HATUTAKUWA KIKWAZO CHA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI - NAIBU WAZIRI JUMA AWESO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.                                                    
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso (wa kwanza kulia) akikagua sehemu ya mtambo wa kutibu na kusafisha maji wa Matogoro, pamoja na Meneja Ufundi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Songea (SOUWASA), Mhandisi John Kapinga.
 Mtambo wa kutibu na kusafisha maji wa Matogoro, Songea Mjini, mkoani Ruvuma
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (SOUWASA), Mhandisi Patrick Kibasa katika eneo la Misufini.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akishuka baada ya kukagua tanki la mradi wa Mtendewawa, wilayani Songea Mjini, mkoa wa Ruvuma.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amesisitiza kuwa wizara yake haitakuwa kikwazo cha utekelezaji wa ahadi ya Rais, Dkt. John Magufuli ya kuwapatia wananchi majisafi na salama, bali itasimimamia utekelezaji wa miradi hiyo ipasavyo ili ikamilike kwa wakati na kuleta tija.
Aweso alizungumza hayo katika ziara yake ya kikazi aliyoianza katika mkoa wa Ruvuma, ambapo anakagua utekelezaji wa miradi ya maji katika wilaya zote mkoani humo.

‘‘Niwahakikishieni  wizara haitakuwa kikwazo katika utekelezaji wa miradi ya maji nchini, zaidi ya kuhakikisha miradi yote tunayoitekeleza inaleta tija na kumaliza kero ya maji kwa wananchi kulingana na maagizo ya Rais. Hivyo, lazima fedha zifike kwa wakati na zitumike kwa usahihi ili miradi yote ikamilike kwa wakati kulingana na mikataba,’’ alisema Naibu Waziri.

‘‘Ni jukumu langu kusimamia hilo na ninawaagiza watendaji wote wasimamie miradi yote hatua kwa hatua na watoe taarifa sahihi za maendeleo yake, ili sisi viongozi tujue changamoto na kutoa msukumo katika kufanikisha miradi hiyo  itakayokuwa na tija na thamani halisi ya fedha zinazotumika,’’alisisitiza Aweso.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ametoa pongezi kwa SOUWASA kwa usimamizi mzuri wa miradi na hatua inazozichukua kwa nia ya kumaliza kero ya maji katika maeneo ya mji huo kama Midizini na Misufini ambayo yalikuwa na kero kubwa, lakini kwa sasa wananchi kukiri kupata huduma hiyo.

Katika ziara hiyo ameanza kwa kutembelea Wilaya ya Songea, ambapo ametembelea Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Songea (SOUWASA) na kuweza kuzungumza na menejimenti yake, pamoja na watumishi.

Aidha, alitembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa katika wilaya hiyo ikiwemo eneo la mradi wa Bwawa la Luhira, mtambo wa kutibu na kusafishia maji wa Matogoro, mradi wa upanuzi wa mtandao wa majisafi Songea.

Huduma ya maji kwa mji wa Songea kwa sasa ni asilimia 79, ambapo lita milioni 10.6 zinazalishwa kwa siku na mahitaji yakiwa ni lita milioni 14 kwa siku kwa wakazi wa mji huo. Upanuzi wa mradi wa maji wa Songea mjini unaondelea hivi sasa unategemea kuongeza upatikanaji wa maji kwa asilimia 90 kwa mji wa Songea.                  

WAZIRI MKUU AAGIZA WANAKIJIJI 21 KUFIDIWA ARDHI KABLA YA KRISMASI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Imeandikwa na Mwandishi Wetu
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chomolo wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, wakati waliposimamisha msafara wake jana ili kuzungumza naye. Waziri Mkuu alikuwa anaelekea Tunduru kuendelea na ziara ya kikazi mkoani humo. (Picha na Ofi si ya Waziri Mkuu).
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amempa mwezi mmoja Ofi sa Ardhi wa wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma, Maurus Yera awe ametafuta ardhi ya kuwafi dia wakazi 21 wa kijiji cha Lwinga wilayani humo ambao eneo lao lenye ukubwa wa ekari 101 lilitwaliwa na serikali mwaka 2008.
Eneo hilo lilitwaliwa kupisha ujenzi wa shule ya sekondari ya mkoa wa Ruvuma. Alitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi hao kupitia mabango, ambapo walimuomba awatatulie kero hiyo ya madai ya fidia ya ardhi iliyodumu kwa miaka 10 bila kupatiwa ufumbuzi.
Waziri Mkuu alisema haoni sababu ya Halmashauri hiyo kushindwa kuwafidia wananchi hao sehemu ya ardhi kwa muda wote huo ukizingatia wilaya hiyo ina hifadhi ya ardhi.
“Nataka wananchi hawa wawe wamelipwa fidia yao ya ardhi kabla ya siku kuu ya Krismasi ya mwaka huu. Serikali haiko tayari kuona wananchi wake waliotoa ardhi kupisha maendeleo wakisumbuliwa,” alisema.
CHANZO HABARI LEO 

WAZIRI MKUU AMPA OFISA ARDHI MWEZI MMOJA KUFIDIA WANANCHI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amempa mwezi mmoja Ofisa Ardhi wa wilaya ya Namtumbo Bw. Maurus Yera awe ametafuta ardhi ya kuwafidia wakazi wa kijiji cha Lwinga wilayani Namtumbo.

Wakazi hao 21 mwaka 2008 eneo lao lenye ukubwa wa ekari 101 lilitwaliwa na Serikali kupitia halmashauri ya wilaya hiyo kwa ajili ya kupisha ujenzi wa shule ya sekondari ya mkoa wa Ruvuma na waliahidiwa kulipwa fidia.Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana jioni (Alhamisi, Novemba 23, 2017) alipozungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Lwinga akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma.

Alitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi hao kupitia mabango, ambapo walimuomba awatatulie kero hiyo ya madai ya fidia ya ardhi iliyodumu kwa miaka 10 bila kupatiwa ufumbuzi.Waziri Mkuu alisema haoni sababu ya Halmashauri hiyo kushindwa kuwafidia wananchi hao sehemu ya ardhi kwa muda wote huo ukizingatia wilaya hiyo ina hifadhi ya ardhi.“Nataka wananchi hawa wawe wamelipwa fidia yao ya ardhi kabla ya siku kuu ya Krismasi ya mwaka huu. Serikali haiko tayari kuona wananchi wake waliotoa ardhi kupisha maendeleo wakisumbuliwa.”

Waziri Mkuu alisema Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli inataka kila mtumishi ahakikishe anatumia taaluma yake vizuri kwa kuwahudumia wananchi ikiwa ni pamoja na kutatua kero zinazowakabili kwa wakati.Pia Waziri Mkuu alitoa wito kwa wananchi hao kuhakikisha hawakubali kutoa rushwa pale wanapohitaji kupata huduma mbalimbali kutoka kwa watumishi kwa kuwa ni haki yao kuhudumiwa.

Aliwataka wananchi kuwa na imani na Serikali yao na kuiunga mkono katika mapambano dhidi ya rushwa kwani vitendo hivyo vinakwamisha shughuli za maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka watendaji kuhakikisha miradi wanayosimamia inakuwa na thamani inayolingana na kiasi cha fedha kilichotolewa na iwapo watabainika kwenda kinyume hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

“Lazima kiasi cha fedha kinachotolewa kugharamia mradhi kilingane na thamani ya mradi husika. Mfano tumetoa sh. milioni 70 kugharamia mradi na kukuta mradi uliojendwa ni wa sh. milioni 30 aliyeshughulikia ujenzi huo nasi tutamshughulikia hatutamuacha salama.”Awali, Waziri Mkuu alifungua ghala la kuhifadhiia mpunga na mchele katika wilaya ya Namtumbo lililojengwa na MIVARF na kisha alizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo na kuwataka wafanye kazi kwa bidii na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bibi Christine Mndeme alisema mkoa huo unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa masoko kwa mazao ya mahindi na mbaazi, ambapo Waziri Waziri Mkuu alisema sula hilo linashughulikiwa hivyo wananchi waendelee kuwa na subira.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
iJUMAA, NOVEMBA 24, 2017.

WAZIRI MKUU KUFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOANI RUVUMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa (Mb) anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Ruvuma kuanzia tarehe 23 - 25 Novemba, 2017.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 22 Novemba 2017 na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema Mheshimiwa Waziri Mkuu atawasili mjini Songea siku ya Alhamisi tarehe 23 Novemba, 2017 na kupokelewa na viongozi wa Chama na Serikali katika Uwanja wa ndege Songea majira ya 7.00 mchana.

Baada ya kuwasili atapokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa na ile ya Chama Tawala Uwanja wa Ndege Songea. Kisha ataelekea Wilaya ya Namtumbo ambapo atafungua ghala la MIVARF, kuongea na Madiwani na watumishi wa Umma na baadaye ataongea na wananchi wa Namtumbo kwenye mkutano wa hadhara. Ijumaa tarehe 24 Novemba, 2017 Mheshimiwa Waziri Mkuu ataendelea na ziara yake kwa kuongea na wananchi wa kijiji cha Mchomoro kisha ataelekea Wilaya ya Tunduru ambapo atasalimia na wananchi wa vijiji vya Rahaleo,Milonde na Matemanga akiwa njiani kuelekea mjini Tunduru.

Aidha, Mheshimiwa Waziri Mkuu atatembelea kituo cha Afya cha Nakayaya, ghala la kuhifadhia Korosho na kupata taarifa ya Chama Kikuu Cha Ushirika TAMCU. Jioni Mheshimiwa Waziri Mkuu ataongea na wananchi kwenye mkutano wa hadhara utakaofanyika mjini Tunduru katika uwanja wa michezo. Jumamosi tarehe 25 Novemba, 2017 Mheshimiwa Waziri Mkuu atahitimisha ziara yake mkoani Ruvuma na kurejea Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa Mndeme ametoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Ruvuma kujitokeza kwa wingi katika mapokezi kuanzia uwanja wa Ndege Songea atakapowasili Aidha amewaomba wananchi kujitokeza kwenye maeneo yote ambayo Waziri Mkuu atapita na kwenye mikutano ya hadhara ili wapate fursa nzuri ya kumsikiliza Mheshimiwa Waziri Mkuu na kupokea maelekezo atakayoyatoa.

VIDEO:RC RUVUMA AMEPIGA MARAFUKU KUMWITA MWANAFUNZI WAKIKE BABY.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amewataka wafunzi wakike waliopo mashuleni kuacha mara moja tabia ya kukubali kuitwa mababy hayo yamesemwa katika ziara yake ya siku moja katika shule ya NASULI iliyopo wilayani NAMTUMBO mkoani habari kamili hii hapa video yake

DKT. NDUMBARO AWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUZINGATIA UADILIFU, KUJITUMA NA KUWAJIBIKA KWA WANANCHI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akitoa maelekezo mbalimbali ya masuala ya kiutumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji mkoani Ruvuma. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hamashauri ya Wilaya ya Madaba Bw. Shafi Mpenda na kushoto kwakwe ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Bw. Bwai Biseko.
Baadhi ya watumishi wa Hamashauri ya Wilaya ya Madaba wakisikiliza kwa makini maelekezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) aliyoyatoa katika halmashauri hiyo, wakati ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji mkoani Ruvuma.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma, Bw. Biseko Bwai akitoa taarifa ya utekelezaji wa masuala ya kiutumishi kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu huyo mkoani Ruvuma yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijiji Bw. Simon Bulenganija akitoa taarifa ya utekelezaji wa masuala ya kiutumishi Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu huyo mkoani Ruvuma, yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Ibrahim Mahumi akitoa maelekezo kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini kuhusu taratibu zinazohusu menejimenti ya Rasilimaliwatu serikalini, wakati wa ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro ya kuhimiza uwajibikaji.
Baadhi ya watumishi wa Hamashauri ya Wilay ya Songea Vijiji wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi ya katibu mkuu huyo ya kuhimiza uwajibikaji katika Hamashauri hiyo.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro amewataka Watumishi wa Umma nchini kuzingatia uadilifu katika utendaji kazi, kujituma, kuwajibika kwa wananchi na kwa Serikali ili kujenga Utumishi wa Umma uliotukuka.

Dkt. Ndumbaro amesema hayo, katika ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani Ruvuma yenye lengo mahususi la kubaini changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma katika maeneo yao ya kazi na kuzitafutia ufumbuzi ili kuwawezesha watumishi kutekeleza majukumu yao ipasavyo, ikiwa ni pamoja na kuwasisitiza Watumishi wa Umma juu ya mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Dkt. Ndumbaro akiwa katika Halmashauri za Wilaya ya Madaba na Songea Vijijini amewaeleza watumishi wa halmashauri hizo kuwa, misingi ya uadilifu na uwajibikaji itajengwa na watumishi hao kwa kubadili utamaduni wa kufanya kazi kwa mazoea (business as usual).

Dkt. Ndumbaro amesema kwamba, Wakurugenzi pamoja na Wakuu wa Idara nchini wana jukumu kubwa la kusimamia utendaji kazi katika maeneo yao ya kazi ili kubadilisha tabia za baadhi ya watumishi wasiowajibika ipasavyo, na kuwafanya watekeleze wajibu wao kwa bidii na kwa uadilifu mkubwa.

“ Ninyi Wakurugenzi na Wakuu wa Idara mhakikishe mnahimiza nidhamu kwa Watumishi wa Umma katika maeneo yenu, mtumishi akikosea achukuliwe hatua mara moja kwa mujibu wa Sheria , Kanuni na Taratibu za Utumishi wa umma zilizopo” Dkt. Ndumbaro amefafanua.

Dkt. Ndumbaro amebainisha kuwa, kama kuna watumishi wasiotimiza wajibu wao na hawachukuliwi hatua zozote za kinidhamu au za kisheria dhidi yao, kitendo hicho huwakatisha tamaa watumishi wanaojituma katika utendaji kazi wao.

Aidha, Dkt. Ndumbaro amekemea tabia iliyojengeka kwa baadhi ya watumishi ya kuwakatisha tamaa watumishi wanaojituma na wanaozingatia maadili. “Viongozi tusipokemea na kuwachulia hatua watumishi wenye tabia ya kuwabeza na kuwakatisha tamaa watumishi wanaojituma kazini, ni dhahiri kuwa itashusha morali ya utendaji kazi wa watumishi wanaochapakazi” Dkt. Ndumbaro amesisitiza.

Dkt. Ndumbaro amewataka Wakurugenzi na Wakuu wa Idara kuwatambua watumishi wanaofanya kazi kwa bidii kwa kuwapa moyo na motisha, ikiwa ni pamoja na kuwaandikia barua za kuwapongeza ama kuwapa vyeti ikiwa ni mkakati wa kukuza utamaduni wa watumishi kupenda kufanya kazi.

Pia, Dkt. Ndumbaro hakusita kuwasisitiza Maafisa Utumishi, Watumishi wa Masijala na Makatibu Mahususi kuwa na lugha nzuri wakati wa kuwahudumia wateja wa ndani na wa nje pindi wanapofika kwao kupata huduma.

Dkt. Ndumbaro anaendelea na ziara ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji mkoani Ruvuma katika Halmashauri za Wilaya ya Songea Mjini, Tunduru, Mbinga, Nyasa, na Namtumbo.

VIDEO:RC MNDEME AKAGUA MRADI KUBWA WA KITUO CHA WAKULIMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Ujenzi wa kituo cha Mafunzo kwa wakulima OTC , kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya SONGEA, mkoani RUVUMA kimekamilika kwa asilimia 90 ili kiweze kutoa fursa ya kiuchumi, kwa kuwa kitakapokamilika kitatoa fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutangaza bidhaa za mazao yalimwayo mkoani RUVUMA.

VIDEO:RC.MNDEME AMEWATAKA WAKUU WA IDARA KUWA NA NIDHAMU KATIKA MATUMIZI YA FEDHA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mkuu wa mkoa wa RUVUMA, CHRISTINE MNDEME amewataka watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya SONGEA kujituma kufanyakazi kwa kutatua kero za wananchi badala ya kukaa ofisini.

VIDEO:CWT RUVUMA .WALIMU FANYENI KAZI KWA MAADILI .

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mjumbe wa kamati kuu taifa kutoka chama cha walimu Mkoa wa Ruvuma Mwalimu Sabina Lupukila ametoa wito kwa walimu wote nchini kuacha tabia za kutembea na wanafunzi kwani kufanya hivyo ni kukiuka maadili ya kazi na kulete taswira mbaya kwa jamii kwani mwalimu ni kioo cha jamii,habari kamili hii hapa video yake.

VIDEO:WATAKAO CHEZESHA MIZANI TUTAWAKAMATA .DC TUNDURU.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera amevitaka vyama vya ushirika wilayani hapo kuhakikisha wanatumia mizani yenye lengo la kumsaidia mkulima wa zao la korosho awezekupata matunda mema bala ya kulalamika kila siku hayo ameyasema wakati wa kuzindua mnada wa korosho katika kata ya nakapanya mkoani RUVUMA habari kamili hii hapa VIDEO YAKE.

VIDEO:CCM MKOA WA RUVUMA YATAMBA KUCHUKUA KATA ZOTE KATIKA UCHAGUZI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Chama cha mapinduzi ccm mkoa wa ruvuma kimepanga kushinda kata zote zinazoshiriki uchaguzi mwaka huu kwa zile zilizokumbwa na matatizo kama vifo na nk hayo yamebainishwa na katibu wa ccm mkoa wa ruvuma B.Amina imbo wakati akimweleza mkuu wa mkoa wa ruvuma b mndeme alipotembelea ofisini kwake.

VIDEO:RC .DODOMA NAKUKABIDHI MKOA WA RUVUMA UKIWA SALAMA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
aliekuwa mkuu wa mkoa wa RUVUMA ambaye ameamishiwa kanda ya kati DODOMA DKT BILINITH MAHENGE amekabidhi ofisi yake rasmi kwa mkuu wa mkoa wa RUVUMA BI.CHRISTINE MNDEME ili aweze kuwatumikia wananchi wa mkoa wa RUVUMA huku akimtaka kushirikaina vyema na wafanya kazi wa ngazi wote ili mkujenga nchi ya viwanda

VIDEO: RC MNDEME SIJAJA KUCHEZA NIMETUMWA NA RAIS KUFANYA KAZI .

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma B.Christina Mndeme amewataka viongozi wa mkoa wa Ruvuma na wilaya kuhakikisha wanashirikana katika kuuletea maendeleo mkoa,uki kiwataka kumpa ushirikiano zaidi TAARIFA KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE.

RC RUVUMA,AKABIDHI OFISI NA KUMWAGIZA RC MNDEME MAAGIZO MANZITO KUHUSU TANROAD RUVUMA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399Aliekuwa mkuu wa mkoa wa RUVUMA Dkt BILINITH SATANO MAHENGE ambaye sasa amekuwa mkuu wa mkoa wa DODOMA amemwagiza mkuu wa mkoa wa ruvuma CHRISTINA MNDEME kuhakikisha kuwa wakala wa barabara mkoa wa RUVUMA TANROAD wasiendeshe bomoa bomoa katika maeneo ya manispaa ya SONGEA kwa sababu wameshindwa kuendeleza barabara hizo na kama watafanya hivyo basi wahakikishe wanalipa pesa kwanza ndivyo wafanye zoezi hilo taarifa kamili hii hapa video yake.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa