MKUTANO MKUU WA TATU WA PSPF WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Rais mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ali Hassan Mwinyi, akizindua huduma mpya ya PSPF Pamoja nawe na PSPF call centre, itolewayo na mfuko wa Pensheni wa PSPF, baada ya kufungua Mkutano mkuu wa tatu wa wadau wa mfuko huo Feb 26.2014.
 Mgeni rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Hassan Mwinyi, kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, kulia kwake ni Ndugu Peter Ilomo aliyemwakilisha Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF George Yembesi, Mkurugenzi Mkuu PSPF, Adam Mayingu na Katibu Mkuu MPAIC, John Haule
Wakurugenzi wa idara mbalimbali za mfuko wa Pensheni wa PSPF, mstariu wa mbele, wakiwa miongoni mwa wajumbe wanaohudhuria mkutano mkuu wa tatu wa wadau wa mfuko huo kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa julius Nyerere jijini Dar es Salaam Februari 26, 2014.

  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSPF, Neema Muro akijadili jambo na mmoja wa wadau wa PSPF

Usikivu 
 Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima akimkaribisha Mgeni Rasmi Rais Mstaafu wa Awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi alipowasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimtaifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana, kuhudhuria mkutano mkuu wa tatu wa Mfuko wa PSPF wa wadau Februari 26.2014.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu (kushoto), akimkaribisha Mgeni Rasmi Rais wa Mstaafu Ally Hassan Mwinyi kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimtaifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kuhudhuria mkutano mkuu wa tatu wa Mfuko wa PSPF wa wadau Februari 26.2014.


 Kutoka kushoto ni Meneja wa Kitengo Mawasiliano ya simu, Fatma Elhadgy, Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina Martin na Ephraim Kibonde 

 Mgeni rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Hassan Mwinyi 
Mgeni rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ally Hassan Mwinyi akionyesha zawadi aliyopewa na PSPF, kushoto kwake ni Ndugu Peter Ilomo aliyemwakilisha Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF George

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MHAGAMA ; TEHAMA ITAONDOA TATIZO LA WALIMU, VITABU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
WADAU wa elimu wamekubali kutumia teknolojia ya habari na mwasiliano kufundisha na kujifunza ili kukabili tatizo la uhaba wa walimu na vitabu linalokwaza maendeleo ya elimu nchini.
Hayo ni baadhi ya maazimio yaliyotokana na mjadala wa siku mbili wakati wa kongamano la elimu ulioandaliwa na Taasisi ya Learning InSync International kwa kushirikiana na British Council na kufanyika mjini Moshi, Kilimanjaro.
Akizungumza kwenye kongamano hilo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenister Mhagama, alisema ili kuharakisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) shuleni, serikali itaongeza kasi ya kuwaelimisha walimu na wanafunzi kuhusu matumizi ya teknolojia itakayorahisishwa na kusambazwa kwa
mkongo wa taifa.
“Pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya kiteknolojia duniani, Tehama pia itatuwezesha kuhimili tatizo la uhaba wa walimu na vitabu nchini,” alisema Mhagama na kuongeza kwamba mwalimu atatumia kitabu kufundisha wanafunzi wengi kwa wakati mmoja.
Chanzo;Tanzania Daima

TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA WADAU WA PSPF

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MFUKO WA PENSHENI WA
PSPF

TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA WADAU
Mfuko wa Pensheni wa  PSPF unatangaza kwamba kutakuwa na Mkutano Mkuu wa tatu wa wadau utakaofanyika tarehe 26 na 27  Februari 2014 kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi jioni katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere uliopo barabara ya Shaban Robert  jijini Dar es salaam.
Madhumuni ya Mkutano huu ni kutoa taarifa ya hesabu ya mwaka na utendaji wa Mfuko na kutathmini mafanikio na changamoto zinazokabili Mfuko na sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa ujumla.
“PSPF - TULIZO LA WASTAAFU”
Mkurugenzi Mkuu
Mfuko wa Pensheni wa PSPF,
Makao Makuu,Golden Jubilee Towers,  S.L.P 4843. Dar-es-Salaam.
Simu: +255222120912/52 au +255222127375 /6
 Nukushi: +255222120930

 Barua pepe:pspf@pspf.tz.org

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Kichanga kilichotupwa kipo hai

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

HUYU ni mtoto aliyetupwa na mama yake mara baada ya kujifungua katika eneo la Mkuzo manispaa ya Songea mkoani Ruvuma hivi karibuni.Mama mzazi wa mtoto huyo anadaiwa kumtupa huku amemuhifadhi ndani ya mfuko kisha yeye kukimbia.Wasamaria wema walimuokota mtoto huyo akiwa hai na kumpeleka katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma HOMSO  ambako anaendelea kulelewa na kupata huduma zote muhimu kwa mtoto mchanga.
Wauguzi wa hospitali ya mkoa wa Ruvuma  wamempa jina la Thomas huku wakiendelea kutoa malezi bora kwa mtoto huyo ambaye alizaliwa akiwa na uzito pungufu.Hata hivyo mtoto anaendelea vizuri katika wodi ya wazazi na uzito wake unaongezeka .Hapana shaka mtoto Thomas akitimiza uzito unastahili anaweza kwenda kulelewa katika vituo vinavyolea watoto yatima kama vile kituo cha kulelea yatima cha watawa wa mtakatifu Agnes Chipole Songea.
Tabia ya wasichana na wanawake kujifungua kisha kuwatupa watoto wao inaonekana kuendelea kuwa sugu katika maeneo mbalimbali nchini.Mtoto Thomas anahitaji msaada kwa kuwa hafahamiki hadi sasa mama yake wala baba yake, kama umeguswa na unapenda kumsaidia mtoto huyu mahitaji muhimu kwa watoto unaweza kutembelea wadi ya wazazi katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma ama wasiliana nami kwa  baruapepe albano.midelo@gmail.com,au piga simu 0784765917.
Chanzo;Kwanza jamii

RC RUVUMA AWATAKA POLISI KUFUATA MAADILI YA KAZI

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said thabit Mwambungu amelitaka jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma kufuata Maadili na kuheshimu Kanuni, Taratibu na Sheria za Nchi
                  
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu ameyasema hayo wakati Jeshi la Polisi lilipofanya Maadhimisho ya kuukaribisha mwaka 2014 Sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) sherehe zilizotanguliwa na paredi la Kikosi cha kutuliza ghasia.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amesema Kazi kubwa ya Jeshi la Polisi ni kulinda mali za raia pamoja na kutii mamlaka yaliyopo katika Dola kinyume na hapo nikulidhalilisha jeshi la Police kimaadili.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu amesema sifa ambayo inaliondolea heshima Jeshi la Police heshima  ni kuwa na moyo wa ubinafsi, chuki na visasi visivyo na tija.

Naye Kamanda wa polisi anayehamia Manyara Deusdedit Nsmeki amesema katika kuukaribisha mwaka 2014 Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma linajivunia kwa asilimia 75% kupunguza ujanji na kuweza kukamata nyara za serekari pia kuwa karibu na wananchi

Kamanda wa Polisi Deusdedit Nsmeki amesema jambo lingine la kujivunia ni kupungua kwa ajali za barabarani kutoka maelfu ya ajali kwa kila mwaka na kubaki katika mamia ya ajali. Jeshi la Polisi litaendelea kutoa Elimu ili kupunguza ajali.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Adaiwa kumuua mwanawe kwa kumbamiza kwenye lami

Mkazi  wa kijiji cha Madaba Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, Onestory Mgaya (31), ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kumuua mtoto wake mwenye umri wa miaka saba kwa kumbamiza  kwenye barabara ya lami.
Kamanda wa Polisi mkoani Ruvuma, Deusdedit Nsimenke, alimtaja mtoto aliyeuawa kuwa ni  Nesta Mgaya.

Kamanda Nsimenke alisema tukio hilo lilitokea Februari 9, mwaka huu saa 5:00 asubuhi katika kijiji cha Lilondo wilayani Songea.

Alifafanua kuwa inadaiwa kuwa siku ya tukio, mtuhumiwa huyo, mkewe, Blesila Mponda (30)  na mtoto wao Nesta, walitoka Madaba kwenda kijiji cha Lilondo kusalimia wazazi.

Hata hivyo, alisema wakiwa njiani kurudi nyumbani kwao,mkewe Blesila alibaini kuwa amesahau kadi ya kliniki ya mtoto wao na hivyo akalazimika kumuachia mumewe mtoto huyo ili yeye akaichukue kadi hiyo.

Lakini alisema mtuhumiwa huyo alianza kumbamiza mtoto kwenye barabara ya lami huku akiwa amemshika miguu na kichwa chini.

Hata hivyo, alisema wakati akiendelea kufanya ukatili huo, watu waliokuwa jirani walikwenda kutaka kumuokoa mtoto huyo lakini mtuhumiwa alikimbilia porini na kumuacha mtoto..

Alisema wasamaria wema walimkimbiza mtoto huyo katika Kituo cha Afya cha Madaba kwa matibabu.

Kamanda Nsimenke, alisema baadaye mtoto huyo alipelekwa katika Hospitali ya Mkoa ya Songea kwa matibabu zaidi lakini alifariki dunia siku iliyofuata.

Hata hivyo, Kamanda Nsimenke alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa siku hiyo hiyo na anatarajiwa kupelekwa kupimwa akili yake kabla ya kufunguliwa mashitaka ya mauaji.
 
CHANZO: NIPASHE
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Polisi 14 nguvuni kwa kuiba mali ya Sh900 mil

Polisi mkoani Ruvuma, wameingia katika kashfa, baada ya askari wake kutuhumiwa kuiba vitu vyenye thamani ya zaidi ya Sh900 milioni waliyokuwa wakivilinda. Vitu hivyo ni mali ya mkandarasi aliyefukuzwa katika mradi wa ujenzi wa Barabara ya Namtumbo hadi Tunduru.
Tayari polisi 14 wamesimamishwa kazi na wanasubiri kuvuliwa magwanda ili kufikishwa mahakamani. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Deusdedit Nsimike, jana alithibitisha habari hizi kwa njia ya simu.
Alisema tukio hilo limelifedhehesha Jeshi la Polisi na kwamba taratibu za kuwafukuza kazi askari hao zinaendelea kabla ya kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Mtoa habari wetu alisema kashfa hiyo iligundulika mwezi uliopita, lakini haikutangazwa kutokana na unyeti wake na kwamba suala hilo limeishtua Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Ruvuma.
Akifafanua zaidi alisema kwamba Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), waliipatia polisi kazi ya kulinda mitambo, magari na vifaa mbalimbali vya Kampuni ya Progressive Hgleig JV ya India, baada ya kampuni hiyo kushindwa kazi na hatimaye kufukuzwa.
Alisema Serikali iliifukuza kampuni hiyo na kutoa agizo la kushikilia mali zake hadi itakapolipa fidia kwa hasara iliyoipata.
Mtoa habari ambaye jina lake linahifadhiwa alisema askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Ruvuma, walipata zabuni ya kulinda mali hizo, lakini baadaye imegundulika kuibwa mali za mamilioni ya fedha.
Baadhi ya mali zilizoibwa ni pamoja na mafuta, matairi na vipuri vya magari. Meneja wa Tanroads mkoani Ruvuma, Abraham Kisimbo, alithibitisha habari hizo.
Alisema tukio hilo ni baya na kwamba anayeweza kulizungumzia zaidi ni na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma au Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu.
Chanzo;Mwananchi
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa