Barua kwa kwa watumishi wa umma

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
meiomosi-2013Nawasalimuni nyote katika jina la nchi yetu nzuri Tanzania, Jina ambalo huko nyuma sote tuliliimba “Tazama ramani utaona nchi nzuri, yenye mito na mabonde mengi ya nafaka…nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzaniaaa!” Hakika wimbo huu vijana wengi siku hizi wanashindwa kuuimba, kwa nini? Uzuri wa taifa lao haupo tena, umepotezwa na baadhi yenu watumishi wa umma wasio na uadilifu. Sio siri vijana wetu kwa muda mrefu wameshindwa kujivunia taifa lao, wameshindwa kuongea mbele za watu kwa sauti kubwa kwamba wao ni Watanzania, uzuri wa taifa lao na sifa nzuri ya nchi yao imeharibiwa na vitendo kama ufisadi uliokithiri ambao umesababisha wachache katika taifa kunufaika huku wengi wakiteseka. Ndugu zangu watumishi wa umma, Ni kwa kupitia jina la nchi hii ndiyo leo nawaandikieni, kuwakumbusha juu ya wajibu wenu ambao kwa muda mrefu sana umekuwa hautimizwi ipasavyo! Kwanza kabisa niseme wazi kwamba nayafahamu mateso yenu, nayafahamu mahangaiko yenu ya maisha magumu, ambayo wakati mwingine yamefanya uaminifu wenu kutikiswa. Pamoja na hayo yote nasema hakuna jambo hata moja linalohalalisha kwenu ninyi kupoteza vigezo vitano muhimu vya utumishi wa umma ambavyo ni; 1.UADILIFU 2.UAMINIFU 3.KUSEMA KWELI DAIMA 4.UZALENDO NA DHAMIRA 5.HOFU YA MUNGU. Yeyote kati yenu aliyehalalisha kuondoka kwa vitu vitano nilivyovitaja hapo juu kwa sababu ya aidha kipato kidogo anachokipata serikalini, akavunjika moyo na kuacha kuwatumikia wananchi, ama akachagua kuendeleza rushwa na kukosa uzalendo, huyu hatufai kuwa mtumishi wa umma. Kwa muda mrefu mmekuwa mkilalamikiwa, mkinung’unikiwa na wananchi kwa sababu ya utendaji mbovu unaosababishwa na kukosekana kwa mambo matano niliyoyataja hapo juu, kwa kweli ilionekana kana kwamba uadilifu katika taifa hili hauwezekani tena, vivyo hivyo uaminifu, kusema kweli, uzalendo na hofu ya Mungu vilitoweka. Uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, 2015 na kumwingiza madarakani rais ambaye hawezi kumaliza hotuba yake bila kusema “TUNAMTANGULIZA MUNGU MBELE” Dk. John Pombe Joseph Magufuli umerejesha tena imani ya Watanzania kwamba, kumbe utumishi wa umma uliotukuka unawezekana, yote haya yamefanyika ndani ya siku chini ya arobaini tangu aingie madarakani! Kwa matendo yake hayo, nimesikia kwa masikio yangu watu waliompinga Rais Dk. Magufuli wakati wa kampeni wakijuta na kusema: “Laiti ningejua ningempa kura yangu!” haya yanatokea ndani ya siku chini ya hamsini tangu rais huyu aingie madarakani, upepo umebadilika, utumishi wa umma uliowekwa madarakani na watu kwa ajili ya watu kumbe unawezekana. Ule msemo wa wazungu usemao “Once you shake the top, you have shaken the bottom” yaani ukishatikisa juu, tayari utakuwa umetikisa na chini, sasa umedhihirika kwamba ni kweli. Tanzania inakimbia mbio, kuanzia serikalini mpaka kwenye sekta binafsi, adui uvivu ameanza kupotea kwa sababu tu raia aliyeingia madarakani sio mvivu. Kwa mara ya kwanza maishani mwangu nimeanza kusikiliza taarifa za habari na kusikia habari za kamatakamata, fukuzafukuza, kila kona ya nchi. kila kiongozi, kila mtendaji sasa anajaribu kutimiza wajibu wake, yote haya kwa sababu amebadilishwa mtu mmoja tu juu ambaye kauli mbio yake ni “HAPA KAZI TU!” Ndugu zangu Watumishi wa Umma, Nawaandikieni barua hii kuwakumbusha kwamba ile kauli yenu ya kusema “huu ni moto wa mabua” naomba muiache, anayesema hivyo hamfahamu vizuri rais wetu, kwa wanaomfahamu hawawezi hata siku moja kutoa kauli hiyo, haigizi, haya ndiyo maisha yake, ni kama mapafu ambavyo kazi yake ni kupumua, ndiyo ilivyo kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli. Ndugu zangu, Nawasihi mfanye kazi, timizeni wajibu wenu mliopangiwa kwa faida ya taifa hili, ambaye hatayasikia maneno haya, hakika ajiandae kukumbuka ninachokisema kwani mfumo utamtema! Ni wakati wa kuchapa kazi, si wa kuchati kwenye mitandao ya jamii saa ya kazi. Tukifanya jambo hili kwa pamoja, ninawahakikishieni taifa letu litasonga mbele kutoka hapa tulipo kwenda tunakotakiwa kwenda, rais wetu ni MUADILIFU, ndivyo itakavyokuwa kwa Makamu wake wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, serikali nzima na hatimaye vijijini, vivyo hivyo katika uchapakazi, kama rais wetu si mvivu, wavivu wote watang’oka, watake wasitake. Matarajio yangu ni kwamba kama watumishi wa umma mtatimiza vyema wajibu wenu, mtafanya kazi kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo wa hali ya juu, lazima kipato cha taifa letu kitaongezeka na maisha yenu yataboreshwa na rais huyu huyu tuliyemweka madarakani. Lakini niwasihi msipoteze hali yenu ya kujiamini kwa kusema “Rais ni mkali mno” matokeo yake mkawa ni watu wa kutekeleza mambo kwa nidhamu ya woga, taifa la watu wenye aina hii ya nidhamu, ambao hutekeleza mambo yao kwa kutaka tu kumfurahisha mkuu huwa halisongi mbele, matokeo yake huzaa hata uonevu kwa sababu tu mtu alikuwa anataka aonekane anafanya kazi. Sidhani rais wetu ni mtu wa aina hii, bali ni mtu anayependa kufanya kazi na watu wanaojiamini na wachapakazi na atakuwa tayari kujenga jamii ya watu wenye kujiamini si wanaotetemeka ovyo kila wanapokutana naye wakimpa ushauri anaopenda kuusikia, si ule anaotakiwa kuusikia hata kama hautamfurahisha. Nimeyasema haya kwa sababu msipokuwa makini wale mlioko madarakani, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi nk. Mtajikuta mkionea watu au kuwatoa watu sadaka kwa sababu tu mnataka kumfurahisha mkuu au muonekane mnafanya kazi na baadaye kupanda vyeo kwa gharama za maisha ya watu wengine. Sitaki kusema mengi siku ya leo, kwa haya machache niliyoyasema nawatakieni utendaji mwema wa kazi katika Awamu hii ya tano ya HAPA KAZI TU! Tendeni kazi zenu kwa kujiamini na uadilifu wa hali ya juu, nawahikikisheni awamu hii ya tano itabadilisha maisha yenu, kama anavyosema mwenyewe Rais Magufuli, tumuombee kwa Mungu atimize ndoto yake yakutufikisha kwenye nchi ya ahadi. Ahsanteni. NUKUU WASALAAM Eric Shigongo James

KIJANA FIKIRIA MARA MBILI KISHA WEKA TIKI KWA MGOMBEA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Bi. Samia Suluhu Ahaidi Umeme Kila Kijiji Ruvuma, Viwanda vya Mahindi, Kahawa

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu (katikati) akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini, Martin Mtonda (kushoto) na mgombea udiwani wa CCM.


MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu ameanza ziara yake mkoani Ruvuma akiinadi ilani ya chama hicho huku akiahidi neema kwa wakulima wa kahawa na mahindi wa mkoa huo.

Bi. Samia Suluhu ambaye amehutubia mikutano mitatu katika majimbo mawili ya mkoa wa Ruvuma yaani Jimbo la Nyasa na Mbiga Vijijini, akizungumza katika mikutano yake amesema serikali itakayoundwa na CCM endapo itashinda itahakikisha inashusha umeme katika vijiji vyote vya mkoa huo kwa awamu ili kuchochea maendeleo ya wananchi.

Alisema kwa kuwa mkoa huo unazalisha mazao ya mahindi na kahawa serikali itahakikisha inaanzisha viwanda eneo hilo vya kusaga na kuandaa unga wa mahindi kwa wakulima na kuwawezesha ili wauze unga na kunufaika zaidi tofauti na ilivyo kwa sasa ambapo wamekuwa wakilanguliwa.

Alisema viwanda vingine ambavyo Serikali ya CCM itavianzisha ni pamoja na viwanda vya kubangua kahawa na kuiandaa kikamilifu tayari kwa kutumika, jambo ambalo alisema licha ya kuongeza thamani ya zao hilo itaongeza ajira kwa vijana na kuchochea uchumi wa wakulima eneo hilo.
Akizungumzia miundombinu ya barabara ambayo bado ni changamoto kwa mkoa huo hasa vijijini alisema serikali itakayoundwa na CCM chini ya uongozi wa Dk. John Pombe Magufuli pamoja na yeye watahakikisha wanajenga na kuboresha barabara za maeneo hayo ili ziweze kupitika kwa uhakika.

Hata hivyo kiongozi huyo amesema Serikali itakayoundwa na CCM endapo itashinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2015 imejipanga kuboresha vizuri huduma za afya kuondoa ukiritimba na rushwa, elimu kwa kutoa elimu bure toka darasa la kwanza hadi kidato cha nne pamoja na ujenzi wa mabweni na uwezeshaji vijana na akinamama kiuchumi popote walipo mjini na vijijini.

Ziara ya mikutano ya kampeni ya mgombea mwenza huyo wa urais tiketi ya CCM, inaendelea leo katika Mkoa wa Ruvuma na ataingia Jimbo la Tunduru kuendelea kuinadi ilaya ya chama hicho kuomba ridhaa kwa wananchi ili waweze kurejeshwa madarakani na kuunda dola.

Pichani juu ni baadhi ya wananchi na wanaCCM wakiwa wamefurika katika kiwanja cha Kijiji cha Maguu Wilaya ya Mbinga kumsikiliza mgombea mwenza wa urais kupitia tiketi ya CCM alipokuwa akiinadi ilani ya chama hicho.


Pichani juu ni baadhi ya wananchi na wanaCCM wakiwa wamefurika katika kiwanja cha Kijiji cha Maguu Wilaya ya Mbinga kumsikiliza mgombea mwenza wa urais kupitia tiketi ya CCM alipokuwa akiinadi ilani ya chama hicho.
Baadhi ya wananchi na wanaCCM wa Kijiji cha Maguu wilayani Mbinga wakimsubiri mgombea mwenza wa urais, CCM, Bi. Samia Suluhu. 


Pichani juu ni baadhi ya pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda zilizompokea mgombea mwenza wa CCM urais, Bi. Samia Suluhu mara baada ya kuingia Wilaya ya Mbinga zikiwa zimeegeshwa pembeni huku mkutano wa hadhara ukiendelea. 

Mmoja wa wajumbe wa kamati ya kampeni ya mgombea mwenza, Bi. Asumpta Mshama akizungumza na wanaCCM na wananchi (hawapo pichani) katika Kijiji cha Maguu, Wilaya ya Mbinga. 
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu (kulia) akizungumza na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu, kabla ya kuanza kuhutubia katika mikutano wake wa kampeni.  

Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu (katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi wa CCM ambao ni wenyeji wake mkoa wa Ruvuma.

Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu (katikati) akizungumza na mmoja wa vijana walemavu waliohudhuria mkutano wake wa hadhara Kijiji cha Maguu. Bi. Suluhu alimsaidia fedha kijana huyo. 

*Imeandaliwa na www.thehabari.com

LOWASSA AENDELEA "KUTISHA" MAELFU WAFURIKA KUMSIKILIZA HUKO RUVUMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

MGOMBEA kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, akiwapungia maelfu ya wananchi akiwa kwenye gari, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Matarawe, Songea Mjini, Mkoani Ruvuma leo Septemba 1, 2015 ambapo alihutubia mkutano wa kampeni ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni akiwa kwenye mkoa watatu baada ya kuzindua rasmi kampeni zake jijini Dar es Salaam. Mh. Lowassa ameendelea kuonyesha "nguvu" zake kisiasa kutokana na maelfu ya wananchi wanaojitokeza kwenye mikutano yake. (Picha zote na Othman Michuzi)

DK MAGUFULI AKISHINDA URAIS AAHIDI SERIKALI KUJENGA RELI KUTOKA MTWARA HADI MBAMBA BAY RUVUMA, KUPUNGUZA BEI YA VIFAA VYA UJENZI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni wa CCM kumnadi mgombea urais Dk John Magufuli  wilayani Masasi leo. Dk Magufuli amesema kuwa CCM ikishinda Serikali  itajenga Reli kuanzia Mtwara hadi Mbamba Bay Ruvuma
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akijinadi katika mkutano wa kampeni mjini Masasi, mkoani Mtwara leo.
 Mfuasi wa CCM  akiwa amejichora usoni huku kidevuni akiwa aqmeandika jina la Mgombea Urais wa Tanzania kuptia CCM, Dk Magufuli.
 Wananchi wakishangilia wakati Dk Magufuli akitoa ahadi mbalimbali za maendeleo endaqpo akichaguliwa
 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika leo wilayani Namtumbo, Ruvuma. Dk Magufuli alitangaza kwamba akichaguliwa atahakikisha vifaa vya ujenzi bei yake inashuka kupunguza kodik.
 Dk Magufuli akionesha  Ilani ya Uchaguzi kabla ya kumkabidhi Mgombea ubunge jimbo la Namtumbo. Injinia Edwin Ngonyani
 Mama mkazi wa Kijiji cha Chomolo, wilayani Namtumbo, mkoani, akishangilia baada ya Dk Magufuli kutangaza kwamba akishinda urais kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne hawatolipa ada
 Dk Magufuli akihutubia baada ya kuzuiwa  na wananchi katika Kijiji cha Kilimasela wilayani Namtumbo, alipokuwa akienda kufanya kampeni Masasi mkoani Mtwara
  Dk Magufuli akihutubia baada ya kuzuiwa  na wananchi katika Kijiji cha Kilimasela wilayani Namtumbo, alipokuwa akienda kufanya kampeni Masasi mkoani Mtwara
  Dk Magufuli akihutubia baada ya kuzuiwa  na wananchi katika Kijiji cha Nandembo  wilayani Tunduru, alipokuwa akienda kufanya kampeni Masasi mkoani Mtwara
  Dk Magufuli akihutubia baada ya kuzuiwa  na wananchi katika Kijiji cha Matemanga wilayani Tunduru.
 Akina mama wakiwa karibu na mti wenye picha ya Mgombea urais kupitia CCM, Dk John Magufuli
 WAFUASI WA ccm wakishangilia wakati Dk Magufuli akijinadi
 Ni furaha iliyoje kwa Bibi kizee huyu baada ya kumuona Dk Magufuli wakati wa mkutano wa hadhara mjini Tunduru leo
 Dk Magufuli akijinadi katika mkutano wa kampeni mjini Tunduru
 Mrembo akiwa amejiremba ki ccm katika mkutano huo wa kampeni mjini Tunduru
 Baadhi ya wananchi wakiwa juu ya ukuta ili wapate kumuona Dk Magufuli akihutubia mjini Tunduru
 Dk Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Tunduru Kaskazini, Ramo Makani
 Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya Dk Magufuli
 Dk Magufuli akiwapongeza wafuasi wa CUF  waliokihama chama hicho na kujiunga na CCM KATIKA MKUTANO WA HADHARA ULIOFANYIKA MJINI TUNDURU
 Mambo ya warembo wa ccm
 Msafara wa Dk Magufuli ukiwasili  katika Kijiji cha Ligunga, wilayani Nanyumbu, Mkoa wa Mtwara

 Mwanafunzi  akiwa akiparamia mti ili aweze kumuona Dk Magufuli
Dk Magufuli akihutubia wananchi waliomzuia katika Kijiji cha Michiga, wilayani Nanyumbu alipokuwa akienda Masasi kuendelea na kampeni

DK MAGUFULI AZIDI KUNOGESHA KAMPENI ZA CCM ZA URAIS MKOANI RUVUMA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Pombe Magufuli akiwapungia mikono wananchi ikiwa ni ishara ya kuwasalimia alipowasili kwenye mkutano wa kampeni mjini Mbinga, Mkoa wa Ruvuma leo, ambapo aliahidi kuboresha kiwanda cha kukoboa kahawa na kujenga barabara ya lami kutoka Mbinga hadi Mbamba bay.
 Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Songea mjini kwenye uwanja wa majimaji ambapo aliwaeleza wananchi hao kuwa Serikali yake itafanyakazi kwa ajili ya maendeleo ya watanzania.
 Mbunge wa zamani wa Jimbo la Songea Mjini, Dk. Emmanuel Nchimbi  akiwaomba wananchi wa Ruvuma kumpigia kura Mgombea urais wa Tanzania kupitiaa CCM,, dK John Magufuli waqkati wa mkutano wa kampeni wa CCM kwenye Uwanja wa Maji Maji Mjini Songea, mkoani Ruvuma. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mgombea urais wa Tanzania kupitiaa CCM,, dK John Magufuli akiwa na watoto aliowapatia zawadi alipokuwa akiondoka baada ya kujinadi katika Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma
 Mwananchi akimpigia makofi Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk Magufuli baada ua kufurahishwa na hotuba yake katika Kijiji cha Kigonsera, wilayani Mbinga, Ruvuma leo.
 Dk Magufuli akisalimiana na dada wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Nyasa kupitia CCM, na mhamasishaji Mkuu wa CCM, marehemu Kapteni John Komba, alipokwenda kutoa shada la maua kwenye kaburi  Kapteni Komba katika Kijiji cha Lituhi, wilayani Nyasa, mkoani Ruvuma akiwa katika ziara ya kampeni za urais, ubunge na udiwani
 Dk Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Kapteni Komba
 Dk Magufuli na viongozi wengine wa CCM, wakiomba dua kwenye kaburi la marehemu  Kapteni Komba
 Ngoma ikitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni za urais, ubunge na udiwani katika Kijiji cha Lituhi, Wilaya ya Nyasa
 Dk Magufuli akinadi kwa wananchi katika Mji wa Lituhi, Wilaya ya Nyasa, Ruvuma
 Dk Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Nyasa, Stelah Manyanya katika mkutano wa kampeni katika Mji wa Lituhi
 Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya Dk Magufuli
 Dk Magufuli akimvisha kofia ya CCM, aliyekuwa Mwenyekiti Mtedaji wa Kijiji cha Kwanza Kata ya Lituhi, kupitia Chadema, Sixbert Nyembo baada ya kutangaza kuwa yeye na wenzie zaidi ya 270 kukihama chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Lituhi, wilayani Nyasa leo
 Wananchi wakimshangilia Dk Magufuli katika wakati msafara wake ulipozuiwa katika Kijiji cha Rwanda, wilayani Mbinga
 Wananchi wakishangilia katika Kijiji cha Amani  walipomuona Dk Magufuli wakati msafara wake ulipozuiwa katika Kijiji hicho kilichopo wilayani Mbinga
 Msafara wa Dk Magufuli ukipita kwenye Barabara mpya ya lami inayotoka Songea kwenda Mbinga
 Dk Magufuli akishangiliwa alipokuwa akiwahutubia wakati wa Kijiji cha Kigonsera waliomzuia alipokuwa akienda kwenye kampeni mjini Mbinga
 Dk Magufuli akiwasamia wananchi alipowasili kwenye mkutano wa kampeni mjini Mbinga
 Dk Magufuli akihutubia wananchi na kutoa ahadi mbalimbali atakazozitekeleza akiwa chaguliwa kuwa rais ambapo alisema kuwa kila kijiji kuanzia mwakani kitapewa sh. mil. 50 za kuwakopesha vijana na akina mama
 Dk Magufuli akimkabidhi Mgombea Ubunge Jimbo la Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda Ilani ya Uchaguzi ya CCM wakati wa mkutano huo wa kampeni
 Dk Magufuli akionesha Ilani ya Uchaguzi ya CCM kabla ya kumkabidhi mgombea ubunge Jimbo la Mbinga Vijijini wakati wa mkutano huo
 Dk Magufuli akimsalimia mmoja wa walemavu waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni mjini Mbinga
 Sehemu ya wananchi walioshiriki kwenye mkutano wa kampeni za CCM katika Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma leo
 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi wakati wa mkutano wa kampeni katika Jimbo la Peramiho
 Mma mfuasi wa CCM akifurahi baada ya kumsikia Dk Magufuli akiahidi kuanzisha pensheni kwa wazee kuanzia mwakani
 Mgombea Ubunge Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama akipokea Ilani ya Uchaguzi ya CCM kutoka kwa Mgombea Urais kupitia chama hicho, Dk Magufuli wakati wa mkutano huo wa kampeni.
 Mgombea urais wa Tanzania kupitiaa CCM,, dK John Magufuli akiwapungia mkono wananchi kuwaaga baada ya kujinadi katika Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma
 Mgombea urais wa Tanzania kupitiaa CCM,, dK John Magufuli akiwapungia mkono wananchi kuwaaga baada ya kujinadi katika Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma

 Sehemu ya wanchi wa Ruvuma wakinyoosha mikono kukubali kumpigia kura Mgombea urais kupitia CCM, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa MajiMaji mjini Songea
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu nchini,  Amon Mpanju akiwashutumu viongozi wa upinzani akiwemo mgombea urais kupitia Umoja wa Katiba Wananchi Ukawa, Edward Lowassa kwa kitendo chake cha kuwadhihaki walemavu. Mpanju alikuwa akihutubia  katika mkutano wa kumnadi Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea
Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Songea mjini kwenye uwanja wa majimaji ambapo aliwaeleza wananchi hao kuwa Serikali yake itafanyakazi kwa ajili ya maendeleo ya watanzania.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa