Dondoo za yanayojiri Bungeni Dodoma leo Ijumaa Trh 25 Aprili 2014

Jana akiahirisha bunge, makamu mwenyekiti aliwakumbusha  wajumbe kuwa wasome karatasi walizogawiwa kwa kuwa leo watafanya maamuzi magumu ya kubadili kanuni, ni kanuni zile zinazopigiwa upawa na ukawa, huenda kanuni ya theluthi mbili ili wapitishe katiba yao kilaini.

---------------------

Manda

Anawasilisha azimio la kufanya marekebisho ya kanuni kutoka na vifungu vya 56 na 57 ya kanuni za bunge maalum.

-kanuni ya 32,33,35,41,60, 62 na kanuni ya 82.
-yatasomwa iwe yatawasilishwa.
-Msingi wa kufanya marekebisho ni kuweka utaratibu mzuri kwa wajumbe kupeleka majedwali katika kamati zao badala ya kwenye bunge
. inapendekezwa kufutwa kwa utalratibu wa awali wa kuleta mapendekezo bungeni.
. kurekebisha ili maoni ya wachache wasome wenyewe.

Suzan Marwa anasema;
tumekuja kutunga katiba ya wananchi sio ya chama. Kitu ambacho kinafanya watu tushindwe kuelewana ni muundo wa serikali. Hii ndo imefanya watu hadi watoe maneno machafu.

Haya maneno ya wananchi watu wanasema sio sahihi. Mi napendekeza turudi kwa wananchi tuwahoji wananchi tena kwa hivi vifungu kama wanataka serikali mbili au tatu. Haya tunayo yafanya sio wananchi wanayotegemea.

Miaka 50 ya uhuru wananchi wanalala chini hawana madawa wala huduma. Wananchi wanataka katiba itakayo watua mzigo huu.

Miaka hamsini ijayo inaweza kuwa si mizuri sababu ya uchu wa madaraka.
Mimi siwezi kuikashifu rasimu ya walioba kwa sababu tumeweza kujua kero za wananchi ambapo tunaweza kukaa chini na kufanyia marekebisho tukapata katiba njema. Hasira hukaa kifuani kwa wapumbavu. Kitu kizuri kule na ndugu yako, ndugu yako ni wananchi walio njee. Leo tupo katika uongozi kesho hatupo kwenye uongozi watoto wetu watarothi nini?

Nawasihi wajumbe tutumie malidhiano ndipo tutafika mwisho. Haya marumbano tunayo yafanya hayawasaidii wananchi.

Isack Cheyo anasema:
Tujielekeze katika kutunga Katiba sio kejeli na maneno. Wangetuletea katiba yenye serikali moja, mbili, tatu ili tuchague tofauti na hizi walosema serikali tatu tu.

Sijafurahia wanao mkejeli Mh. Warioba. Inanisikitisha sana sababu tangu tuanze kujadili muundo watu wamekua wakijiita wazanzibar baadala ya watanzania na hii ni kwasababu hiki kitu kinachoitwa Tanzania Zanzibar. Watu wa visiwani wapo makini sana na haya mambo sabau ya udogo wao na uchache wao. Utasikia sisi wazanzibar tunataka nini tena? tumepewa oic, bendera.' Haya mambo sio mazuri. Tungeanza na utanzania kwanza kuliko huu uzanzibar kama mwl. alivo iacha. Mwalimu aliacha taifa moja yenye serikali mbili. lakini leo hii tuna serikali mbili na mataifa mawili.

Nakubaliana na kiswahili iwe lugha ya taifa lakini tusibeze kingeleza ambayo ni kiswahili cha ulimwengu. Haya matusi ya kiswahili tunayosema humu tunawafunza wanetu. Sikukuu ya 12 dec ni sikukuu ya Tanganyika. tukubali hiyo kuna kosa gani kuitaja tanganyika?
Siku moja Tanganyika itakuwepo na Itakuwepo kwa hadhi yake ile ile. Asanteni sana


Usi Sumali anasema;

watu wanazungumza swala la zanzibar wamekiuka katiba na uwezo wa rais wa zanzibar.

Baraza la mitihani kuna tatizo la uwazi.

Mfuko wa elimu ya juu nawapongeza. lakini tatizo lililopo ni la uwiano katika scholarship, kulipa kodi mara mbili, haya matatizo yaangaliwe.
Swala la rais wa zanzibar kuondolewa kwenye makamu wa rais wa Tanzania. Kwenye ajira uwiano sio mzuri hivi viangaliwe upua

Yusuph Omar Chunda anasema;

Swala la Muungano huu tusiuchezee kwani una historia kubwa. Mimi mnina asili ya bara lakini nimezaliwa zanzibar na baba yangu amezaliwa zanzibar. siwezi kukuelewa ukiniambia muungano uteteleke.

Tumshukuru Nyerere na Karume waliotuunganisha. Watu 14 walioleta mapinduzi tuwashukuru pia, ndg said abdallah natepe, hamis duruheshi mhamed kauole hamisi ndui abdala mfalanyaki washoto mokero pili sulemani amir haji, saidi seif bakari omar ndo waliosababisha kuikomboa zanzibar. Nazani hata kesho wanaweza kumbukwa pia.

Changamoto za muungano zipo na zinafaa zishughulikiwe. Rais wa zanzibar achukue nafasi yake.

Lugha ya kiswahili kimetusaidia kutuunganisha na kuleta amani zaidi.

Natoa ombi kwamba vyombov ya habari tbc na zcb Upande wa radio.

Anna Abdallah anasema:

Nlikua mwenyekiti wa kamati namba kumi. nlipewa mapendekezo
1. Tanzania si shirikisho ni jamhuri ya muungano wa Tanzania
2.Vyombo vya shirikisho tulipendekeza viwe vya Muungano.

Wenzetu hawana uvumilivu wa kusikia maneno ya wenzao. Hili ndio tatizo kubewa sana. sisi tulioko humu ndani ndio tunaotunga katiba ya Watanzania.

Mambo mengine lazima kuvumiliana. Kila mtu ana uhuru wa kuonge yaliyo yakwake. Lakini la kuwakashifu wasisi hilo halisameheki na halikubaliki. Kuwatukana wasisi ni sawa na kuwatukana wazazi wako. mtu wa hivyo inabidi apimwe akili.

Zamani hatukujua huyu ametoka zanzibar au bara hata huko wenzetuhawajui, wanajua sisi ni Watanzania. Mimi ni Muumini wa serikali mbili

Kingunge.

Nawashukuru sana waganga wa tiba asili kwa kunifanya nije hapa. Mimi nlikua mlezi wa chama hiki tangu 1998. Waliokua wanahoji walitaka watu waseme kwamba nimepenyapenya lakini mimi nimependekezwa na hiki chama. Ni chama cha heshima kwani kinatoa dawa za miti shamba sio ramli.

Haya mambo mliokua mnafanya ya kuzomea si sawasawa. kuna lugha zimetumika hazifanani na sisi wala Watanzania. Lugha za ugomvi na kudhalilisha.
Lugha za kudhalilisha wasisi wetu eti mwalimu Nyerere si Mungu je nani alikuambia ni Mungu?

Watu tumewasomesha . Swala kubwa la msomi ni unyenyekevu. Hapa tunapishana kwa mawazo tu. Hata rasimu hii ina mawazo tu, hakuna watu mle ndani ya rasimu. Hapa hatuwazungumzi wajumbe wa timu, Warioba bali tunazungumzia haya mawazo yaliyo katika rasimu. Tuache kumshambulia Walioba. Chama changu CCM kina adabu sasa wewe unamshambulia walioba unafedhehesha chama changu.

Mazungumzo tuliyo yafanya sura ya 1 na 6 tumefanya vizuri sababu maoni ya walio wengi na wachache yamejitokeza. Lakini kazi ya kufanya maamuzi bado.

Maoni yangu mimi; Sisi hapa tumetumwa na wananchi ili ipatikane katiba mpya iliyo bora sio ilimradi katiba.
Inabidi kwanza ijue katika miaka hii 50 tuna mafanikio makubwa kwa hiyo katiba bora lazima izingatie yale mazuli mfano Muungano wetu, Haya yote mafanikio yametokana na Muundo wa namna wake wa Serikali mbili.

Tunataka katiba itakayo punguza au kuondoa kero za Muungano, kama tutashindwa kuondoa hayo mapungufu itakua sio katiba bora. Naamini tutatumia kipindi hiki cha kupumzika kutafakari hili.

Tumeishi duniani na tumejifunza mambo. Katiba mpya lazima ilete mambo ya msingi na kuondoa hili kero la Umasikini uliokithili wa Nchi yetu. Mtaandika katiba lakini kama mtashindwa zungumzia Umasikini itakua sio katiba bora, Katiba mpya lazima izungumzie uchumi wa watanzania walio wengi.

Kupata katiba Mpya lazima kuwepo na maelewano humu ndani. Waliotoka nje walionyesha mapungufu makubwa lakini tunaomba warudi na wakirudi naomba tuelewane. Kupata theruthi mbili ya bara na zanzibar ni sheria.

Kule zanzibar kulilkuwepo na tatizo tangu mwaka 1998 limedumu kwa miaka 18 kila siku tunazungumza baadae tukaelewana tukazungumzi na Hamad rashid Nahodha mimi mwisho wa siku tukapata fomula maalim Seif sasa hivi ni Makamu Rais wa kwanza ni kutokana na Mazungumzo.

Sasa tunzungumze mpaka tuelewane na wakubwa nao inabidi wazungumze.Asante kwa kunivumilia may 30 ntafikisha miaka 82 si haba. asanteni sana

Kificho anasema:

Mimi nimeshangaa sana watu wanaosema eti mimi naunga mkono serikali tatu, Tangu lini?
Mimi nasema naunga mkono serikali mbili ambazo zimedumisha Huu muungano wetu kwa miaka 50.

Balozi Seif Idd (makamu wa pili wa rais zanzibar) anasema ;

Mimi naungana na walio wengi kwamba muungano wetu huu uwe wa walio serikali mbili. Wananchi wametuleta humu ili tuwapelekee katiba itakayokua kwa masirahi yao. Tumetumia gharama kubwa kutengeneza ukumbi huu ili tukae tustarehe lakini wenzetu wakaamua kutoka nje. Nawaomba warudi sababu katiba haitungwi Barabarani wala popote pale isipokua humu ndani tu.

Humu ndani kila mmoja nalipwa sh laki tatu kila siku tunayo kaa humu. kwa siku70 tulizopangiwa tumetumia bil 20 mpaka sasa. ndizo tulikua tutumie mpaka leo hii. pesa nyingi zimetumika katika kutunga kanuni baada ya hapo kujadili siri au wazi. watu wakang'ang'ana sana kura ya siri. Lakini wale wale waliotaka kura za siri wakapiga wazi. uharibifu wa fedha.

sura ya kwanza na ya sita tu ndo zimetumia bil 20. Leo tunaahilisha mpaka tarehe 5/8. Rais alikubali kuongeza siku 60 sasa tuangalie siku 60 tutatumia kiasi gani. Nia yetu humu ndani ya kutunga katiba. Watu wameshindwa kutunga katiba wameanza mwalimu nyerer karume na kombo wakati hawawezi kuwajibu.

Mimi naomba wenzetu warudi waje tujadili katiba mpya ambayo wananchi wametutuma. Kero hizi za Muungano zinaweza kutekelezeka kwa muundo huu wa Muungano tulionao.

Nawasihi wenzetu walio toka warudi. asanteni.

Peter Pinda anasema;
Mimi nilikua kamati namba moja. Nlikua nasikiliza mjadala huu kwa makini sana. tanzania ni miongoni mwa Nchi barani afarika ambayo tumeweza kuwa wamoja kutokana na muungano wetu ulio asisiwa na wasisi wetu. Mijadala iliyopita ilikua na vijembe na kejeli. Naishukuru kamati yako ya kanuni kwa kuendelea kuboresha kanuni hizi. Tunapokwenda tutajipanga vizuri zaidi.

Muungano wa Zanzibar na Tanganika umeelezwa na kuandikwa sana lakini ni vizuri tuendelee kuyaheshimu mawazo ya waasisi wetu wa Muungano.

Watu wanajaribu kulilia kitu ambacho hawajaexperience hata kidogo, nashangaa sana. Tanganyika imedumu mwaka mmoja na nusu lakini miaka 50 tupoTanzania. Tunaitaka Tanganyika Tanganyika ipi hyo?.

Mwalimu si mtu ambaye unaweza kumbeza kwa kiasi hicho kwani anaheshimika dunia nzima. Leo mtu anasimama kijana wa juzi anatumia lugha chafu kwa baba huyu! jamani.

Nikweli kero za muungano zipo. kweli muungano ulikua na kero 31 leo zimebaki 6. Ibara ya109 katika rasimu hii wameunda tume ya kushughulikia kero za Muungano. Nawashukuru sana tume ya Warioba kwa hili.

Yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Hawa wenzetu waliotoka nawaomba kwa dhati kabisa warudi. Katiba yoyote kazi kubwa inayofanyika ni ya ujenzi wa katiba. Tuliwambia tuboreshe hii wakakataa eti wanataka mpya, mpya kwani ndo tunapata uhuru? sasa kipi kipya kilichoingia kwenye hii?. Siafiki hata kidogo kwamba tume imetumia fedha nyingi kwa hiyo inabidi iletwe ya serikali tatu,

Watu wametazama takwimu wamehoji.

wakati wa kuwasilisha wrasimu ya katiba limerudia sana kwamba ofisi ya waziri mkuu imependekeza serikali tatu. Mimi sikua ndani yake bali mimi nlitoa maoni yangu kama mimi. Na hii ya kutumia ofisi hizi mbili kupendekeza serikali tatu kwamba wananchi ndo wamependekeza hivyo sio sahihi hata kidogo.

Nawashukuru tume kwa kufanya kazi nzuri. Asanteni sana.

Samwel Sitta
 anasema;

Maoni ya mapendekezo tuliyo yatoa sasa tunayakabidhi kwa katibu ili wapewe kamati ya waandishi. leo saa kumi jioni Rais atatoa Hotuba katika ukumbi wa TPA sabasaba kuhusu mambo ya Muungano.

Wajumbe wanahojiwa kama wanaafiki wote wamesema ndio.

-Kiti kimetuhumia hatukuweza kudhibiti matusi. kanuni hazikusema hivyo bali ni kuwaondoa nje ikibidi kwa nguvu. tulisita kwa kuwe kungetokea ugomvi.
-Nilifanya ziara kwa viongozi wa dini bado sijamaliza. ntatembelea makundi mbalimbali. Wale wenzetu ambao hawapo hapa labda tuliwakasirisha basi ntafanya jitihada kupitia vyama vya siasa ili tukirudi turudi nao.
Anasoma dua ya kushukuru na kumaliza.


Bunge limeahirishwa hadi tarehe 05 .08 . 2014 siku ya Jumanne saa tatu asubuhi.


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


























CHANGAMOTO ZA USAFIRI RUVUMA ZA PUNGUA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wameisifu SUMATRA kwa kuweza kusimamia safari za Mabasi na kufanikisha kupanga safari katika sehemu ambazo zilikuwa ni kero kwa Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.
                       
Mohamed Chichi akizungumza kwa niaba ya Wasafiri katika Kituo Kikuu cha Mabasi Songea, amesema katika Changamoto zilizokuwa zinawakabili Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma ni kukosa Usafiri wa Songea – Dodoma, Songea – Mwanza na Songea – Mbamba Bay. Njia zote hizo zimefunguka tunaishukuru Serikali kwa kuweza kutatua changamoto hizo.

Afisa Mfawidhi wa SUMATRA Mkoa wa Ruvuma Denis Daudi amesema Mkoa wa Ruvuma una changamoto nyingi za usafiri, Ukiwemo usafiri wa Songea – Mkenda –njia inayo unganisha na Nchi ya  Msumbiji na Tanzania ,na Songea  Tunduru bado kunahitajika Usafiri wa uhakika,

Barabara ya Songea – Mkenda serekali ina fanya mipango ya kumpata mfadhili ili atengeneze njia hiyo  kwa kiwango cha Lami itaweza kufungua mawasiliano kati ya Msumbiji na Tanzania. Amewataka  wananchi kuwa watulivu wakati juhudi za serekali zikitafuta njia ya kutatua changamoto hizo
 

PICHA ZA MAZISHI YA MWANDISHI WA HABARI "THOMAS LIPUKA KOMBA"ALIYEZIKWA KIJIJINI KWAO MKILI WILAYANI NYASA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakiwa mbele ya sanduku Marehemu Lipuka komba
Baadhi ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Ruvuma wakishusha sanduku kaburini
Katibu mtendaji wa Ruvuma Press akichukuwa matukio
Mjane wa marehemu Christina Haule akiweka shada la maua

Mwandishi wa habari Thomas Lipuka Komba amezikwa kijijini kwake Mkili wilayani Nyasa Juzi.
 
Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu hali iliyosababisha kifo cha ghafla.
Marehemu Thomas Lipuka Komba ni miongoni mwa waanzilishi wa chama cha waandishi wa habari Ruvuma RPC mwaka 1995 alikuwa mwanachama mwaminifu hadi kifo chake.

Tunawashukuru wale wote walotuombea tusafiri salama tunapenda kuwajulisha kwamba tumeludi salama.Picha na Mpenda Mvula

Wafanyabiashara Songea walazimishwa kugoma

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Baadhi ya wafanyabiashara wa mjini Songea wamelazimishwa na wenzao kuingia katika mgomo wa kupinga matumizi ya mashine za kielektroniki za kutolea risiti za EFD.
Waliolazimishwa ni wamiliki wa baa na vituo vya kuuza mafuta ambao wamekuwa wakiendelea kufanya biashara zao kabla ya baadhi ya wenzao kukodisha ‘mabaunsa’ kuwalazimisha kufunga biashara zao kwa kile kilichoelezwa kuwa ni wasaliti.
Pamoja na serikali mkoani Ruvuma kutumia polisi kufanya doria katika maeneo mbalimbali ya mji mgomo huo umeendelea huku wahusika wakishinikiza Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Ruvuma, Apily Mbaruku afukuzwe kazi au ache kuwaandikia barua za vitisho za kutumia mashine hizo.
Akizungumzia shinikizo hilo, Mbaruku alisema hatishwi na wafanyabiashara hao na kusema kuwa TRA inawataka wafanyabiashara kuendelea kutumia mashine hizo.
Akizungumza wakati wa kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Bombambili jana, msemaji wa wafanyabiashara hao, John Oscar alisema wamechoka kuburuzwa na TRA na safari hii mgomo walioitisha ni mkubwa ukihusisha wafanyabiashara wa kada mbalimbali.
Alidai kuwa mashine hizo ni mpango wa wakubwa ambao wanataka kupata fedha kupitia wao na kumtaka meneja wa TRA wa mkoa kuacha tabia ya kuwakejeli kuwa hawana uwezo wa kufunga maduka kwa wiki moja.
Akisoma maazimio ya mkutano huo, makamu mwenyekiti wa umoja wa wafanyabiashara hao, Wilson Mbilinyi alisema hawatafungua maduka yao kwa siku mbili na baada ya hapo wataandamana kwenda ofisi za TRA kwa ajili ya kuzifunga kutokana na kushindwa kusikiliza matatizo yao.

Meja Jenerali Msemwa kuzikwa leo

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399
<p>MWILI  wa  aliyekuwa  Meja Jenerali  wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),  Kevin Msemwa, umewasili  mjini Songea  na  kupokewa na viongozi mbalimbali wa  serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu.</p> <p>   Mwili  huo uliwasili  jana, saa 4 asubuhi kwa ndege ya jeshi   hilo  katika Uwanja wa Ndege wa  Ruhuwiko  wa mjini Songea na kuelekea  nyumbani kwa marehemu maeneo ya Seed Farm   mjini humo.</p> <p>   Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili kwa  mwili huo, Luteni Jenerali na Mnadhimu wa Jeshi, Samweli Ndomba, alisema  marehemu Msemwa anatarajiwa kuzikwa leo saa 8 mchana katika makaburi ya  Mfaranyaki mjini Songea.</p> <p>   Msemaji wa familia, Nicas Msemwa, alisema kuwa Kevin  alifariki dunia Aprili 3, mwaka huu alipokuwa akipatiwa matibabu katika  Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, Dar es Salaam.</p> <p>   Nicas ambaye ni mdogo wa marehemu, alisema misa ya mazishi  itafanyika katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba,  mjini Songea.</p>MWILI  wa aliyekuwa  Meja Jenerali  wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kevin Msemwa, umewasili  mjini Songea na  kupokewa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu.
Mwili  huo uliwasili jana, saa 4 asubuhi kwa ndege ya jeshi  hilo  katika Uwanja wa Ndege wa Ruhuwiko  wa mjini Songea na kuelekea nyumbani kwa marehemu maeneo ya Seed Farm  mjini humo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili kwa mwili huo, Luteni Jenerali na Mnadhimu wa Jeshi, Samweli Ndomba, alisema marehemu Msemwa anatarajiwa kuzikwa leo saa 8 mchana katika makaburi ya Mfaranyaki mjini Songea.
Msemaji wa familia, Nicas Msemwa, alisema kuwa Kevin alifariki dunia Aprili 3, mwaka huu alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, Dar es Salaam.
Nicas ambaye ni mdogo wa marehemu, alisema misa ya mazishi itafanyika katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba, mjini Songea.
 Chanzo;Tanzania Daima

WAZABUNI SONGEA WAKUMBUSHIA DENI LAO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAZABUNI wa vyakula katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea, wameikumbusha serikali kuangalia uwezekano wa kuwalipa deni lao la zaidi ya sh bilioni moja lililotokana na kulisha katika shule za sekondari, vyuo na taasisi mbalimbali mkoani hapa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Tanzania Daima jana, wazabuni hao ambao hawakutaka kutajwa majina, walisema pamoja na ahadi nyingi za viongozi wa kitaifa kutolewa juu ya kulipa madeni hayo, lakini hadi sasa hakuna  utekelezaji.
Walisema mbali ya Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenista Mhagama, kuwaahidi waendelee na kazi  ya kulisha katika shule na vyuo wakati malipo yao yakishughulikiwa, jambo hilo hadi sasa limekuwa hadithi.
Walisema wamekuwa wakiendesha shughuli ya kulisha kutokana na mikopo inayotolewa kwenye taasisi za fedha, jambo ambalo wamedai hivi sasa limewaweka mahali pabaya kutokana na taasisi hizo kutaka kuuza mali zao kutokana na kuchelewesha marejesho.
Walisema endapo serikali haitaharakisha malipo hayo, watashindwa kuendelea kulisha katika shule hizo, kwani fedha iliyotumwa kwenye baadhi ya shule za sekondari na vyuo kiasi cha sh milioni 72 hazitoshi kwa kugawana wazabuni wote kwani zinatosha kulisha kwa siku 40 tu.
Chanzo:Tanzania Daima 

MWAMBUNGU AMPONGEZA MKANDARASI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu, amepongeza mradi wa ujenzi wa majengo ya Shule ya Sekondari Unberkant iliyopo kwenye Kata ya Mtipwili wilayani Nyasa mkoani hapa unaofanywa na Kampuni ya Ovans Construction (Ltd) ya Mbinga.
Mradi huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia (WB) kupitia Serikali ya Tanzania kwa thamani ya sh 288,254,380.
Mwambungu alitoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki baada ya kutembelea shuleni hapo kwa lengo la kujionea maendeleo ya ujenzi alipofanya ziara wilayani Nyasa.
Alisema mkandarasi anayesimamia mradi huo anastahili pongezi kwa kuonyesha uzalendo na uaminifu katika ujenzi huo wa kiwango kinachotakiwa ambapo amewataka wengine kuiga mfano huo kwa madai kwamba hali hiyo itasaidia kuokoa fedha nyingi za serikali ambazo zinapotea kutokana na baadhi yao kujenga miradi chini ya kiwango.
Kutokana na hali hiyo mkuu wa mkoa huyo amezitaka halmashauri zote mkoani hapa kuhakikisha zinatoa kazi za ujenzi kwa makandarasi wazalendo, huku akionya matendo ya rushwa kwa madai kwamba kufanya hivyo kunasababisha kupata makandarasi wabovu.
Kwa upande wake, mkuu wa shule hiyo ya sekondari, David Kilowoko, akisoma taarifa ya shule yake mbele ya mkuu wa mkoa huyo, alisema mradi huo wa ujenzi wa nyumba moja ya mwalimu, maabara moja, matundu nane ya vyoo vya wanafunzi, mfumo wa uwekaji wa umeme wa jua na mfumo wa maji ya kisima na ukarabati wa vyumba sita vya madarasa umefanikiwa kupitia mpango wa matokeo makubwa sasa unaotekelezwa katika sekta ya elimu.
Kilowoko alisema kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari wa awamu  ya pili (SEDP II), shule hiyo pia imepata kiasi cha shilingi milioni 26 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba moja ya mwalimu ambayo itatumiwa na familia za walimu wawili.
Akizungumzia kwa upande wa taaluma, alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa walimu wa masomo ya sayansi ambapo hadi sasa shule hiyo ina mwalimu mmoja tu wa somo hilo na kudai kwamba hali hiyo imesababisha kupata matokeo yasiyoridhisha ambayo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na upungufu wa walimu.
Aidha mkuu huyo wa shule ameishukuru serikali kwa jitihada zake za kuboresha miundombinu ya shule jambo ambalo amedai kuwa hali hiyo itakuwa chachu ya maendeleo ya elimu kutokana na kuwa mazingira ya kusomea na kufundishia yatakuwa rafiki.
Chanzo;anzania Daima
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa