KLABU YA MAJIMAJI YAJA NA MIKAKATI MIPYA YA MSIMU HUU WA LIGI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  

Mwenyekiti wa majimaji ambaye amechaguliwa hivi karibu bwana steven Ngonyani amesema msimu huu mpaya wa ligi kuu TANZANIA bara lazima klabu hiyo ichukue ubigwa.NGONYANI AMESEMA  mara baada ya kuchaguliwa kwa asilimia 93.5 na anachukua nafasi hiyo iliyoachwa wazi na mtangulizi wake HAMPHREY MILANZI aliyemaliza muda wake huku wajumbe 6 wamechaguliwa isipokuwa makamu mwenyekiti ameshindwa kupatikana sababu ya kukosa vigezo. 

KWA HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE.  

UKAGUZI WA MAZINGIRA YA SHULE YA MSINGI LITOLA WILAYA YA NAMTUMBO MKOANI RUVUMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 MKURUGENZI wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Christopher Kilungu katikati akikagua mazingira ya Shule ya msingi Litola ikiwa ni pamoja na ujenzi mpya wa matundu 12 ya vyoo vya wanafunzi wa shule hiyo. Picha na Yeremias Ngerangera

VIDEO:SHULE YA SEKONDARI LONDONI YASHIKA NAFASI YA KWANZA KATIKA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA KWA MANISPAA YA SONGEA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
  Shule ya sekondari LONDONI iliyopo katika manispaa ya SONGEA mkoani RUVUMA, ni kati ya shule zilizofanya vizuri katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2017 ambapo kwa mwaka 2017 imeshika nafasi ya kwanza katika manispaa ya SONGEA huku kimkoa imeshika nafasi ya nne.HABRI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE.

KATIBU MKUU CHADEMA KORTINI, LISSU ‘AJIFICHA’

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

 Imeandikwa na Muhidini Amri, Songea
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Vincent Mashinji pamoja na viongozi watano wa chama hicho wakiwemo wabunge wawili, wamefi kishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Ruvuma, wakikabiliwa na makosa mawili ikiwemo kufanya mkusanyiko uliotishia usalama wa nchi.
Dk Mashinji alifikishwa mahakamani hapo jana na wanachama wengine watano wakiwa chini ya ulinzi mkali wa askari Polisi wa Kituo Kikuu cha Polisi Songea Mjini. Walisomewa mashitaka mawili ya kufanya mkusanyiko usio halali na kufanya maandamano kinyume cha sheria, ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wa nchi.
Akisoma mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Ruvuma, Simon Kobelo, Wakili Mfawidhi wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kanda ya Songea, Renatus Mkude alidai Julai 15, mwaka huu mjini Mbamba Bay wilayani Nyasa, washitakiwa walikamatwa na Polisi wakiwa katika maandamano bila kuwa na kibali.
Aidha, Mkude alifafanua kuwa kosa lingine ni kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria, hivyo kuhatarisha usalama wa nchi. Katika kesi hiyo ya jinai namba 113 ya mwaka 2017, mbali na Dk Mashinji, washitakiwa wengine ni wabunge Zubeda Sakuro wa Viti Maalumu na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kusini Masasi na mbunge wa Ndanda kupitia chama hicho, Cecil Mwambe.
Wengine ni Katibu wa Ulinzi wa Taifa wa Chadema, Sanuda Madawa, Katibu Mwenezi Kanda ya Kusini Masasi, Charles Makunguru na Katibu wa Chadema Kanda ya Kusini Masasi, Filbert Ngatunga.
Washitakiwa baada ya kusomewa mashitaka yao, walikana kutenda makosa hayo. Hata hivyo wakati wanasheria wa Chadema wakikamilisha taratibu ya dhamana, Jeshi la Polisi liliwachukua washitakiwa na kuwapandisha kwenye gari na kuwapeleka rumande hadi kesho, ambapo kesi hiyo itatajwa tena.
DK Mashinji na wanachama hao walikamatwa Julai 15, mwaka huu katika mji mdogo wa Mbamba Bay wilayani Nyasa na Jeshi la Polisi Wilaya ya Nyasa wakiwa katika maandamano na kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria, licha ya serikali kuzuia mikutano yote vyama vya siasa.
Baada ya washitakiwa hao kushikiliwa na polisi wilayani Nyasa kwa saa 48, walipata dhamana kabla ya Jumanne na kupelekwa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa mjini Songea, kabla ya jana kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.
Upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Edson Mbogoro ulilalamikia kitendo cha wateja wao, kupelekwa mahabusu kwani hakimu tayari alishatoa ruhusa ya dhamana kwa washitakiwa, jambo ambalo alisema ni kinyume cha taratibu.
CHANZO HABARI LEO

VIDEO:WATAALAMU WA AFYA WAMETAKIWA KUJENGA MAZOEA YA KUWATEMBELA WAGONJWA MARA KWA MARA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Zaidi ya asilimia 80 ya saratani za mlango wa kizazi hutokea katika nchi zinazoendelea, Tanzania ikiwa nchi mojawapo ukilinganisha na Nchi nyingine,kutoka na tatizo hilo maganga mkuu wa mkoa wa ruvuma goziberth mutayhabarwa amewataka wataalamu kuwa na desturi ya kuwa angalia wagonjwa pale wanapokuja kucheki afya zao.Rai hiyo ameitoa wakati wa kufungua mkutano wa siku mbili wa kuhamasisha timu za afya kuhusu saratani ya mlango wa kizazi ,matiti na kifua kikuu.HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE.

VIDEO: WALIOCHAGULIWA KWENYE USAILI KUSHIRIKI UCHAGUZI WA KLABU YA MAJIMAJI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Hatimaye orodha ya MAJIMAJIya waliochaguliwa kwenya usaili wa klabu ya MAJIMAJI yaanikwa hadharani kwa habari kamili angalia video yake.

VIDEO: KAMA HUNA SIFA HIZI USIJE KWENYE USAILI WA KLABU YA MAJIMAJI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
katibu wa kamati huru ya uchaguzi wa KLABU ya MAJIMAJI ELISIUS NDUNGURU ametoa sifa za kugombea kwenye uchaguzi wa klabu ya majimaji utakaofanyika hapo AGOST 5 .

“ TUNDURU MPYA INAKUJA,TUPIGE KAZI KWA KUSHIRIKIANA ,HAKUNA KITAKACHOSHINDIKANA” DC TUNDURU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera
Wilaya ya Tunduru ni moja kati ya Wilaya tano za Mkoa wa Ruvuma, Ni wilaya iliyokuwa nyuma kimaendelea kuanzia miundo mbalimbali japo ni wilaya iliyojaa utajili wa madini. Mkuu wa wilaya hiyo Juma Homera anakuja na na mkakati wa Tunduru Mpya , fuatilia ujue ni upya gani anakuja nao ambao utaiweka tunduru kuwa ya kisasa.

VIDEO – UMEWAHI KUSOMA KITABU CHA NEEMA YA GESI NA MAFUTA TANZANIA? MAWAZO YA MWANDISHI NA HATUA ZA RAIS ZINAENDANA?

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Albano Midelo ni Mwandishi wa kitabu cha Neema ya Mafuta na Gesi Tanzania, Azungumzia sababu za kuandika kitabu hicho ambacho kimeanza kuzaa matunda kutokana nay ale aliyoyaandika, Je amepata mafanikio gani katika uandishi wa kitabu hicho ? pia azungumzia vitabu vingine anavyoviandaa kuviingiza sokoni.

VIDEO:RPC RUVUMA- MADEREVA PIKIPIKI JAMII INATAMBUA HUDUMA ZENU.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Madereva pikipiki maarufu kwa jina boda boda wametakiwa kujitambua wao ni watu muhimu katika jamii inayowazunguka kutokana na huduma wanazotoa,Kauri hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa RUVUMA GIMINI MUSHY , wakati akizungumza nao katika ukumbi wa Songea Club uliopo Wilaya ya Songea Mkoani RUVUMA.habari kamili hii hapa video yake

VIDEO:RUSHWA NI ADUI WA HAKI WANACCM.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Katibu wa chama Cha MAPINDUZI CCM mkoa RUVUMA AMINA IMBO amewataka wale wote watakaochukua fomu za kugombea katika ngazi za wilaya na mkoa kuachana na tabia za kupiga kampeni kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria za chama cha mapinduzi.HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE.

VIDEO:TAMASHA LA MAJIMAJI SEREBUKA KUTIMU VUMBI JULAI 22 HADI 30

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Msimu wa tatu wa tamasha la MAJIMAJI SEREBUKA linaloandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali Songea Mississipi, linatarajia kuanza julai 22 mwaka huu,Huku mishezo mbalimbali itahusishwa ikiwemo riadha,ngoma za asili,maonyesho ya kiabiahara na mdahalo,na nini hasa lengo la tamasha hilo huyu hapa mwenyekiti wa tamasha DAMASI NDUMBARO anabainisha. HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa