WATAALAMU KUTOKA WIZARA YA NISHATI NA MADINI WAENDELEA KUWAPIGA MSASA WACHIMBAJI WADOGO JUU YA UCHIMBAJI BORA WA MADINI HUKO TUNDURU, RUVUMA


Kamishna Msaidizi- Uendelezaji wa Uchimbaji Mdogo, Mhandisi Fredy Mahobe kutoka Wizara ya Nishati na Madini akifafanua taratibu za kupata mikopo kwa wachimbaji wadogo.
Mhandisi Heri Issa kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) akionesha jinsi uchekechaji wa madini unavyofanyika, katika mafunzo ya wachimbaji wadogo yanayoendelea huko Tunduru mkoani Ruvuma.
Mjiolojia Mwandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini Bw. Julius Sarota akielezea matumizi ya zebaki kwenye uchenjuaji wa madini katika mafunzo ya wachimbaji wadogo yanayoendelea huko Tunduru mkoani Ruvuma.
Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini ( waliokaa mbele) ikiwa ni pamoja na washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa. 
Picha na Michuzi Media

PSPF YAZINDUA MPANGO MPYA WA UUZAJI NYUMBA KWA BEI NAFUU, SOMA HAPA KUJUA BEI ZAKE




Mfuko wa Pensheni wa PSPF unapenda kuutaarifu Umma kuwa umezindua Mpango Mpya wa uuzaji nyumba zake zilizojengwa kwa ajili ya makazi katika mikoa ya Dar es Salaam- Ilala (Buyuni), Morogoro (Lukobe), Tabora (Usule), Mtwara (Mang’amba), Shinyanga (Ibadakuli) na Iringa (Mawelewele).
Bei za nyumba ni kati ya sh. 52,000,000.00 hadi sh. 71,000,000.00 (bila VAT). Bei hizi ni kulingana na ukubwa wa nyumba na mkoa nyumba ilipo.   Ukubwa wa nyumba ni kuanzia vyumba viwili hadi vinne.
Chini ya utaratibu huu mpya unaoanza kutumika kuanzia Februari 2014; Muombaji atapaswa kuainisha kwenye fomu ya maombi aina ya nyumba anayohitaji na Mkoa ilipo.  Malipo yanaweza kufanyika kwa njia zifuatazo:
1)                           UNUNUZI KAMA MPANGAJI (HIRE PURCHASE):
Mnunuzi atalipia kwa mpango wa mwezi mmoja mmoja au miezi mitatu kwa mkupuo (installments) kulingana na thamani ya nyumba. Katika mpango huu, mnunuzi anaweza kulipia kutokana na vyanzo vingine vya mapato yake mbali na mshahara wake. Mwanachama wa PSPF aliyechangia chini ya  miaka mitano (5) atatakiwa kulipia kiasi cha sh. 5,000,000.00 kama malipo ya mwanzo ya nyumba na asiye mwanachama wa PSPF atatakiwa kulipia kiasi cha sh. 10,000,000.00 kama malipo ya mwanzo ya nyumba kukidhi vigezo vya kununua nyumba (kama mpangaji).

Mpango huu wa Ununuzi kama Mpangaji (Hire Purchase) utamwezesha mnunuzi kulipa kati ya sh. 450, 000.00 (laki nne na hamsini tu) na
sh. 813,000.00 (laki nane na kumi na tatu tu) kwa mwezi kama malipo ya nyumba zinazouzwa na Mfuko kulingana na ukubwa na eneo nyumba ilipo.

2)                           MALIPO YA MARA MOJA (OUTRIGHT PURCHASE)
Mnunuzi atalipia gharama ya kununua nyumba kupitia akaunti ya Mfuko na kisha kusaini makubaliano kabla ya kuhamishiwa umiliki (transfer).

3)                           MKOPO WA NYUMBA KUPITIA BENKI (MORTGAGE BASIS):
Mnunuzi anaweza kuchukua mkopo katika mojawapo ya Benki ambazo Mfuko wa PSPF ina mikataba nazo na kutumia mkopo huo kununulia nyumba. Mabenki hayo ni; CRDB, Azania, Exim na NMB. 
MUHIMU! Iwapo utanunua nyumba kupitia mkopo wa benki (Mortgage) utapaswa kuwa umesajiliwa kwenye Mfuko na kuchangia kwa muda wa miaka mitano au zaidi. Muda wa kurejesha mkopo ni mpaka miaka ishirini na mitano (25) kulingana na matakwa ya Benki husika.
Mwombaji anayehitaji kuona au kukagua nyumba awasiliane nasi kupitia simu: +255 22 2120912/52 au +25522 2127375-6 au E-mail: pspf@pspf-tz.org.

Kwa maelezo zaidi fika Makao Makuu ya PSPF yaliyopo jengo la Golden Jubilee Towers, Barabara ya Ohio au ofisi zetu zilizopo katika kila mkoa.

Imetolewa na

Mkurugenzi Mkuu,
Mfuko wa Pensheni wa PSPF 

Wachimbaji wadogo watakiwa kuzingatia kanuni za usalama migodini


Mtaalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mhandisi Dkt. Crispin Kinabo akiwasilisha mada juu ya utunzaji wa mazingira kwenye migodi wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika mapema leo katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma. Mafunzo hayo yalishirikisha viongozi na watendaji wa wilaya, madiwani, wakuu wa vitongoji na wachimbaji wadogo lengo lake likiwa ni kuwapa uelewa wa kanuni za uchimbaji bora wa madini.
Mmoja wa wakilishi wa wachimbaji wadogo ambaye ni mmiliki wa mgodi katika eneo la Mhesi Mapinduzi lililopo wilayani Tunduru Bi Sofia Hamdan akichangia mada wakati wa mafunzo hayo.
Mpepo Ismail ambaye ni mmoja wa wachimbaji wadogo na mmiliki wa machimbo ya shaba Mbesa akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho. Ameitaka Serikali kuangalia uwezekano wa kuwasaidia wachimbaji wadogo kwa kuwakopesha vifaa vya kuchimba madini.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinawasilishwa na watoa mada kwa nyakati tofauti (hawapo pichani).


Na Greyson Mwase, Tunduru

Wachimbaji wadogo wametakiwa kuzingatia kanuni za usalama migodini ili kuepuka majanga yanayoweza kujitokeza na kuleta athari kwa jamii kwa ujumla.

Hayo yalisemwa na Afisa Madini Mkazi Tunduru Mhandisi Frederick L. Mwanjisi alipokuwa akiwasilisha mada kwenye mafunzo yaliyoshirikisha wachimbaji wadogo, viongozi na watendaji wa wilaya, madiwani na wenyeviti wa vitongoji yanayoendelea wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.

Mhandisi Mwanjisi alisema kuwa wachimbaji wengi wamekuwa wakithamini madini kwanza badala ya mazingira kwa jamii inayowazunguka jambo linalosababisha kujitokeza kwa majanga ya mara kwa mara kama vile kuanguka kwa vifusi na kemikali kuathiri binadamu ikiwa ni pamoja na wanyama.

“ Wachimbaji wamekuwa wakitanguliza msemo usemao “madini kwanza” kwa kufikiria maslahi yao binafsi badala ya kufikiria jamii inayowazunguka kwa kuweka mazingira katika hali ya usalama yaani msemo uwe “Usalama kwanza” Alisisitiza Mhandisi Mwanjisi.


Mhandisi Mwanjisi alibainisha athari zinazosababishwa na majanga yanayotokana na kutokuzingatia usalama migodini ni pamoja na mmiliki kupoteza fedha nyingi kwa ajili ya fidia, miundombinu kuharibika, kupoteza imani kwa wafanyakazi na umma kwa ujumla hali inayoweza kupelekea hata mgodi kufungiwa.

Aliendelea kutaja athari nyingine kwa upande wa wafanyakazi kuwa ni pamoja na kupoteza nguvu kazi, ulemavu wa maisha, kuathirika kisaikolojia ikiwa ni pamoja na kukosa furaha ya maisha.

Mhandisi Mwanjisi aliongeza kuwa jukumu la usalama kwenye migodi ni la wote kuanzia wamiliki wa migodi, wafanyakazi, serikali ikiwa ni pamoja na jamii inayozunguka migodi.

Mhandisi Mwanjisi aliainisha kanuni za usalama migodini ikiwa ni pamoja na uvaaji wa vifaa vya kujikinga na mazingira hatarishi, kuweka mgawanyo wa kazi kulingana na taaluma na uzoefu wa wafanyakazi migodini, kufukia mashimo ikiwa ni pamoja na kuwekea wigo maeneo hatarishi ndani ya migodi.

Aliongeza kanuni nyingine za usalama ni pamoja na kufanya ukaguzi wa maeneo ya machimbo kabla ya kuanza kazi ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa mkaguzi wa migodi juu ya matukio ya hatari au ajali zinazotokea migodini.

Kanuni nyingine ni pamoja na kuwa na orodha ya wafanyakazi wote wa mgodi katika daftari maalumu, vifaa vya huduma ya kwanza na kutoshirikisha watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 katika kazi za machimbo.

Aidha Mhandisi Mwanjisi aliwataka wachimbaji wadogo kuwa na mpango wa usalama kwenye migodi wenye kuainisha tahadhari zinazoweza kuchukuliwa pindi majanga yanapotokea katika migodi badala ya kutokuwa na mpango wowote hali inayopelekea ugumu katika kushughulikia kwa haraka majanga yanapojitokeza.

Wakati huo huo mtaalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Idara ya Jiolojia Mhandisi Dkt. Crispin Kinabo aliongeza kuwa wachimbaji wadogo mbali na kuzingatia kanuni za usalama migodini wanatakiwa kufanya tafiti za kijiolojia kabla ya kuanza uchimbaji wa madini ikiwa ni pamoja na kusoma ramani za kijiolojia.

Dkt. Kinabo aliwataka wachimbaji wadogo kuachana na uchimbaji wa mashimo kiholela bila kusoma ramani za kijiolojia za maeneo husika hivyo kupelekea kuwa na mashimo kila mahali na hivyo kupelekea majanga ya kujitakia.

Aidha Dkt. Kinabo aliwataka wachimbaji kuzingatia kanuni za mazingira kwa kutunza vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na mpango wa kuotesha miti.

Mafunzo haya yaliandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini lengo lake likiwa ni kuwapa uelewa wa kanuni za uchimbaji bora wa madini wachimbaji wadogo ikiwa ni pamoja na viongozi na watendaji wa wilaya, madiwani, wakuu wa vitongoji na wachimbaji wadogo.
Chanzo : Michuzi Media Group

PSPF YATOA PONGEZI KWA WAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WA WIZARA YA FEDHA



MFUKO WA PENSHENI WA (PSPF)
                       
SALAMU ZA PONGEZI

Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum (MB)
 Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Mh. Adam K. Malima. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha; Mh. Mwigulu L. Nchemba.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini na wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wanatoa pongezi za dhati kwa Mhe. Saada Mkuya Salum (MB) kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Fedha.


Vile vile, PSPF inatoa pongezi kwa kuteuliwa kwao Naibu Mawaziri wapya wa Wizara ya Fedha; Mh. Mwigulu L. Nchemba (MB) na Mh. Adam K. Malima.

Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wote wamepokea kwa furaha uteuzi wenu mliopewa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. PSPF ipo tayari wakati wote kushirikiana nanyi katika kuleta tija katika utendaji wa Wizara ya Fedha na sekta nzima ya Hifadhi ya Jamii kwa ujumla hapa nchini.

PSPF - Tulizo la Wastaafu

Mkurugenzi Mkuu
Mfuko wa Pensheni - PSPF

Tunduru yapitisha bajeti YA MAENDELEO

HALMASHAURI ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma imepitisha bajeti ya zaidi sh.bilioni 40.3 kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya kawaida ikiwa ni pamoja na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa mwaka 2014/15.
Akisoma taarifa ya mapendekezo ya mpango wa bajeti ya halmashauri hiyo,Ofisa
Mipango wa halmashauri hiyo, Kenneth Haule, alisema halmashauri hiyo inatarajia kukusanya zaidi ya sh.milioni 134.7 kutoka katika vyanzo vyake vya mapato kwa ajili ya miradi ya maendeleo na matumizi ya kawaida mishahara na mengineyo sh.bilioni 25.3.
Alisema, bajeti hiyo imeongezeka kwa sh. bilioni 4.5 ambapo wanatarajia zaidi kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kuweza kuongeza mapato ya halmashauri hiyo.
Akichangia wakati wa kikao hicho Mbunge wa Jimbo la Kusini, Abdallah Mtutura, aliwataka madiwani kusimamia mapato kwani wao ndiyo wanaojua namna mapato yanavyovuja kwani wao ndiyo wanaoishi na wakusanya ushuru. Aliwataka madiwani hao wasimamie pia matumizi ya fedha walizokusanya ikiwa ni pamoja na kuacha kufanya siri bali wawafichue wanaohujumu mapato ya halmashauri hiyo

Chanzo;Majira

MIKAKATI YA TENESCO KUHUSU UMEME MKOANI RUVUMA

 Engineer Boniface Njombe akitoa Elimu kwa Wandishi wahabari jinsi Umeme unavyo fanya Kazi akiwa na wafanyakazi wa Tenesco
 Engineer Boniface Njombe akionyesha mashine zilizoko Katika Mtimbo iliyoko Kiblangoma Manspaa ya Songea
 Engineer Boniface Njombe akicheza na Watoto eneo la Magagula Songea vijijini
 Alipo ulizwa jinsi gani anajisikia kucheza na watoto Engineer alijibu kuwa hujisikia vizuri kucheza na watoto kwa kuwa hata yeye alipata malezi mazuri kutoka kwa watu tofautofauti jambo lililo mpa ujasiri alio nao hadi leo


 Changamoto zipo pale unapo taka kitu kizuri hata Asali ni Tamu lakini utengenezaji wake ni mgumu ukiwa uliza nyuki kufika Tulila Chipole ni kazi hapo  Gari la Engineer Boniface Njombe lime kwama katika mlima Magagula songea vijijini ili chukua saa moja kuli kwamua
 Jopo la walatamu wa Umeme kutoka kulia ni Engineer Boniface Njombe anaye fuatia ni Mtawa Hisani Mhagama aliye kati ni Engineer Ake Aurebekk na anaye fuata ni Mhandisi chui na wa mwisho ni msaidizi wa meneja wa Tenesco Songea
 Engineer Ake Aurebekk akionyesha jinsi bwawa la umeme litakavyo jengwa eneo la Tulila

maporomoko ya maji katika mto Tulila yanayo jengwa kwaajili ya uzalishaji Umeme

Waandishi wahabari kutoka vyombo mbambali wakipata chakula baada ya kazi kubwa ya kutembelea mporomoko ya maji katika kijiji cha Tulila  ambayo yana jengwa kwa ajili ya kufua umeme

MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA(PSPF) UNAWATAKIA WATU WOTE SIKUKUU NJEMA MAULID



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MFUKO WA PENSHENI WA PSPF






MAADHIMISHO YA SIKU YA KUZALIWA KWA MTUME MUHAMMAD (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam)
Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) wanaungana na Waisalamu na Watanzania wote katika kusheherekea siku ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam)
“PSPF TULIZO LA WASTAAFU”
Mkurugenzi Mkuu,

PSPF

SALAM ZA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUTOKA MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA(PSPF)








JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MFUKO WA PENSHENI WA PSPF





Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) wanaungana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Ali Mohamed Sheni pamoja na wananchi wote wa Tanzania katika kuadhimisha miaka hamsini ya Mapinduzi ya Zanzibar, 12 Januari 2014. 

 


Kwa Mahitaji yako ya Hifadhi ya Jamii PSPF ni chaguo lako, Jiunge sasa

“PSPF TULIZO LA WASTAAFU”

Mkurugenzi Mkuu,

PSPF

SALAM ZA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUTOKA MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA(PSPF)








JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MFUKO WA PENSHENI WA PSPF





Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) wanaungana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Ali Mohamed Sheni pamoja na wananchi wote wa Tanzania katika kuadhimisha miaka hamsini ya Mapinduzi ya Zanzibar, 12 Januari 2014. 

 


Kwa Mahitaji yako ya Hifadhi ya Jamii PSPF ni chaguo lako, Jiunge sasa

“PSPF TULIZO LA WASTAAFU”

Mkurugenzi Mkuu,

PSPF

TATIZO LA UKOSEFU WA UMEME RUVUMA KUMALIZIKA MWAKA 2015

Mkoa wa Ruvuma unatarajia kuondokana na tatizo la umeme ifikapo mwaka 2015 baada ya mradi wa umeme kutoka Luli Chipole kukamilika na kuweza kutoa MG 8 ambazo zitasaidia kusambazwa katika Wilaya ya Mbinga, Nyasa na Songea.

Naibu Mkurugenzi wa TANESCO Bonifance Njombe ameyasema hayo alipokuwa akiongea na Waandishi wa Habari kuelezea kero ya umeme inayoukabili Mkoa wa Ruvuma.

Naibu Mkurugenzi amesema mahitaji halisi ya umeme kwa Mkoa wa Ruvuma ni MG 4.3 lakini kwa sasa umeme unaopatikana ni MG 1.6. Jambo linalosababisha kuwepo kwa mgao. Amesema hayo yote yanatokana na kuharibika kwa Mashine 3 zinazosambaza umeme katika Manispaa ya Songea.

Naibu Mkurugenzi wa TANESCO Bonifance Njombe amesema kutokana na jitihada za Shirika la umeme Mashine mbili zimeshatengenezwa na kuweza kupunguza kero za mgao wa umeme, Mashine ya mwisho ikishapona itasaidia kuwa na umeme wa ziada KW 400.

Naibu Mkurugenzi wa TANESCO amesema mashine zinazotumia maji za chipole zikikamilika zitaweza kutoa MG Wat 8 wakati Matumizi ya Chipole ni MG 1 moja tu jambo litakalouwezesha Mkoa wa Ruvuma kuwa na Migawat 14 ambazo zitasambazwa wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma.

MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA(PSPF) WAOMBOLEZA MSIBA WA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA MAREHEMU DKT. WILLIAM A. MGIMWA


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MFUKO WA PENSHENI WA PSPF
Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) unatoa salamu za rambirambi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Wizara ya Fedha na Familia ya aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. William A. Mgimwa
Mfuko utamkumbuka kwa ushauri wake na ushirikiano aliouonyesha akiwa Waziri wa Fedha katika kufanikisha maendeleo na ustawi wa Mfuko.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

AMIN

MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA(PSPF) WAOMBOLEZA MSIBA WA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA MAREHEMU DKT. WILLIAM A. MGIMWA


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MFUKO WA PENSHENI WA PSPF
Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) unatoa salamu za rambirambi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Wizara ya Fedha na Familia ya aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. William A. Mgimwa
Mfuko utamkumbuka kwa ushauri wake na ushirikiano aliouonyesha akiwa Waziri wa Fedha katika kufanikisha maendeleo na ustawi wa Mfuko.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

AMIN

WAZIRICHIZA AMSIMAMISHA KAZI KIGOGO

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Cristopher Chiza
 
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Cristopher Chiza, amemsimamisha kazi mrajisi wa mkoa wa Ruvuma, Watsoni Nguniwa, kwa kushindwa kutatua kero zinazowakabili wakulima wa mkoa huo.
Akitoa agizo hilo jjijini Dar es salaam Waziri Chiza alisema wakati umefika kwa watendaji wote wa wizara yake ambao watashindwa kwenda na kasi ya sheria mpya ya mwaka 2013 wapishe wenyewe kabla rungu la sheria hiyo halijawaangukia.

Mrajisi huyo anatuhumiwa kushindwa kufanya ukaguzi kwa miaka minane na kushindwa kutatua matatizo ya wakulima ya wilaya nne za mkoa wa Ruvuma za Namtumbo, Tandahimba, Songe na Mbinga.

“Sheria ya sasa haitaki mchezo, sasa kama kwa pamoja tumeamua kusimamia kero zinazowakabili wakulima halafu mwingine anakwamisha, ni lazima awajibishwe,” alisema Waziri Chiza katika mahojiano na NIPASHE.

Waziri Chiza alisema baada ya sheria mpya kuanza kufanyakazi anawataka maafisa kilimo wote nchini kuhahikisha wanatatua matatizo ya wakulima bila kushurutisha.

Hata hivyo, alisema kumekuwa na uwelewa mdogo kuhusu wizara yake na kwamba wananchi wamekuwa wa nalalamika kuhusu masoko ya bidhaa za kilimo. 
CHANZO: NIPASHE

MLEMAVU WA KUSEMA NA KUSIKIA AMUUA BABA YAKE MZAZI KWA KUMTANDIKA NA MPINI WA SHOKA.‏

Kijana wa umri wa Miaka 29 mwenye ulemavu wa kushindwa kuongea (Bubu) aliyefahamika kwa jina la Zuberi Hatima Said anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua Baba yake Mzazi  akiwa anamtuhumu kumroga.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Deusdedit Nsimeki amemtaja Marehemu huyo kuwa ni Hatima Said Lung’ande (70) na kwamba katika tukio hilo mtuhumiwa alimuua kwa kumpiga na mpini wa Shoka.
Kamanda Nsimeki aliendelea kufafanua kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 29 /2013 majira ya Saa 12  Jioni katika kitongoji cha Mchangani kilichopo katika Kijiji cha Kazamoyo Tarafa ya Lukumbule Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma.





Alisema kuwa kufuatia hali hiyo mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani ili sharia iweze kufuata mkondo wake baada ya kukamilika kwa taratibu za mahojiano yatakayo washirikisha wataalamu wa Lugha za alama. 

Akizungumzia tukio hilo mkalimani wa familia hiyo Mtoto wa kwanza kati ya watoto wane wa marehemu Lung’ande Bw.Adamu Sadiki alisema kuwa kabla ya tukio hilo ndugu yake huyo ambaye ni kati ya watoto watatu wa marehemu wenye ulemavu huo alidaikuwa kwa muda mrefu amekuwa akimuona marehemu usiku akiwa anamuwangia.

“Tumezaliwa watoto Wanne katika familia yetu kwa Baba na mama Lung’ande lakini kutokana na mipango ya mungu wenzangu wote ni mabubu hivyo mimi nimekuwa kiunganishi kikubwa katika familia, wageni pamoja na ndugu na jama” alisema Bw. Adamu na kuongeza kuwa Zuberi amekuwa akimlalamika baba kuwa ni mchawi siku za hivi kalibuni hali ambayo iliwaweka katika mazingira ya utata miongoni mwao.


Mganga aliye ufanyia uchunguzi mwili wa Marehemu Lung’ande, Dkt. Joseph Ng’ombo alisema kuwa kifo hicho kilisababishwa na tukio la kutokwa na damu nyingi kufuatia kipigo hicho. Alisema katika tukio hilo marehemu aliumia vibaya Kichwani upande wa jicho la kulia pamoja na kupasuka kwa fuvu la kichwa chake na jicho la Kulia kufutia kipigo hicho.

Serikali yaombwa kushirikiana na kampuni binafsi upimaji viwanja

 Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeombwa kuona umuhimu wa kuchukuwa makampuni binafsi ya upimaji wa viwanja ili kuwarahisishia wananchi upatikanaji rahisi wa viwanja badala ya kutegemea halmashauri ifanye kazi hiyo peke yake, anaripoti Cresensia Kapinga, Songea.
Ombi hilo limetolewa hivi karibuni na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Namanyigu uliopo katika halmashauri ya Manispaa ya Songea Bw.Fidolin Malindisa wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye ofisi ya afisa mtendaji wa mtaa huo.
Malindisa alisema kuwa mpango wa mzuri wa serikali wa kupima viwanja kupitia makampuni binafsi umeonekana kuwa na matunda mazuri kwa wakazi wa manispaa ya Songea baada ya mtaa wake kuibua mradi wa upimaji wa viwanja 3000 ambao umekuwa na mafanikio makubwa kwa zaidi ya asilimia 75.
Alieleza zaidi kuwa kila mkazi wa mtaa huo anayehitaji kuwa na kiwanja hawezi kuwa na sababu ya kukosa kwani viwanja vilivyopimwa ni vingi na gharama yake ni ndogo tofauti na ilivyokuwa awali kwani wananchi wa mtaa wake wamehamasika kwa kiasi kikubwa na wana kiu ya kuondokana na makazi holela yaliyokuwa yanawabana hata kupata mikopo kwenye taasisi za fedha.
"Nawashauri wananchi wa mitaa mingine na hata katika halmashauri zingine hapa nchini waige mfano wa mtaa wa Namanyigu ambako wananchi wamepimiwa viwanja vyao kwa gharama nafuu na itamsaidia kila mwananchi kufaidika kupitia ardhi yake mwenyewe,"alisema Malindisa.
Hata hivyo ameipongeza kampuni ya Ardhi Plan yenye makao makuu jijini Dar es Salaam kwa kufanya kazi nzuri ambayo imeonekana machoni mwa wakazi wa mtaa wa Namanyigu kwani viwanja 3000 tayari vimeshapimwa na kwa sasa hivi zinachongwa barabara kwenye maeneo ya viwanja vyote vilivyopimwa na kazi ya uchongaji itakapokamilika watamalizia kwa kupanda mawe na tayari kwa kila mwenye kiwanja atakabidhiwa eneo lake.
Aidha ameiomba halmashauri ya Manispaa ya Songea kuhakikisha kuwa inaunga mkono Kampuni ya Ardhi Plan kwamba kila mkazi aliyepimiwa kiwanja anapewa hati ya kiwanja mapema iwezekanavyo ili wananchi waanze haraka iwezekanavyo kujenga nyumba kwenye maeneo hayo ambayo tayari yameshapimwa

Chanzo;Majira

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa