Ruvuma yazalisha chakula kingi

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



Aidha, imeelezwa kuwa mkoa huo umezalisha tani 689,123 za mahindi ambalo ni zao la chakula, katika msimu wa mwaka 2014/2015. Uzalishaji huo ni sawa na ongezeko la asilimia 17.3 ikiwa ni ongezeko la asilimia 6.7 ya mavuno yaliyopatikana katika msimu wa kilimo wa mwaka 2013/2014.
Mkuu wa mkoa huo Said Mwambungu alisema hayo wakati akizungumza mjini hapa na wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma. Alihimiza wananchi kutobweteka kutokana na mafanikio hayo badala yake waongeze juhudi katika uzalishaji hasa katika kilimo.
Aidha alisema kwamba wastani wa pato kwa mtu mmoja limezidi kukua kutoka Sh 1,913,526 mwaka 2013/2014 hadi kufikia Sh 2,082,167 ambalo ni ongezeko la asilimia nane kwa mwaka 2014/2015. Mwambungu alisema, kwa takwimu hizo inaonesha mkoa wa Ruvuma ni mkoa wa tano ukitanguliwa na mikoa ya Dar es Salaam, Iringa, Kilimanjaro na Arusha.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa alisema lengo ni kushika nafasi ya kwanza ifikapo mwaka 2018.
Alisema, mkoa unaendelea kupiga hatua nzuri katika ukuaji wa uchumi unaoendana na kuboresha maisha ya wananchi wake.
Mwambungu ametoa mwito kwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kusimamia na kuchukua hatua dhidi ya watu wanaohujumu kazi za kilimo ili usimamizi wake uende hadi katika ngazi ya kijiji. Alisema serikali itaendelea kuhakikisha wananchi hususani wakulima wanapata soko na bei nzuri ya mazao yao.

Chanzo: Gazeti la Habari leo

HIZI NDIZO SABABU ZILIZOPELEKEA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI NAMABENGO ILIYOPO MKOANI RUVUMA KUANDAMANA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wanafuzi 106 wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Namabengo wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wameandamana kwenda kumwona mkuu wa mkoa Said Mwambungu kumpelekea malalamiko dhidi ya vitendo vya udharirishaji wanavyofanyiwa na makamu mkuu wa shule hiyo Shaibu Champunga. Ebu wasikilize kupitia RUVUMA TV on Line.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa