DIRA: Kikwete na woga wa kufanya uamuzi mgumu

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Wakati Rais Jakaya Kikwete akifungua Bunge Maalumu la Katiba wiki iliyopita mjini Dodoma alisema kuwa asingependa kuona muundo wa Serikali tatu ukitokea wakati bado akiwa madarakani.
Alisema angependa ikitokea hivyo iwe ni baada ya yeye kumaliza muda wake.
Ilikuwa baada ya kutoa ufafanuzi mrefu wa athari za kuchagua muundo wa serikali tatu huku akisisitiza msimamo wa chama chake, CCM wa serikali mbili.
Hotuba yake ilikuja siku chache tu baada ya mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kuhutubia Bunge hilo.
Katika hotuba yake, Warioba alielezea jinsi tume yake ilivyokusanya maoni na mwelekeo wake katika hilo.
Alisema kati ya wananchi 38,000 waliotoa maoni yao kuhusu Muungano visiwani (Zanzibar), watu 19,000 walizungumzia suala la muundo huku zaidi ya nusu wakitaka marekebisho ya Katiba yatakayowezesha uwepo wa serikali tatu.
Kwa upande wa Tanzania Bara, asilimia 61 ya waliotoa maoni juu ya Muungano walipendekeza serikali tatu na kwa upande wa Zanzibar asilimia 60 walipendekeza serikali ya mkataba.
Suala la  Muungano ni nyeti katika mchakato huu wa Katiba, hasa kwa kuwa limekuwa na malalamiko mengi kwa pande zote mbili, yaani Tanganyika na Zanzibar.
Ili kuonyesha kuwa Wazanzibari hawaridhishwi na Muungano huo, ndiyo maana mwaka 2010 walibadili Katiba yao iliyopora kabisa madaraka ya Serikali ya Muungano.
Kwa maana nyingine Katiba ya Muungano imeshavunjwa. Hapo tena kuna Muungano gani kama siyo kujifariji?
Kama kweli Rais Kikwete angekuwa na uchungu wa Muungano, mbona hakuchukua hatua dhidi ya kitendo hicho cha Wazanzibari? Huyu ndiye Rais aliyeapa kuilinda Katiba? Upo wapi ujasiri wake?
Ilitegemewa kuwa Rais Kikwete angetumie fursa hii kulipatia ufumbuzi wa kudumu, lakini anaogopa kuonekana mbaya kwa wana CCM wenzake na ndiyo maana ameamua kutoa maoni yake ya faida za serikali mbili katika muda ambao Bunge la Katiba linajiandaa kuanza kujadili Rasimu ya Katiba.
Chanzo;Mwananchi

VIJIJI VIWILI VYAANZA KUVUNA ASALI KWA WINGI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Wananchi wa vijiji vya Mtyangimbole na Gumbiro Songea  Vijijini baada ya miezi miwili  wanatarajia kuvuna kilo 500 za Asali  na Nta kilo 50 baada ya kutundika mizinga 50 katika Msitu wa Hifhadhi
                            
Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu amesema hayo katika wiki ya kitaifa ya kutundika mizinga iliyo fanyika kijiji cha Mtyangimbore .Amesema Mpango wa serekari wa Matokeo Makubwa sasa ni kubuni mipango mbali mbali ya kumwongezea Mwananchi wa Chini kipato kupitia Ufugaji wa Nyuki’

Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti amesema umefika wakati sasa wa kujenga urafiki na Nyuki badala ya kuwaona Nyuki kama Adui amewataka wananchi kuepuka na  kuchoma misitu ovyo unao sababisha viumbe wengi kutoweka wakiwemo nyuki.

Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph joseph Mkirikiti akimwakilisha mkuu wa Mkoa Said thabit Mwambungu amesema Serekari ina buni mbinu mbali mbali kuongeza kipato kwa Mwananchi kupitia Mali asili tulizo nazo nyuki walioko wapatao milioni 9.2 wakitunzwa vizuri wataweza kuongeza hali ya uchumi kukua ikiwa pamoja na kuongeza fedha za kigeni ,Hivyo tabia ya kuangamiza viumbe vyenye kuleta tija iachwe mara moja


Meneja wa Misitu Wilaya ya Songea Manyisye Mpokigwa amesema juhudi za Idara yake kuhusu Utundikaji wa Mizinga na kulinda Misitu sasa inaonyesha mafanikio wananchi wengi wa vijijini wameanza kuvuna Asali .

Naye Mwakilishi wa Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Gaudens Kilasi amesema kutokana na Mizinga 25 iliyotolewa mwaka jana na mizinga 25 ya sasa itawasaidia wananchi kuvuna Tani 500 za Asali swala litakalo saidia kupunguza umasini kwa wananchi wa vijijini.

Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph joseph Mkirikiti amesema Jumla ya Makundi Milioni 9.2 ya nyuki yapo hatarini kutoweka endapo wananchi hawataacha mtindo wa kuchoma Misitu ovyo, amewaomba Wananchi kuacha kuwa Maadui na Nyuki au Misitu sasa wawe marafiki kwa Nyuki.
 

Mamba amuua mvuvi Mto Lwika

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
MASALIA ya mwili wa Charles Mkoma (37), mwanakijiji wa Liuli, wilayani Nyasa, Ruvuma yamekutwa kandokando ya Mto Lwika.
Mkoma, aliuawa baada ya kukamatwa na mamba wakati alipokwenda kuvua samaki kwenye mto huo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Akili Mpwapwa, alisema mabaki hayo yalipatikana mchana wa Machi 8, mwaka huu.
Akifafanua zaidi alisema mabaki ya mwili wa marehemu huyo yaligunduliwa na watu waliokuwa wakimtafuta baada ya kutooneka nyumbani kwake kwa siku nne.
 Chanzo;Tanzaniz Daima

Chadema yawaonya wanaochafuana

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa amewaonya baadhi ya wanachama wanaochafuana na waliojitokeza kutangaza nia ya kugombea nafasi mbalimbali za udiwani, ubunge kabla ya wakati akiwamo mwenyekiti wa chama hicho mkoani hapa, Joseph Fuime.
Mwenyekiti huyo anadaiwa kutangaza nia ya kugombea ubunge wa Jimbo la Songea mjini na kutakiwa kuacha mara moja, kabla ya hatua kali za kinidhamu hazijachukuliwa dhidi yao kama kanuni ya chama hicho inavyosema,ikiwamo pamoja na kufukuzwa uanachama, kusimamishwa au kupewa adhabu zilizopo kwenye kanuni.
Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu jana kuhusu onyo lake Dk Slaa amesema, kutangaza nia siyo dhambi ni haki ya mwanachama na siyo mgogoro ila anapaswa afuatae kanuni za chama zinavyoelekeza na iwapo kanuni zitavunjwa na mgombea basi hawatasita kumchukulia hatua.
“Ni kweli kuna baa dhi ya wanachama wanatangaza nia na hawafuati kanuni zinavyosema,tayari chama kimeshapeleka waraka katika majimbo, wilaya na mkoa wasome na kuelewa,iwapo hawajapata waraka huo wawasiliane na ofisi yangu watumiwe kwani wakibainika watapata matizo pamoja na kuchukuliwa hatua za kinidhamu,”alisema Dk Slaa.
Mwenyekiti wa chama hicho Singida, Joseph Fuime hakuweza kupatikana kuzungumzia tuhuma hizo kwani simu zake zote za mkononi hazikupatikana.
Chanzo;Mwananchi

Diwani apinga ongezeko la mitaa, kata

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
DIWANI wa Misufini katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea, Ruvuma, Salum Mfamaji (CHADEMA), amesema kuongezwa kwa mitaa katika manispaa hiyo ni kuibebesha mzigo serikali na wananchi.
Mfamaji alisema hayo wakati akichangia hoja katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani humo kilichofanyika chini ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea, Charles Mhagama.
Alisema mantiki ya kuendelea kuongeza mitaa wakati iliyopo kuihudumia kwake ni matatizo huku akisisitiza kwamba kuendelea kuongeza kata wakati watendaji wa mitaa na kata wanalipwa mishahara midogo isiyokidhi mahitaji yao kwa mwezi badala yake iwaboreshee mishahara yao.
 Chanzo;Tanzania Daima

BASI LA SAIBABA LAPATA AJALI LIKITOKA SONGEA KUELEKEA DAR ES SALAAM

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 









Picha zikionesha basi la kampuni ya Saibaba Express linalofanya safari zake kati ya dar - Songea likiwa limeacha barabara na kuparamia mti uliopo pembeni mwa barabara eneo la Kidegebasi iRINGA, barabara ya Iringa Mbeya

Haikufahamika maramoja chanzo cha ajali hiyo, na kama kuna majeruhi ama la, lakini mwandishi wetu ameshuhudia polisi pamoja na abiria wakiwa eneo la tukio kuona namna ya kufanya
Basi hilo lilikuwa likitoka Songea kuelekea dar es Salaam, na imetokea majira ya saa nne asubuhi
Vijimambo Blog

MAZISHI YA MCHEZAJI WA ZAMANI NA MMOJA WA WAANZILISHI WA TIMU YA MAJI MAJI YA SONGEA.‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Mzee Abdala Alli alikuwa mmoja wa waanzilishi wa timu ya Majimaji ya Songea wana lizombe,yeye na wenzake watatu ndiyo walianzisha timu hiyo,Alikuwa mzee Mbegambega,Mzee Mshamu wakiongozwa na Mhe,Laurensi Mtazama Gama hao wote kwa sasa ni marehemu.
PICHA NA MPENDA MVULA.
 Mmoja wa watani wa Kabila la Wayao akimpaka unga usoni mtoto wa Kwanza wa kiume Hamisi Abdala Alli,
 Siyo Igizo ni utani kati ya Wamwela na Wayao.
 Mfiwa uruusiwi kufuta huo unga ukifuta tu wanakuja na debe zima wanakumwagia bora uwe mpole.
 Mzee Abdala Alli muda wake mwingi aliutumia kwenye mchezo wa mpira mpaka tatizo la upofu lilipompata ndipo akastaafu mambo ya soka akawa mshauri tu kwa Viongozi wa timu yake ya Majimaji.


 Mwili wa Marehemu ukitoka ndani ya nyumba yake.


 Watu wengi walijitokeza.


 Watani wa Kiyao wakishangilia.
 Watani wa Kiyao wakimfuatisha marehemu alivyokuwa akitembea enzi ya Uhai wake.
 Amezikwa kwenye Mashamba yake hapa Kipera Songea.


 APA NDIYO MWISHO WA SAFARI YAKE MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI AMINA....
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa