KAMPUNI YA MSAMA PROMOTIONS KUPELEKA MATAMASHA MENGINE MJINI SONGEA, NI KUTOKANA NA MWITIKIO WA WANASONGEA‏


1 
Mwimbaji wa Muziki wa injili Upendo Nkone akiimba mbele ya mashabiki wa muziki huo kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea ambapo tamasha kubwa la Krismas limefanyika na kushirikisha waimbaji mbalimbali kutoka nchini na nje ya Tanzania, onesha la leo lilikuwa ni hitimisho la matamasha ya Krismas yaliyofanyika katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Ruvuma yakishirikisha waimbaji kama Upendo Nkone, Faraja Ntaboba kutoka nchini DRC Congo , Edson Mwasabwite.
Mwimbaji Upendo Kirahilo akipagawisha mashabiki wake wakati alipokuwa akiimba jukwaani katika tamasha la Krismas lililofanyika kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea leo. 3 
Mwimbaji Upendo Kirahilo akipagawisha mashabiki wake wakati alipokuwa akiimba jukwaani katika tamasha la Krismas lililofanyika kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea leo. 6 
Mwimbaji Upendo Kirahilo akserebeka na Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama alipokuwa akiimba jukwaani katika tamasha la Krismas lililofanyika kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea leo. 8Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama na MC wa Tamasha hilo Bw. Mwakipesile wakielekea kumtunza mwimbaji wa muziki wa injili Joshua Mlelwa wakati alipokuwa akionyesha uwezo wake jukwaani kwenye tamasha la Krismas lililofanyika mjini Songea leo. 11Mgeni rasmi wa tamasha hilo Meya wa mji wa Songea Mh. Charles Mhagama akizungumza na mashabiki wa muziki wa injili kwenye uwanja wa majimaji kutoka kushoto ni Mmoja wa waratibu wa tamasha hilo John Melele. MC Mwakipesile na Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion. 9 
Mwimbaji wa muziki wa injili Bonny Mwaiteje nakipagawisha mashabiki wake kwenye uwanja wa majimaji mjini Songea leo. 10 
Mwimbaji wa muziki wa injili Bonny Mwaiteje nakipagawisha mashabiki wake kwenye uwanja wa majimaji mjini Songea leo. 12 

Somlomon Mkukubwa akiimba wimbo unaoelezea kisa cha mkono wake kukatwa ambao unamuelezea mama wa kambo aliyesababisha tukio hilo na kuwaasa mashabiki wake kusamehe kama yeye alivyomsamehe mama yake wa kambo 13Mashabiki wakiimba pamoja na mwimbajo Solomon Mukubwa 01
Mwimbaji Ambwene Mwasongwe akiimba kwa hisia huku akishirikiana na mwimbaji Solomon Mukubwa wakati wa tamasha la Krismas kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea leo kutoka kushoto ni Edson Mwasabwite na Faraja Ntaboba kutoka nchini DRC Congo.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

UKAWA WAAMBULIA VITI 38 TUNDURU

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilani Tunduru, kimeibuka kidedea kwa kupata viti katika vijiji 105 katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyia jana nchi nzima.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimepata viti 38 kati ya vijiji vyote 153 vilivyopo wilayani hapa.
Aidha, takwimu hizo zinaonesha kuwa hadi sasa bado matokeo ya vijiji 10 hayajapatikana, kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za baadhi yake kutopiga kura kwa kukosekana vifaa vya kupigia kura.
Sababu nyingine ambazo zimekwamisha kupatikana kwa takwimu kutoka katika vijiji hivyo, ni pamoja na kutokamilika kwa zoezi la kuhesabu kura na pia kuwepo kwa pingamizi.
Akizungumzia zoezi hilo msimamizi wa Uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Tinna Sekambo, alisema kuwa takwimu kamili za uchaguzi huo zikiwemo za wenyeviti wa vitongoji na wajumbe, zitatolewa kesho baada ya kukamilika kwa zoezi la kuunganisha matokeo hayo.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Chande Nalicho pamoja na mambo mengine, alisema kuwa zoezi hilo limefanyika katika hali ya usalama wa hali ya juu.
Chanzo:Habari Leo

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

RADI YAUA SITA, YAJERUHI WAWILI

WATU sita wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi katika migahawa miwili inayohudumia wanafunzi wa Chuo Cha Maendeleo na Mifugo (LITA).
Tukio tukio hilo lilitokea juzi jioni usiku wilayani hapa wakati wanafunzi hao wakiwa kwenye mgahawa kwa ajili ya kupata mlo wa jioni
Kwa mujibu wa Ofisa Muuguzi Kiongozi wa Kituo cha Afya Madaba, Oraph Pili, siku ya tukio kulikuwa na mvua iliyoambatana na radi ambayo ilipiga eneo walilokuwapo wanafunzi hao
Alisema radi hiyo mara baada ya kupiga ilisababisha vifo hivyo sita na kuwajeruhi wengine wawili waliokuwapo eneo hilo.
Pili aliwataja waliofariki ni Chesko Luoga, mwanafunzi wa mwaka wa pili, Lucas Mabula (mwanafunzi mwaka wa kwanza) Justin Ngonyani na Edwin Funga, wakazi wa Madaba, Hosana Antony Mkazi wa Mbinga na Eva Chapile mkazi wa Njombe ambao walikuwa wafanyakazi wa migahawa hiyo.
Muuguzi huyo aliwataja waliojeruhiwa ni Beatrice Mhagama  mwanafunzi mwaka wa tatu na Leokadia Fusi mkazi wa Madaba
Alisema majeruhi hao mara baada ya kufikishwa kwenye kituo cha afya Madaba na kuonekana wanahitaji matibabu zaidi walihamishwa kwenye hospitali ya rufaa ya Songea wanakoendelea na matibabu.
Muuguzi huyo alisema hali za majeruhi hao zinaendelea vizuri huku miili ya wanafunzi hao imehifadhiwa hospitali ya rufaa Songea na inatarajiwa kusafirishwa kwenda nyumbani kwao kwa mazishi.
Naye Mkuu wa chuo hicho, Darlington Nkenwa, alisema wamesikitishwa na vifo hivyo vilivyotokana radi iliyosababishwa na iliyoanza kunyesha saa 12 jioni hadi saa 5 usiku.
 Chanzo;Tanzania daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

WALIMU WALIOGOMA WATISHWA

WALIMU wa Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, walioshiriki kwenye mgomo uliolitikisa taifa, wametishiwa kuchukuliwa hatua za kisheria na hata kuwajibishwa endapo itabainika walishiriki.

Ofisa Elimu wa Wilaya ya Tunduru, Rashid Mandoa, aliiambia Tanzania Daima juzi kuwa walimu hao watachukuliwa hatua za kuwajibishwa kutokana na kukiuka taratibu za kufanya mgomo na watahesabiwa kama watoro katika siku walizoshiriki mgomo huo.

Akifafanua tukio hilo, alisema walimu hao watatakiwa kujutia kitendo hicho kutokana na kupotoshwa na uongozi wa Chama cha Walimu (CWT). Mandoa alisema tayari wamekwishatuma timu ya waratibu elimu kata na makatibu kata kutembelea shule zote wilayani humo, ili kubaini walimu walioshiriki mgomo huo.
Chanzo;Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa