TUANGALIE FURSA KUTOKA MKOANI RUVUMA: UJUE MTO RUVUMA AMBAO NI CHANZO KIKUBWA CHA MAPATO KWA JAMII INAYOISHI KANDO KANDO YA MTO HUO


Mto Ruvuma unavyo onekana kwa juu 

 Hawa ni Vijana wa Ruvuma maarufu kwa WAYAO  wakijitifautia ridhiki  katika mto Ruvuma , Kila pikipiki moja huoshwa kwa Shilingi Elfu moja(1000) wanapokuwa wanaosha mafuta husambaa katika maji . Je kwa hali hii kuna matumizi mazuri ya vyanzo vya mto Ruvuma ikiwa  mbele yake watu hutumia maji haya kwa matumizi ya nyumbani(kupikia na kunywa)   Pia mto huu huumwaga maji yake katika Mto RUVUMA
 
Hawa ni akina mama wakifua nguo katika mto huu wa Ruvuma na pembeni kukiwa na mtoto anayechezea maji ,pengine mtoto huyu uwenda akawa anachota kwa mikono yake na kunywa
 Hii ndiyo hali halisi ya chanzo cha  mto Ruvuma ulipo Ruvuma kwa WAYAO ukiwa umeanza kukauka maji kutokana na matumizi mabaya ya vyanzo vya maji kwa kupitisha mifugo kiholela na ulimaji pembezoni mwa mto,

 Bibi(MBUYA) akisuuza nguo baada ya kufua katika mto Ruvuma huku mjukuu wake akitelemka kumfuata ndani ya maji
 Vijana wakiwa kazini kuelekea katika kuvua samaki

Baadhi ya watalii pamoja na watu mbalimbali ambao ni wakazi wa pembezoni mwa mto huo wakitazama mambo mbalimbali pamoja na kununua Samaki

Hapo mwaka 1886, Askofu wa Kanisa la Anglikana, Charles Alan Smythies, alikuwa MZUNGU sio mtu wa Kwanza kuona chanzo cha mto RUVUMA. Inaelezwa kuwa Askofu huyu alifika katika chanzo cha mto Lujenda, naodaiwa kuwa chanzo muhimu cha mto Ruvuma.
Inasemekana kwamba wakati askofu huyo alipokiona chanzo hicho, uvumi ulienea miongoni mwa wenyeji kwamba kwa vile chanzo hicho kilikuwa na MASHETANI basi Askofu Smithies angekufa. Hata hivyo askofu huyo hakufa kama ilivyohofiwa.

Vile vile yafaa kukumbushana hapa kwamba Askofu Charles Allan Smithies ndiye alikuwa askofu wa kwanza wa UMCA (University Mission to Central Africa) – ya Anglikana visiwani ZANZIBAR hapo mwaka 1892
 

Wadai kutonufaika na rasilimali za taifa

WATU wenye ulemavu wilayani Namtumbo, Ruvuma wamedai rasilimali za taifa zinawanufaisha zaidi watu wasiokuwa na ulemavu  ukilinganisha na watu wenye ulemavu.
Walitoa madai hayo kwenye mafunzo yaliyotolewa na shirika lisilo la kiserikali la kuwaendeleza watu wenye ulemavu na yatima (SHIKUWATA) kwa ufadhili wa The Foundation For Civil Society yalifanyika wilayani  hapa.
SHIKUWATA imeendesha mafunzo ya siku tano kwa watu wenye ulemavu Kata ya Namtumbo yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kujua sera ya maendeleo na huduma kwa watu wenye ulemavu.
Wakichangia mada kwa nyakati tofauti juzi, waliiomba serikali kuzingatia uwiano katika mgawanyo wa rasilimali za taifa, ajira, kupewa matibabu bure kama ilivyo kwa watu wasiokuwa na ulemavu.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa shirika hilo, Magreth Mapunda, aliwataka washiriki hao kufuatilia mafunzo hayo kikamilifu ili yaweze kuwasaidia kujua haki zao za msingi.
Aliwataka watu hao wenye ulemavu kuwa huru katika kuchangia kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye mafunzo hayo, ili waweze kuzitafutia ufumbuzi kwa kushirikiana na serikali.
Mratibu wa shirika hilo, Laura Martin, alisema wameamua kuendesha mafunzo hayo katika Kata ya Hanga, Namtumbo, Msindo na Namabengo kwa ajili ya kuwawezesha kujua sera inayozungumzia kundi lao kwa lengo la kuelewa kama inatekelezwa baada ya kugundulika kuwepo kwa tabaka kubwa la kuwatenga na mgawanyo wa rasilimali za taifa.
Chanzo;Tanzania Daima
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa