa kwa Sh.1,000, ambayo itamwezesha mkulima kulipwa fedha zake bila kukidai chama cha msingi.

Mkulima kutoka Wilaya ya Nanyumbu mkoani humo, Fatuma Chisanga, aliomba mkutano huo usiendeshwe kisiasa huku akitoa angalizo kutorudia makosa yaliyofanywa katika mkutano uliopita.

Awali akitangaza bei dira ya zao hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Mfaume Juma, alisema kuwa bodi hiyo ilipendekeza korosho kuuzwa kwa Sh. 800 kwa kilo kwa daraja la kwanza na la pili Sh. 600.

Mbunge wa Tunduru, Mtutula Mohamed Mtutula, alimuomba  Mwenyekiti wa wadau hao, Hemed Mkali kuwachunguza  waliopendekeza bei dira hiyo.

“Mwenyekiti wewe ni mwanasiasa wa siku nyingi, naomba hawa watu waliopendekeza bei hii wachunguzwe kama kweli wanamapenzi ya dhati, nikisema hivi naamini hata wewe unaelewa kwa kuwa unatambua ninamaanisha kitu gani. Sina imani na hawa watu waliopitisha bei dira na wala sidhani kama wanatutakia mema, ” alisema Mtutula.

Mbunge wa Newala ambaye pia ni Waziri wa  Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Geogre Mkuchika, alishauri mkutano huo kutopunguza bei hiyo huku akihofia endapo  mkutano huo utapitisha bei ya Sh. 1,000, utasababisha matatizo makubwa kwa wananchi wao.

Baada ya  vuta nikuvute hiyo, Mwenyekiti wa wadau alipata wakati mgumu na kupendekeza wadau kupiga kura ili kufahamu bei wanayohitaji katika msimu huu.

Baada ya kupigwa kura, wadau hao walipendekeza bei korosho kuuzwa kwa Sh. 1,000  hivyo wabunge kujikuta wakishindwa.

 
CHANZO: NIPASHE


Kesi za mauaji 37 kusikilizwa


Ruvuma
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania kanda ya Songea mkoani Ruvuma imeanza vikao vyake katika vituo viwili tofauti Songea na Mbinga ambapo kesi 37 za mauaji zitasikilizwa.
Msajili wa wilaya mahakama kuu Tanzania kanda ya Songea Wilfred Nyansobera alisema kati ya kesi hizo zitakazosikilizwa zipo ambazo maelezo ya awali na ushahidi utasikilizwa.
Nyansobera alisema kikao cha kwanza kitaendeshwa na Jaji Patricia Fikirini akisaidiana na wakili mkuu mfawidhi wa serikali kanda ya Songea Andikalo Msabila na wakili wa kujitegemea Christandus Komba na Frank Ngafumika.
Alifafanua kuwa katika kikao hicho cha kwanza jumla ya kesi 16 zimepangwa ikiwa 12 zitasikilizwa maelezo ya awali na nne zitasikilizwa ushahidi.
Alisema kikao kingine kitaendeshwa na Hakimu Mkazi Mkuu Wilfred Dyansobera akisaidiana na wakili wa serikali Okoa Mgavilenzi na wakili wa kujitegemea Dickson Ndunguru ambapo kesi 10 zimepangwa ikiwemo nne za wauaji kwa ajili ya kusikiliza ushahidi na sita rufaa za jinai.
Kikao kingine kinaendeshwa Mbinga na Jaji mfawidhi kanda ya Songea Mwanaisha Kwariko ambapo jumla ya kesi 11 zimepangwa ikiwa kesi tano za mauaji zitasikilizwa ushahidi na kwamba kesi tatu ni za rufaa za jinai huku zingine tatu zikiwa ni maombi na rufaa ya kesi za madai.
Chanzo: Tanzania Daima

Wakulima Korosho Walalamikia mfumo wa soko la zao hilo



Ruvuma

WAKULIMA wakorosho wameitaka serikali na wadau wa sekta ya korosho nchini kushughulikia kero zilizo katika mfumo wa soko la zao hilo ili liweze kumnufaisha mkulima na kuongeza tija. 

Hatua hiyo inatokana na zao hilo kushindwa kutoa mchango stahiki kupunguza mzigo wa umaskini kwa wakulima wa zao hilo linalotoa mchango mkubwa katika pato la taifa na kuingiza fedha nyingi za kigeni.

Wakichangia mada ya DHANA YA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI iliyowasilishwa katika mkutano wa wadau wa sekta ya zao la korosho baadhi ya wakulima hao ndg Ally Maneno wa Pwani,Nicodemas Wilson wa Lindi na Zainabu Kalikalanje wa Ruvuma wamesema swala la upotevu wa korosho katika maghala ya wanunuzi ni changamoto kubwa ambayo isiposhughulikiwa inakatisha tamaa wakulima.

Wamesema kinachoendelea katika mfumo wa soko la korosho ambapo unyaufu unafikia asilimia 25 ya korosho zinazotunzwa katika maghala ni wizi ambao unsipoangaliwa utaua sekta ya kilimo cha zao hilo hapa nchini.

Kumekuwepo na upotevu wa korosho zinapokuwa katika maghala kusubiri bei ya soko mnadani ambao umekuwa ukichukuliwa kama unyaufu madala ya upotevu ambao unepelekea wahusika kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Kisayansi unyaufu unaoruhusiwa katika zao la korosho ni kati ya asilimia 0.9 kwa kipindi cha mwezi mmoja hadi asilimia 1 kwa kipindi cha miezi sita.

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa