WANAFUNZI TUNDURU WASOMEA CHINI YA MTI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
WANAFUNZI wa darasa la awali shule ya Msingi Nakayaya wilayani hapa mkoani Ruvuma, wanasomea chini ya mti kutokana na darasa hilo kuendeshwa bila ya kuwa na chumba maalum.
Hali hiyo imebainika, baada ya mwandishi wa habari hizi kuitembelea shule hiyo hivi karibuni na kuwakuta wanafunzi wakiendelea na masomo hayo nje chini ya mti ulio na kivuli cha kuwahifadhi wakati wa jua kali.
Akizungumza shuleni hapo, Kaimu Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Christina Mhowera, alisema watoto hao wamelazimika kusomea nje baada ya huduma ya elimu hiyo kuanzishwa shuleni hapo bila ya kuwa na jengo maalum kwa wanafunzi wa awali.
Alisema awali wanafunzi hao walikuwa wakisomea kwenye gofu (jengo mbovu), lililokuwa jirani na shule, lakini walilazimika kuondolewa baada ya jengo hilo kutwaliwa kwa matumizi mengine.
Aliongeza kuwa baada ya hapo walihamishiwa kwenye nyumba ya mwalimu kabla ya kukamilika, lakini waliondolewa tena na kuanza kusomea nje chini ya mti hadi sasa.
Alisema darasa hilo lenye wanafunzi 92, linaendeshwa bila ya kuwa na chumba cha darasa maalum wala madawati kutokana na shule hiyo kukabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa hadi hapo watakapopata darasa maalum kwa ajili ya wanafunzi hao.
Kwa upande wake mwalimu wa darasa hilo, Teckla Milanzi, alisema mbali na darasa hilo kutokuwa na chumba, linakabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo ya uhaba wa vitendea kazi kama vitabu na vyenzo zingine za kufundishia na hakuna bajeti yoyote inayotumwa kuliwezesha darasa hilo.
Aidha, uchunguzi uliofanywa katika shule nyingine tatu za Wilaya ya Tunduru, yaani Shule ya Msingi Nanjoka, Majengo na Shule ya Msingi Tunduru Mchanganyiko kuangalia mazingira ya utoaji elimu ya awali katika shule hizo umebainisha kukabiliwa na changamoto nyingi hali ambayo inahatarisha msingi wa elimu kwa wanafunzi.
  Chanzo Tanzania Daima

MWAMBUNGU AKIPONGEZA CHUO CHA MT. JOSEPH

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Said MwambunguMKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu, amekipongeza chuo kikuu cha sayansi ya kompyuta cha Mtakatifu Joseph Tawi la Songea kwa jitihada zake za kuendelea kupanua wigo wa kutoa huduma na kukuza elimu ya juu hapa nchini.
Mwambungu, alitoa pongezi hizo juzi wakati wa mahafali ya tano ya chuo hicho mjini Songea, yaliyohusisha wahitimu 119 wa shahada na stashahada.
Alisema kuanzishwa kwa chuo hicho, kumesaidia kulipunguzia taifa tatizo la ukosefu wa wataalamu wa sayansi hususani katika ukanda wa kusini na taifa kwa ujumla.
Alisema kuwa kuanzishwa kwa chuo kikuu cha sayansi ya kilimo na teknolojia katika sekta ya kilimo ni jambo jema kwa ustawi wa nchi huku akiwataka wahitimu hao kuitumia elimu waliyoipata kwa ajili ya kuleta mabadiliko katika jamii na taifa kwa ujumla kwa kufanya kazi kwa bidii na ufanisi.
Alisema kuwa katika maisha ya hivi sasa, hakuna njia fupi ya kufikia mafanikio katika maisha zaidi ya kufanya kazi kwa bidii na maarifa na kudai kwamba, changamoto zilizopo katika chuo hicho zigeuzwe kuwa fursa pekee ya kujipanua na kutoa elimu bora  huku akiwataka kuboresha mawasiliano ili kukuza wigo wa utatuzi wa changamoto mbalimbali.
Aidha, amewaomba wanafunzi wa chuo hicho, kuombea amani hususani katika kipindi hiki kigumu ambacho taifa linaingia kwenye mchakato wa uundwaji wa katiba mpya.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya chuo hicho, Askofu John Ndimbo, alisema kuwa anajisikia fahari kuona chuo hicho kinazalisha wataalamu wengi wa sayansi ukanda wa kusini huku akidai kuwa elimu ni tunu kubwa ya maendeleo.
Chanzo;Tanzania Daima

DCI: BOMU LILILOJERUHI POLISI NI LA KIENYEJI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Issaya Mngulu
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Issaya Mngulu, (pichani) amesema bomu waliorushiwa polisi wanne limetengenezwa kienyeji.
 
Hata hivyo, amesema bomu hilo limetengenezwa kitaalamu zaidi kuliko mabomu mengine yaliyotengenezwa kienyeji na kulipuliwa katika baadhi ya maeneo nchini, lakini akasema hadi sasa hakuna anayeshikiliwa kwa tuhuma hizo.
 
Alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya polisi Mkoa wa Ruvuma.
 
Mngulu alisema bomu hilo ni la aina yake,  ingawa kwa sasa hawezi kuelezea zaidi kwa sababu akifanya hivyo atatoa  nafasi kwa watu wengine kutengeneza mabomu hayo na kuendelea kuhatarisha amani nchini.
 
“Nimekagua matukio mengi hapa Tanzania yanayohusiana na milipuko ya mabomu. Lakini tukio la Songea, bomu hili ni la aina yake. Kwani lina ‘cover’ ya bati gumu, ambalo linaonyesha limetengenezwa kiufundi zaidi,” alisema Mngulu.
 
Alisema katika tukio hilo, askari watatu walijeruhiwa; wawili kati yao bado hali zao ni mbaya na wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa huo.
 
Aliwataja askari hao kuwa G7351 PC Ramadhan, WP 10399 PC Felista na H 3484 PC Respicus, ambaye ametibiwa na kuruhusiwa.
 
Alisema uchunguzi wa kuwabaini waliohusika na tukio hilo unaendelea kufanyika kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama.
 
Wakati huo huo, majeruhi wawili waliojeruhiwa katika tukio hilo, ambao wamelazwa katika hospitali hiyo walisema hali zao zinaendelea vizuri na tayari wameshafanyiwa upasuaji.
 
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa huo, Dk. Benedicto Ngaiza, alisema hali za majeruhi zinaendelea vizuri.
 
CHANZO: NIPASHE

MSAADA WA WHEELCHAIR TOKA MAREKANI‏


Kuna masamalia mwema ametuka Wheelchair kwa Scholastica Mhagama (76)  mwenye ulemavu wa viungo anayeishi pekee yake katika kibanda kilichoezekwa kwa nyasi.
Bibi huyo mkazi wa Kijiji cha Lundusi Kata ya Peramiho wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma, Msamalia huyu kutoka Maryland Marekani anaitwa Joyce Rwehumbiza aliguswa na stori iliyoandikwa na gazeti la mwananchi iliyoweka mawasiliano na  albano.midelo@gmail.com, 0688551355 iliyobeba kichwa cha habari "Bibi ajitengenezea jeneza baada ya kuchoshwa na dhiki" 

Joyce Rwehumbiza ameishatuma Wheelchair hiyo inafika Dar es Salaam leo Ahamisi Sept 11, 2014 na amejaribu kuwasiliana na mwandishi wa hii stori lakini hakuweza kumpata ameomba tafadhali Albano Midelo awasiliane na namba 0765 835722 wheelchair itafikia hapo na ameombwa afanye haraka kwani baada ya siku 2 huyu mama anatarajiwa kusafiri.
Bibi Scholastica Mhagama akiwa amejitengenezea jeneza lake

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

NHC YAPANIA KUENDELEZA MKOA WA RUVUMA‏



Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw.  Nehemia Mchechu na ujumbe wake wakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Bw. Abdulah Lutavi akiwatembeza kwenye eneo lililotengwa na Wilaya hiyo kwa ajili ya kujengewa nyumba na NHC. Shirika la Nyumba litajenga nyumba za gharama nafuu katika halmashauri hiyo hivi karibuni.

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw.  Nehemia Mchechu, Mkuu wa Wilaya Natumbo, Bw. Abdulah Lutavi na ujumbe wao wakijadiliana kwenye eneo litakalojengwa nyumba za gharama nafuu na Shirika la Nyumba.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw.  Nehemia Mchechu na msafara wake wakikagua mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu wa Mkuzo, Songea. Mradi huo una jumla ya nyumba 18.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw.  Nehemia Mchechu akitembelea nyumba za Shirika za gharama nafuu zilizojengwa eneo la Mkuzo, Songea.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw.  Nehemia Mchechu akizugumza na Watendaji wa Halmashauri zote za Mkoa wa Ruvuma kuhusu mpango wa NHC wa kuwekeza ujenzi wa nyumba katika halmashauri hizo.

 Sehemu ya Watendaji wa Halmashauri za mkoa wa Ruvuma wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw.  Nehemia Mchechu (hayuko pichani) alipozungumza na mkoa huo kuonyesha jia ya kujenga nyumba katika mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Mwambungu akiongea na Watendaji wa Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma na Shirika la Nyumba la Taifa na kulihakikishia Shirika kupewa viwanja vya kujenga nyumba katika halmashauri zote za mkoa huo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw.  Nehemia Mchechu akiangalia ufyatuaji wa matofali wa vikundi vya vijana Peramiho vilivyosaidiwa mashine hizo na NHC.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw.  Nehemia Mchechu akisikiliza maelezo ya kiongozi wa kikundi cha vijana Peramiho.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw.  Nehemia Mchechu akishiriki katika ufyatuaji wa matofali na vikundi vya vijana wilayani Peramiho mwishoni mwa wiki.
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw.  Nehemia Mchechu ukitembezwa katika maeneo yenye viwanja katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mwishoni mwa wiki.

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw.  Nehemia Mchechu akionyeshwa ramani ya eneo walilokabidhiwa na halmashauri ya Mbinga
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw.  Nehemia Mchechu na ujumbe wake wakionyeshwa viwanja na Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Bw. Julius Mwakafwila vitakavyotumika kujenga nyumba za gharama nafuu.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw.  Nehemia Mchechu katika picha ya pamoja na Watendaji wa wilaya ya Mbinga na NHC wakati akiagana na ujumbe wa Halmashauri ya Mbinga mwishoni mwa wiki
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

TANGAZO MUHIMU KWA WAHITIMU WOTE WA CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA (CBE) , WANAALIKWA KWENYE MKUTANO 4 OKTOBA 2014


C H U O   C H A   E L I M U   Y A   B I A S H A R A (CBE)

CHINI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA”
MKUTANO WA CBE ALUMNI MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI



         KAMPASI YA MBEYA
Mkuu wa Kampasi ya Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Mbeya, Dionize A. Lwanga , Akizungumzia Mikakati na maandalizi ya awali ya Kutimiza Miaka 50 ya Chuo hicho, na Mkutano Mkubwa utakaofanyika Mwezi Octoba ambao utawakutanisha wanafunzi wote waliowahi kusoma chuo hicho ili kujadiliana mambo kadha wa kadha wakati wanajiandaa na miaka hiyo 50 na kutengeneza Alumni Association.
 Afisa Taaluma wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Kampasi ya Mbeya akizungumza Jambo wakati wa Majadiliano juu ya maandalizi ya Kikao cha mwezi Octoba.
Mkufunzi Msaidizi wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Kampasi ya Mbeya Akizungumza jambo wakati wa mazungumzo mafupi juu ya Maandalizi ya mkutano huo utakaofanyika Octoba
Majadiliano yakiwa yanaendelea




MKUU WA CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA ANAWATANGAZIA WAHITIMU WOTE WA MIAKA YA NYUMA NA WA SASA WA CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA WANAOISHI KATIKA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI KUHUDHURIA MKUTANO WA WANA JUMUIA YA CBE (CBE ALUMNI) UTAKAOFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 4, 10, 2014 KATIKA VIWANJA VYA MBEYA HOTEL, JIJINI MBEYA, KUANZIA SAA 7.00 MCHANA. BAADA YA MKUTANO KUTAKUWA NA CHAKULA CHA PAMOJA.

MIONGONI MWA MAMBO YATAKAYOFANYIKA SIKU HIYO NI PAMOJA NA:

1)      KUUNDA ALUMNI ASSOCIATION KWA NYANDA ZA JUU KUSINI

2)      KUCHAGUA VIONGOZI WA ALUMNI ASSOCIATION WA KANDA

3)      KUPATA TAARIFA YA MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA CBE

4)      MADA KUHUSU MCHANGO WA CBE KATIKA KUENDELEZA BIASHARA NCHINI

5)      MADA KUHUSU CBE ILIPOTOKA, ILIPO KWA SASA NA CBE IJAYO

6)      KUBADILISHANA UZOEFU NA MAWAZO (NETWORKING)

MADA HIZI ZITAWASILISHWA NA WAKUFUNZI, WAHITIMU, WANAFUNZI NA WADAU WENGINE WA CBE.

TAFADHALI, UPATAPO TAARIFA HII MJULISHE NA MWENZIO.

 PAMOJA TUNAWEZA

KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA MKUU WA KAMPASI YA MBEYA

BARUA PEPE: dir.mbeya@cbe.ac.tz

Simu                 :025- 2500571
                          :0654- 878704, 0717 -288874, 0655- 080858






C H U O   C H A    E L I M U    Y A    B I A S H A R A (CBE)


CHINI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA”

KAMPASI YA MBEYA



NAFASI ZA KUJIUNGA NA MASOMO NGAZI YA ASTASHAHADA (CERTIFICATE) NA STASHAHADA (DIPLOMA) KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015 KATIKA FANI ZIFUATAZO:


  • Uhasibu ( Accountancy)
  • Masoko (Marketing Management)
  • Ununuzi na Ugavi (Procurement & Supplies Management)
  • Usimamizi wa Biashara (Business Administration)

1.  Fomu za kujiunga zinapatikana Chuoni Jengo la chuo kikuu Huria ( Kituo cha Mbeya) Forest ya zamani, CBE DAR ES SALAAM, CBE DODOMA, CBE MWANZA au   Bofya hapa Chini Ku Download


2. Wahitimu wa kidato cha nne wenye ufaulu usiopungua D nne watajiunga moja kwa moja.

3. Kujiunga na stashahada (diploma) wahitimu wa kidato cha sitwenye    ufaulu usiopungua Principal pass moja, subsidiary pass mbilAu wenye    astashahada husika yaani (certificate) kutoka Chuo kinachotambuliwa na NACTE



Masomo kwa ngazi zote yanatolewa kuanzia asubuhi hadi jioni (FULL TIME)  na jioni (EVENING PROGRAM) jumatatu hadi ijumaa.


Ewe mwananchi jiunge na chuo chenye uzoefu wa zaidi ya miaka 49 katika elimu ya Biashara, Ujasiriamali, Ushauri na Utafiti.


Tunaendelea kupokea maombi ya kujiunga katika ngazi zote



Kwa maelezo zaidi piga  simu namba, 0654-878704 / 0767-288874
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa