MAGAZETI YA LEO JUMATATU TAR 27.07.2015

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
















LOWASSA AZIDI KUPATA MAPOKEZI MAKUBWA KILA ANAKOKWENDA, SONGEA ALAZIMIKA KUKAA JUU YA PAA LA NYUMBA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

WAZIRI Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa amesema hana shaka na swala la kukatwa jina lake katika vikao vya Chama cha Mapinduzi(CCM), kwani anaamini Chama chao kitatenda haki kwa kurudisha jina lake kuwa mgombea urais wa Tanzania.

Lowassa ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wa Mkoa wa Ruvuma katika ofisi kuu za CCM Mkoani humo, wakati akitoa shukrani baada ya kudhaminini na wanaCCM zaidi ya elfu 52.

"Nimekuwa mwanaCCM tangu mwaka 1977 nilipomaliza chuo kikuu, sijawahi kufanya kazi nje ya CCM hivyo nakijua chama na hakuna mgombea atakayeweza kuvunja rekodi ya utendaji wangu katika chama, sasa leo anayetaka kukata jina langu anatoka wapi? anakata kwa sababu gani? Sioni kosa la kukatwa jina na Watanzania hawaoni, kwa hiyo msiwe na wasiwasi jina litarudi tu". alisema Lowassa.

 Lowassa aliwasili Mkoani Ruvuma mapema mchana wa leo akitokea Mkoani Iringa kwaajili ya kusaka wadhamini katika mbio zake za kusaka urais kwa tiketi ya chama hicho, ambapo umati wa watu ulifurika kumlaki na kupelekea kufunga barabara kuu ya mjini, hali iliyompelekea Lowassa kupanda juu ya kibambaza cha jengo la ofisi ya CCM Mkoa ili aweze kuzungumza hao.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, akizungumza na Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma waliokuwa wamesimama nje ya Ofisi za CCM Mkoa huo, mjini Songea leo Juni 21, 2015, wakati alipofika kwa ajili ya kupata udhamini utakaomuwezesha kupata ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwasalimia wanaCCM na Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma. 
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Chifu wa Kabila ya Wangoni, Chifu Ally Yussuf Songea (97). Chifu huyo alikwendwa kwenye uwanja wa Ndege wa Songea kumpokea Mh. Lowassa.
Wakinamama wa Mkoa wa Ruvuma wakimfurahia Mh. Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono wanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.
Mmoja wa Wazee wa Mkoa wa Ruvuma, Mzee Ally Jaibu Rashid akitoa neno kwa niaba ya Wazee wa Ruvuma.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza machache na Wazee wa Mkoa wa Ruvuma.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiondoka kwenye viwanja vya CCM Mkoa wa Ruvuma.

WAZIRI BERNARD MEMBE AENDELEA KUPATA UDHAMINI WA KISHINDO KATIKA MKOA WA RUVUMA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (katikati) akilakiwa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliofika kumpokea nje ya Ofisi ya CCM Mkoa wa Ruvuma iliyopo mjini Songea jana, baada ya kuwasili mkoani humo kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 5,000.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiwapungua mkono wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi, waliofurika nje ya Ofisi ya CCM Mkoa wa Ruvuma iliyopo mjini Songea jana, baada ya kuwasili mkoani humo kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 5,000.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akilakiwa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vijana, waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa mjini Songea jana, baada ya kuwasili mkoani Ruvuma kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 5,000. Picha zote na John Badi
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akisoma moja ya mabango yenye ujumbe mbalimbali yaliyobebwa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vijana, waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa mjini Songea jana, baada ya kuwasili mkoani Ruvuma kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 5,000.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Odo Mwisho akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe, fomu zilizotiwa saini na wanachama wa CCM mkoani humo, waliofika kwenye Ofisi hizo jana, kwa ajili ya kumdhamini ili ateuliwe kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 5,000.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe, akizihakiki fomu zilizotiwa saini na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, kwa ajili ya kumdhamini ili ateuliwe kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo, Odo Mwisho (wa pili kulia), katika Ofisi za chama hicho mjini Songea jana, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 5,000.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Ruvuma, waliofika kwenye Ofisi ya CCM zilizopo mjini Songea jana, kwa ajili ya kutia saini fomu za kumdhamini ili ateuliwe kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 5,000.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (watatu kushoto), akipongezwa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Ruvuma, waliofika kwenye Ofisi ya CCM zilizopo mjini Songea jana, kwa ajili ya kutia saini fomu za kumdhamini ili ateuliwe kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 5,000. Wa pili (kushoto) ni Mkewe, Mama Dorcas Membe.
Wazee wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Ruvuma, wakimuembea dua maalum Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto), kwa ajili ya kumtakia kheri katika safari yake ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kupata wadhamini kutoka mkoa huo jana. Wa pili (kushoto) ni Mkewe, Mama Dorcas Membe.
John Badi

KUELEKEA MAJIMBONI: HALI SIYO SALAMA KWA CCM MAJIMBO YA MBINGA, PERAMIHO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Jimbo la Peramiho ni eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Songea, maarufu kwa jina la Songea Vijijini. Halmashauri hii inaundwa na kata 19, vijiji 74 na vitongoji 617 na kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 hapa Peramiho kuna wakazi 173,821 wanaume wakiwa 86,548, wanawake 87,273 na kuna wastani wa watu wanne katika kila kaya.
Peramiho ni kati ya majimbo ambayo yalikuwa na vuguvugu la mabadiliko mwaka 1995 kwenye uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi, japokuwa lilikuwa chini ukilinganisha na baadhi ya maeneo ya Ruvuma na mikoa jirani.
Vyama vinne vilijitokeza kuweka wagombea na dalili zilionyesha kuwa NCCR ndiyo ingekuwa tishio kubwa kwa CCM, bahati nzuri jambo hilo lilijiri pamoja na kuwa CCM haikuwa kwenye wakati mgumu sana.
Uamuzi wa wananchi kwenye masanduku ya kura yaliipa ushindi mkubwa kwa CCM na kuviacha vyama vingine vikiendelea kujifunza namna ya kupambana na chama hicho kikongwe siku za usoni.
Vyama vya Tadea na CUF vikiwasimamisha Yustin Liganga na Fulgence Kagaruki vilipata asilimia 2.2 ya kura zote kwa ujumla. Ally Madamba wa NCCR alijaribu kuvua asilimia 19.6 (kura 6,651) na Michael Mbilinyi wa CCM alichukua asilimia 78.2 (kura 26,539) na kuwa mbunge wa kwanza wa Peramiho chini ya mfumo wa vyama vingi.
Hata mwaka 2000 kwenye uchaguzi mkuu, Mbilinyi wa CCM ndiye aliibuka mshindi kwa mara ya pili, akiwaacha mbali wapinzani wake kutoka vyama vingine, akafanikiwa kuliongoza jimbo hili hadi mwaka 2005.
Ule uchaguzi wa “kimbunga” ulipowadia (mwaka 2005), CCM ilimuweka Mbilinyi pembeni na kumpa nafasi mwanamama machachari, Jenista Mhagama. Jenista hakuwa na kazi ya kutisha mwaka huo kwa sababu alikutana na wagombea wasio na mitandao mikubwa kutoka vyama vya Chadema, CUF na TLP. Mwisho wa siku mwanamama huyu aliwashinda kwa zaidi ya asilimia tisini ya kura zilizopigwa. Jenista alipata kura 46,480 (93.2%) huku vyama hivyo vitatu vikipata jumla ya asilimia 6.8 ya kura zote. Ndio tuseme, matokeo ya mwaka 2005 yalidhihirisha kuwa nguvu ya CCM imeimarika sana mwaka huo.
Matokeo mabaya kwa upinzani Peramiho yaliendelea mwaka 2010 wakati CCM iliposhinda kwa kishindo ikiwa tena na Jenista Mhagama. CCM ilichukua asilimia 89.43 (kura 28,782) na CUF, chama pekee kilichopambana na CCM kwenye uchaguzi huo, ikipata asilimia 8.21 (kura 2,642), mgombea akiwa ni Emmanuel Chilokota.
Katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwezi Disemba 2014, Katika jimbo la Peramiho Chadema na CUF zilipata zaidi ya vijiji 31 tofauti na mwaka 2009 wakati viliopokuwa na chini ya vijiji 10.
Ndiyo kusema kuwa vyama vya upinzani vinazidi kujiimarusha kwenye jimbo hili, japo vikifanya hivyo polepole sana. Kwa maoni yangu, ushindani mkubwa wa kulisaka jimbo hili mwaka huu utakuwa ndani ya CCM ambako makada mbalimbali wa chama hicho wamezidi kujiimarisha wakiwa na nia ya wazi ya kumuondoa Jenista ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Utaratibu wa Bunge).
Pamoja na kuwa vyama vya Chadema na CUF vina wagombea wazuri, tatizo kubwa lipo kwenye mtandao wa chama kulinganisha na CCM ambayo ina mtandao thabiti mno wakiviacha mbali vyama vingine. Pamoja na hali hiyo, ukweli unabakia kwamba jimbo la Peramiho si zuri kwa CCM miaka michache ijayo na lina kila dalili kwamba litashika kasi ya mabadiliko baada ya mwaka huu.
Wilaya ya Mbinga
Mbinga ni moja kati ya wilaya sita za Mkoa wa Ruvuma.. Kwa ujumla, wilaya ya Mbinga ina kata 45, vijiji 165 na vitongoji 1,108 na kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012. Mbinga kuna wakazi 203,309, wanaume ni 96,347, wanawake 106,962 na wastani wa watu wanne katika kila kaya.
Wilaya hii inaundwa na majimbo mawili ya uchaguzi, jimbo la Mbinga Magharibi na Mbinga Mashariki.
Jimbo la Mbinga Magharibi
Kama vyama vya upinzani, hususan Chadema, Tadea na NCCR vingekuwa na mpango wa pamoja, labda jimbo hili lingechukuliwa na upinzani mwaka 1995. Katika uchaguzi huo, CCM ilimsimamisha Dkt. Luoga Thadeus ambaye alishinda kwa kupata kura 11,331 (63.5%) akifuatiwa na Michael Mahecha wa NCCR aliyepata kura 2,622 (14.7%) na Neema Masanche wa Tadea alishikilia nafasi ya tatu kwa kura 2,567 (14.4%), huku mgombea wa Chadema, Gray Maltaka akishika nafasi ya mwisho kwa kupata asilimia 7 ya kura zote.
Ukichunguza kwa umakini utagundua kuwa kwenye uchaguzi huu vyama vya upinzani vilipata takribani asilimia 40 ya kura zote, jambo lenye maana kuwa kama vingelikuwa vimeweka mgombea mmoja vingeweza kabisa kupata asilimia zaidi ya 51 kutokana na kupigiwa kura za wananchi wasiofanya maamuzi haraka.
Kwenye uchaguzi wa mwaka 2000 yale yale ya 1995 yakajirudia. Huku NCCR ikionekana kuyumba na kupoteza mwelekeo kutokana na migogoro isiyokwisha ndani ya chama hicho, Dkt. Luoga Thadeus alisimamishwa na CCM kwa mara ya pili na kuwashinda wapinzani. CCM iliendelea kuliongoza jimbo hili hadi mwaka 2005.
Aliyewahi kuwa mwimbaji maarufu wa kikundi cha sanaa za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati akiwa ofisa, Kepteni John Komba (sasa marehemu), ndiye alikuwa mgombea wa CCM kwenye uchaguzi wa mwaka 2005 hapa Mbinga Magharibi.
Komba aliendesha kampeni zake kisayansi akitumia vizuri ustadi wa sauti na nyimbo zake. Wananchi wa Mbinga wanasema watu walijazana kwenye mikutano yake mwaka 2005 kwa sababu walikuwa na fursa adimu ya kumuona ‘LIVE” akitumbuiza na kisha baadaye akiwaomba kura. Wakazi hao walimruhusu Komba awe kiongozi wao. Walimpigia kura 32,773 (91.1%). Washindani wake kutoka TLP, Tadea, CUF, NCCR na Chadema waliambulia asilimia 8.5 ya kura zote.
John Komba alitumikia kipindi chake cha kwanza cha ubunge akitumia sehemu kubwa ya muda wake kuzunguka na viongozi wa CCM katika mikutano mikubwa ya kitaifa ambako alikuwa anatumbuiza na kuvuta wasikilizaji wengi, na kwa mtindo huu CCM ilikuwa inajipatia wasikilizaji na huenda kufanikiwa kuwashawishi wengine waunge mkono chama hicho.
Mwaka 2010, CCM bado ilikuwa imara Mbinga Magharibi, japokuwa upinzani uliendelea kukua kiasi. Walau mwaka huo vyama vilijipunguza vyenyewe na kubakia vine, huku CCM ikitaka tena mbunge wake John Komba apewe kipindi cha pili, jambo lililowezekana. Katika uchaguzi wa mwaka 2010 walau walioweza “kuvuta soksi” na kuipa CCM presha kidogo ni Chadema. Hata hivyo chama hicho kilifanikiwa kuchukuu asilimia 10 tu ya kura za CCM tofauti na mwaka 2010 wakati CCM iliposhinda kwa zaidi ya asilimia 90.
Katika uchaguzi huo, Gilbert Jamesa Zannie wa Chadema alipata kura 3,613 (15.26) na kuwa mshindi wa pili huku Kepteni John Komba akiwa na kura 18,969 (80.11%). Safari ya John Komba kuwaongoza wana Mbinga Magharibi hadi mwaka 2015 iliishia katikati, miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2015 alipofariki dunia.
Kabla ya kifo cha John Komba, niliambiwa kuwa ndani ya CCM hakukuwa na hofu ya kuporwa jimbo hili aidha na mtu mwingine zaidi ya Komba mwenyewe au mtu atokeaye upande wa upinzani. Kifo chake kimesababisha makada kadhaa wa CCM kuanza harakati za haraka tangu nyumbani kwake msibani Dar es Salaam hadi alipokwenda kuzikwa kijijini kwake ndani ya jimbo la Mbinga Magharibi.
Wanasiasa hao ndani ya CCM wanapambana kuwa karibu na familia ya Komba ili ikiwezekana, mmoja wa vijana wa John Komba ambaye alikuwa kipenzi cha baba yake aweze kuwaunga mkono na ikiwezekana kuwanadi ndani ya kura za maoni za CCM na hata kwa wananchi kwa kutumia ukuu wa jina la baba yake (marehemu) hapa jimboni.
Hata hivyo nilipowasiliana na kijana huyo sikumpata hewani hadi naamua kuchapisha uchambuzi huu. Lakini pia baadhi ya makada wa CCM wanaoishi Dar Es Salaam na wakiwa na nia ya kurithi viatu vya John Komba, wanasema kuwa huwenda mwanaye mmoja pia akaingia kwenye kinyang’anyiro cha kusaka ubunge ili kuendeleza sifa ya baba yake na labda kumalizia mipango ambayo alikuwa hajaikamilisha jimboni.
Vyama vya upinzani havikupata matokeo mazuri sana kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2014 japokuwa vimefanikiwa kushinda vijiji na vitongoji vingi mno kushinda mwaka 2009. Pamoja na hayo, CCM bado ina nguvu ya kujivunia sana hapa Mbinga Magharibi na sioni kama kuna dalili ya upinzani kutwaa jimbo hilo, badaye Oktoba mwaka huu.
Jimbo la Mbinga Mashariki
CCM ilitumia vizuri mwanya wa uchanga wa vyama vya upinzani katika jimbo hili, mara mfumo wa vyama vingi ulipotangazwa kuanza rasmi na kufuatiwa na uchaguzi mkuu wa kwanza wa kitaifa mwaka 1995.
Kwenye uchaguzi huo, chama hicho kikongwe kilimuandaa kada wake mkongwe, Kanzolo Komba ambaye alipata bahati ya kukutana na wagombea wa upinzani ambao hawakuna uwezo wa rasilimali fedha wala uzoefu wa kutosha wa siasa za ndani ya nchi. Chama kilichoonekana kuwa na nguvu hapa Mbinga Mashariki ni NCCR na mgombea wake Ndemiwaka Ndunguru.
Kura zilipopigwa na matokeo kuwekwa hadharani, upinzani haukweza kupoka kiti cha ubunge. Kanzolo Komba wa CCM alishinda kwa kupata kura 29,348 (76.9%) akafuatiwa na Ndemiwaka Ndunguru wa NCCR aliyekuwa na kura 5,760 (15.1%) huku wagombea wa CUF na TADEA kwa pamoja wakipata asilimia 8.1 ya kura zote. Kanzolo aliingia kwenye historia ya kuwa mwanasiasa aliyeliongoza jimbo hili katika kipindi cha kwanza cha mageuzi ya kisiasa Tanzania.
Mwaka 2000 bado CCM iliendelea kujipanga huku NCCR ikiwa dhoofu. Ngwatura Ireneus ndiye alikuwa mgombea wa chama hicho kilichokuwa na mbunge hapa Mbinga Mashariki. Mgombea huyu alitumia faida ya kuparaganyika kwa upinzani na akafanikiwa kushinda kwa kura nyingi. Na ndiye ameingia katika rekodi kama mbunge wa pili wa CCM jimboni hapa, tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.
Ilipofika mwaka 2005, taratibu za uteuzi ndani ya CCM ikiwemo kura ya maoni zilimbwaga Ngwatura Ireneus na kumpa nafasi kada mwingine wa chama hicho, Gaudence Kayombo. Baada ya Ireneus kukosa nafasi ya kuendeleza kipindi cha pili, alilalamika waziwazi kwamba amechezewa michezo michafu na viongozi wenzie akiwemo huyu Gaudence Kayombo aliyeshinda.
Kura za jumla zilipopigwa, Gaudence Kayombo wa CCM ndiye aliibuka mshindi wa kwanza dhidi ya wagombea kutoka vyama vya TLP, CUF na Chadema. Gaudence Kayombo alipata kura 82,277 (89.1%), akifuatiwa kwa mbali sana na mgombea wa Chadema, Masendi Lupogo Pancras aliyepata kura 7,520 (8.1%) huku Elzear Kawonga wa CUF akiambulia asilimia 1.8 ya kura zote.
Gaudence Kayombo alifanikiwa kuanza uongozi wa jimbo hili kwa maana ya mwakilishi wa wananchi na mshindani wake wa kisiasa ndani ya CCM, mbunge wa jimbo hili mwaka 2000 – 2005, Ngwatura Ireneus, alihamia Chadema na kuanza harakati za kusaka ushindi kupitia upinzani.
Ndiyo maana kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 CCM ilitishika sana, naambiwa ikajipanga kwa hali na mali na viongozi wakubwa wakapelekwa kuweka sawa hali ya mambo. Hofu ya CCM ilikuwa kwamba chama hicho kinapambana na mgombea ambaye amewahi kuwa mbunge wa jimbo hili kwa miaka mitano na amewahi kuwa kada wa CCM kwa kipindi kirefu na kwa hiyo alitegemewa kuwa na ushawishi mkubwa ndani ya CCM na kwa wananchi kwa ujumla.
Mipango na mikakati ya CCM kumdhibiti kada wao wa zamani ambaye mwaka 2010 aligombea kwa tiketi ya Chadema, ilifanikiwa. Mpambano kati ya CCM na Chadema uliishia kwa CCM ikiongozwa na Gaudence Kayombo kupata ushindi wa asilimia 88.88 (kura 54,645) huku Chadema ikiwakilishwa na Ngwatura Ireneus, kupata asilimia 9.06 (kura 5,598). Matokeo haya yalimshangaza kila mwana Mbinga Mashariki kwa sababu yalikuwa mapambano ya vigogo kwa vigogo.
Lakini baadhi ya wananchi wanasema kuwa kulikuwa na dalili zote kuwa Ngwatura angeangushwa kwa sababu alipokuwa mbunge kupitia CCM (mwaka 2000 – 2005) hakufanya kazi kama ambavyo wananchi walitegemea na ndiyo maana hata CCM wenyewe wakamtosa kwenye taratibu za ndani ya chama chao.
Baadhi ananchi wa Mbinga Mashariki ambao nimewasiliana nao, wanasema kwamba mbunge wao amebadilika sana tangu apewe uongozi kwa mara ya pili mwaka 2010 na nilipowauliza ikiwa watamchagua tena, walianza kunitajia amajina ya makada mbalimbali wa chama hicho ambao wameonesha nia ya kusaka ubunge wa jimbo hili.
Hali hiyo inamaanisha kuwa Gaudence Kayombo anaweza kuangushwa kirahisi mno mwaka huu ndani ya kura za maoni za CCM. Hadi sasa, pamoja na juhudi kubwa za vyama vya upinzani kuongeza ushawishi kwa wananchi na kupata ushindi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na kuwa na wagombea ubunge wazuri ambao hawajachujwa, naona sehemu kubwa ya wananchi inaongelea sana ushindani ndani ya CCM kuliko nje ya CCM.
Dalili hizo zinaweza kutufanya tuamini kuwa huwenda vyama vya upinzani vinaweza kukosa jambo kubwa la kujivunia kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu katika jimbo hili. CCM bado iko imara sana Mbinga na kutahitajika miujiza ya upinzani kulitwaa jimbo hili kwa mipango ya muda mfupi kabla ya upigaji kura unaotarajiwa kufanywa miezi michache kutoka sasa.
Hitimisho
Jumatano ya wiki ijayo (Tarehe 27 Mei) tutamalizia mkoa huu kwa kuchambua majimbo ya Songea na Namtumbo na kisha, Jumamosi (Tarehe 30 Mei) tutahamia mkoa wa Mwanza na kuanza uchambuzi wa majimbo ya Nyamagana, Magu na Misungwi.
(Julius Mtatiro ni kiongozi mzoefu katika siasa. Ana shahada ya Uzamili ya Utawala na Uongozi (M.A), na ni mwanafunzi wa fani ya sheria (L LB): +255787536759, kuelekeamajimboni@yahoo.com – Uchambuzi huu ni maoni binafsi ya mwandishi).
Chanzo:Mwananchi

Waziri Nyalandu akagua meno ya Tembo yaliyokamatwa na askari wanyamapori wilayani Namtumbo

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

IMG-20150508-WA0025
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Lazaro Nyalandu na Ofisa Wanyamapori akikagua ngozi za wanyamapori zilizokamatwa  na askari wa wanyamapori toka kwa majangili Likuyu  Sekamaganga Namtumbo mkoani Ruvuma mwishoni mwa wiki iliyopita. 
IMG-20150508-WA0027
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Lazaro Nyalandu na Ofisa Wanyamapori akikagua meno ya tembo yaliyokamtwa na askari wa wanyamapori toka kwa majangili Likuyu  Sekamaganga Namtumbo mkoani Ruvuma mwishoni mwa wiki iliyopita.
IMG-20150508-WA0007
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Lazaro Nyalandu akila chakula cha mchana na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Selous iliyopo Likuyu  wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma mwishoni mwa wiki iliyopita.
IMG-20150508-WA0008
 
 
 
 

UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE SONGEA MKOANI RUVUMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akiwasha Mwenge wa uhuru leo mjini Songea katika Uwanja wa Majimaji ikiwa ni sehemu ya sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2015
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihotubia leo mjini Songea wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa uhuru zilizofanyika kitaifa mkoani Ruvuma.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein (kushoto)akimkabidhi  Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa Juma Khatibu Chum (kulia)  Mwenge wa uhuru leo mjini Songea baada ya uzinduzi wa mbio hizo Kitaifa mkoani Ruvuma.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge kwa mwaka 2015 Juma Khatibu Chum(kushoto) akimkabidhi  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu(kulia)  Mwenge wa uhuru leo mjini Songea baada ya uzinduzi wa mbio hizo Kitaifa mkoani Ruvuma.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu(kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Songea Profesa Norman Sigalla King(kulia) Mwenge wa Uhuru uhuru kwa ajili ya kuanza mbio wilayani humo baada ya uzinduzi ulifanywa leo mjini Songea  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akihotubia leo mjini Songea.
Wananchi wa Mji wa Songea na Vijiji jirani na Mjihuo wakiwa katika uwanja wa Majimaji Mkoa wa Ruvuma kushuhudia uzinduzi wa mbio za  Mwenge wa Uhuru Kitaifa uliowashwa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
Maafisa mbali mbali wakiwa katika uzinduzi wa Mbio za mwenge kitaifa uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika Uwanja wa  Majimaji Songea Mkoa wa Ruvuma

NAIBU WAZIRI WA MAJI MH AMOS MAKALLA AZINDUA MRADI MKUBWA WA MAJI KIJIJI CHA MKONGO NAKAWALE


Naibu Waziri wa Maji Mh. Amos Makalla akisalimiana na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Bi. Agnes Hokororo.


Naibu Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla amefanya ziara ya kikazi wilaya ya Namtumbo pamoja na mambo mengine amezindua mradi mkubwa Maji kijiji cha Mkongo Nakawale ambao watu zaidi ya 4000 wanapata Maji safi.

Aidha amekagua mradi wa Maji Milonji na ametoa agizo hadi kufikia tarehe 12 mei mwaka huu mkandarasi awe amekamilisha kuchimba kisima kingine baada kisima cha awali kuwa na Maji machache.


Pia Mh Makalla amemwagiza Katibu mkuu wizara ya Maji kuunda kikosi kazi cha watalaam kwenda Namtumbo kufuatilia matumizi ya Fedha kwa miradi ya Maji wilaya ya Namtumbo.
Naibu Waziri wa Maji Mh. Amos Makalla akisalimia watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mara baada ya kuwasili Namtumbo kukagua na kuzindua miradi ya maji wilayani Namtumbo. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya Bi. Agnes Hokororo.
Naibu waziri wa Maji Mh. Amos Makalla akifungua maji katika moja ya vituo vya kuchotea maji bara baada ya uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Nakawale kilichopo Namtumbo mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Maji Mh. Amos Makalla akiwa na Mbunge wa Namtumbo Mh. Vitta Kawawa wakiashiria kuzinduliwa kwa mradi wa maji wa kijiji cha Nakawale.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

KAMPUNI ZISIZOSAJILIWA SOKO LA HISA KUBANWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SERIKALI imesema katika siku zijazo haitoruhusu kampuni yoyote isiyosajiliwa katika Soko la Hisa kutolipa kodi na hata kutiliwa shaka kwamba shughuli zifanywazo haziko katika hali ya uwazi.
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema hayo Dar es Salaam na kuongeza kuwa ni vyema wamiliki wa kampuni mbalimbali nchini wakajiandaa kisaikolojia na kuhakikisha kampuni zao zinaandikishwa katika Soko la Hisa ili kuwezesha jamii kutambua kazi wazifanyazo kuwa ni za uwazi na zenye manufaa kwao.
“Kampuni mbalimbali…mtengeneze utaratibu wa kuingia katika Soko la Hisa Tanzania ili kuwezesha wananchi kiuchumi na pia kuondoa dhana kuwa mnaendesha shughuli zenu kwa usiri mkubwa,” alisema Nchemba.
Alisema Taifa linakokwenda si tu halitoruhusu kampuni kutolipa kodi bali hata kutiliwa shaka kwamba zinafanya shughuli zisizokuwa na uwazi. “Ni bora shughuli zenu mnazofanya ziweze kuungwa mkono na Watanzania wote.”
chanzo:Habari Leo
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa