
Na Regina Ndumbaro - Ruvuma Diwani wa Kata ya Misufini B, Manispaa ya Songea Mjini, mkoani Ruvuma, Christopher Fabian Kayombo leo tarehe 8 Januari, 2025 amekabidhi madawati 135 kwa Shule ya Msingi Misufini ili kuboresha mazingira ya kujifunzia wanafunzi. Tukio hilo limefanyika kwa ushirikiano wa karibu na Mratibu wa Kata, Ndugu Adolf Challe, ambapo madawati hayo yamekabidhiwa rasmi kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Ndugu Credo Komba, pamoja na Mtendaji wa Mtaa, Bi Agnes Ndunguru.Diwani Kayombo amesema kuwa wanaishukuru serikali ya mama samia kwa na mkurugenz wa Manispaa Ya songea kwa kuwapa kiasi cha fedha shilingi milioni 25...