Tutangaze vivutio vya kiutamaduni: Prof. Elisante Ole Gabriel

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

eli1 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma  Bw  Hassan Bendeyeko  akifungua kikao  kati ya wadau wa Sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Wizara husika kilichofanyika Mjini Songea Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel na  kulia ni Afisa Elimu MkoaBw.Gharama Kinderu
eli2 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo akisikiliza maelezo ya baadhi ya vifaa vilivyotumika katika vita ya Majimaji kutoka kwa Afisa Elimu Makumbusho ya Taifa  Bi. Blantina Raphael wakati alipotembelea makumbusho hayo mjini Songea, katikati ni Afisa Elimu wa Mkoa wa Ruvuma  Bw.Gharama Kinderu. picha na Zawadi Msalla- WHUSM Ruvuma

Na Zawadi Msalla- WHUSM Ruvuma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel ametoa wito kwa viongozi na wadau wa sekta ya Utamaduni wa Mkoa wa Ruvuma kutangaza Utamaduni na Utalii unaopatikana katika mkoa huo.
Wito huo umetolewa jana mjini Songea na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipokuwa akizungumza na wadau wa sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika ofisi za mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
“Mkoa wenu una vivutio vingi vya asili vinavyoonesha tamaduni za wanaruvuma  ambavyo vikitumika vizuri ni fursa nzuri ya mapato” alisema Prof Gabriel.
Ameongeza kuwa Mkoa wa Ruvuma una vivutio vingi vya Utamaduni  vya kuvutia watalii ambavyo ni fursa nzuri ya kutangaza Utamaduni wa Mkoa na Tanzania kwa ujumla.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Hassan Bendeyeko alikiri kuwepo kwa changamoto ya kuvitangaza vivutio hivyo kutokana na ubovu wa miundombinu iliyopo .
Hata hivyo  alisema kuwa ujenzi wa miundombinu utasaidia vivutio hivyo kufikika kwa urahisi na wanategemea Mkoa huo kuinuka kiuchumi hasa baada ya changamoto hiyo kutatuliwa.
Bw.Bendeyeko alisema kuwa baadhi ya vivutio vya kiutamaduni vinavyo hitaji kutangazwa ili vifahamike ndani na nje ya nchi ni pamoja na Makumbusho ya Majimaji, eneo waliponyongwa wapiganaji wa vita vya majimaji, Ziwa Nyasa pamoja na mbuga mbali mbali.
Aidha alieleza kuwa wanatarajia kuajiri Maafisa Utamaduni wakutosha  katika kila Halmashauri ambapo  kwa kushirikiana na Maafisa Habari na waandishi wa habari kutangaza vivutio hivyo.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa