unnamed
Sophia Abdul (14)
 Na Amon Mtega –  Songea
MTOTO Sophia Abdul (14) anayesoma shule ya msingi Lilahi darasa la tano iliyopo kata ya Mhukulu wilaya ya Songea vijijini mkoani Ruvuma amekumbwa na ugonjwa usiofahamika ambao umejitokeza kwenye  jicho lake  la kulia lililo vimba na kutokezea nje hali inayomletea maumivu makali na kushindwa kwenda shule huku akiomba msaada kwa wasamaria wema.
 Akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za elimu za wilaya hiyo mama wa mtoto huyo Joyce Nyoni alisema kuwa mwanae alianza kupatwa na ugonjwa huo toka Aprili mwaka jana lilianza  kuwasha kisha kujitokeza uvumbe ambao umepelekea jicho hilo kushindwa kuona huku likiwa limetoka kwa nje.
 Alisema baada ya kuona hali ya mwanae inazidi kuwa mbaya alimpeleka katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma na kukutana na madaktari ambao walimwambia kuwa ugonjwa huo hawatauweza badala yake walimtaka atafute fedha ampeleke katika hospitali ya rufaa ya Muhimbili.
Joyce aliongeza kuwa baada ya kupata maelekezo ya madaktari aliamua kupita kuomba msaada kwa wasamaria wema ili kunusuru maisha ya mwanane kwa kuwa yeye mwenyewe hana uwezo wa kifedha na kwamba baba wa mtoto huyo Abdul Rashid alimtelekeza toka akiwa na umri wa mwaka mmoja.
unnamed
Alisema kufuatia hali hiyo mwanae hajahudhuria masomo toka walipofungua shule jambo ambalo linaweza kumrudisha nyuma katika maendeleo yake na haki ya kupata elimu,hata hivyo aliambiwa na madaktari hao kuwa pindi atakapopata fedha za matibabu watamwandikia kibari cha kumruhusu kwenda kupata matibabu Muhimbili.
Aidha mama wa mtoto huyo anawaomba wasamaria wema kutoa mchango wao wa hali na mali ili afanikiwe kumpeleka mwanae kwenye matibabu kiwango cha fedha kinachohitajika hadi sasa hajafahamu baada ya kupewa kibali atafahamishwa kwa watakao guswa na tatizo la mtoto Sophia watoe michango yao kwa simu namba 0683115075 ya mama yake.