HABARI NJEMA KWA WALE WOTE WALIOKOSA NAFASI KUENDELEA NA MASOMO KIDATO CHA TANO SERIKALINI , SASA MNAWEZA KUOMBA KUSOMESHWA SOMA HAPA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


BABA WA KAMBO AMUUNGUZA MIKONO MWANYE KWA KUCHELEWA KURUDI NYUMBANI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


               

Mtoto mmoja wa  miaka nane, mkazi wa Mjimwema Songea mkoani Ruvuma amefanyiwa ukatili wa kutisha na Baba yake wa kambo aitwaye Stan Nyoni kwa kumchoma moto mikono yake yote miwili kwa kosa la kuchelewa kurudi nyumbani.Jeshi la polisi mkoani Ruvuma bado linamsaka mtuhumiwa wa unyama huo,Stan Nyoni ambaye alitoroka baada ya kufanya unyama huo huku mtoto huyo akiwa amelazawa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma Songea.

Tukio hilo la kinyama  limewafanya 

MAGAZETI YA LEO. KURASA ZA MBELE NA NYUMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.























Takukuru yataka sheria ya kufilisi walarushwa

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru,Dk Edward Hosea
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imetoa mapendekezo mapya ya kukabiliana na rushwa ikishauri sheria zirekebishwe kuwabana wenye mali zilizopatikana kinyume cha sheria kushtakiwa na kufilisiwa.
Takukuru imependekeza kuifanyia marekebisho Sheria ya Kupambana na Kuzuia Rushwa, ili kosa la rushwa liwe la uhujumu uchumi na mhusika mwenye mali nyingi anaposhindwa kuthibitisha alivyozipata afikishwe mahakamani na mali zake zitaifishwe.

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hosea, alisema hayo wakati wa majadiliano kwenye semina ya wabunge wa Chama cha Kupambana na Rushwa (APNAC) iliyofanyika mjini hapa mwishoni mwa wiki.

Alisema sheria ya sasa ina upungufu mkubwa, hivyo wanaona ni vema kama ingefanyiwa marekebisho ili kuipa nguvu ya kuwabana watoa na wapokea rushwa pamoja na hao wenye utajiri mkubwa.

Alitaja kwa mfano, sheria ya sasa inatoa adhabu ya kifungo au kulipa faini ya hela kwa mshitakiwa aliyetiwa hatiani na mahakama na inatoa hiari kwa mahakimu kutoa moja ya adhabu kati ya hizo, hivyo wengi wakipewa adhabu ya kulipa faini hawatashindwa.

“Hata kama atatozwa faini ya Sh. milioni 10, watachangishana na mla rushwa ataachiwa huru huku akiendelea kumiliki mali alizojipatia kwa rushwa,” alionya Dk. Hosea na kuongeza: “Tunapendekeza adhabu iwe kifungo na kesi za rushwa ziwe katika kundi la kesi za uhujumu uchumi baadhi ya nchi kama Nepal, Uingereza na Ethiopia wanafanya hivyo.”

Pia alisema wanataka sheria ya madaraka ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) yapelekwa pia kwa Takukuru ili kukamata, kupeleleza, kuendesha mashtaka na pia rushwa iwe na mahakama yake.

Hata hivyo, alisisitiza kuwa kufanya kazi hizo haimaanishi kwamba Takukuru itakuwa inapokonya madaraka ya DPP.
Kuhusu watu wenye mali nyingi, alisema sheria iwatake watu hao kujieleza namna walivyopata mali zao na kama wakishindwa basi wafikishwe mahakamani na mali zao kutaifishwa.

“Hiyo itasaidia sana kupunguza rushwa,” alisema.Mapema akifungua semina hiyo, Jaji Mkuu Mohammed Othman Chande, alisema katika kutathmini mapambano dhidi ya rushwa, siku zote, habari mbaya za rushwa zinachafua matendo au jitihada nzuri za kupambana na rushwa.

Akizungumzia rushwa wakati wa uchaguzi, alisema katika uchaguzi mkuu uliopita, kulikuwa na mashauri 44 ya kupinga matokeo ya uchaguzi huo na mengine yalihusisha vitendo vya rushwa katika kampeni za uchaguzi kwa wagombea.

Alisema kwa mfano, baadhi ya makosa ni wagombea kutoa chakula kwa wapiga kura, kuwapa fedha, kuwakodia magari ya usafiri kutoka sehemu moja hadi vituo vya kupiga kura, kutoa ahadi ya kuboresha miundombinu iwapo mgombea fulani atachaguliwa.

Aliwaambia wabunge hao kuwa kiwango cha kuthibitisha makosa hayo ni cha jinai na siyo cha madai hivyo katika baadhi ya mashauri kulikuwa hakuna ushahidi wa kutosha.

Pia alisema baadhi ya mashahidi walichelewa sana kutoa taarifa tangu kutokea kwa tukio la rushwa na kwamba baadhi yao walijihusisha katika rushwa. Akizungumzia rushwa mahakamani, alisema hakimu anayepokea rushwa anafanya biashara haramu ya kumnyima mlalamikaji haki yake.

Alisema kwa mfano, hakimu anayeendesha kesi hawezi au hatakiwi kukutana na mteja wa upande mmoja wa kesi nje ya mahakama kama vile baa.

Kadhalika, alizungumzia pia kuhusu bajeti ndogo ambayo Idara ya Mahakama inapata na akasema kwa mfano, sera ya serikali inataka mahakimu wa Mahakama ya Mwanzo wasikae kituo kimoja zaidi ya miaka mitatu, lakini kiuhalisia wapo wanaokaa hata miaka 10 kituo kimoja.

Alisema hiyo inatokana na bajeti ndogo ambayo serikali inaipatia mahakama na akafafanua kwamba ili mahakimu hao waweze kuhamishwa kwa mujibu wa muda uliowekwa, gharama ya uhamisho zinakula fedha zote ambazo wametengewa na serikali kwa mwaka.

Alitoa changamoto kwa wabunge kuongeza bajeti na kuwa na Mfuko wa Mahakama kama ambavyo upo Mfuko wa Bunge.

Ofisa Habari wa Bunge, Owen Mwandumbya, akiwasilisha mada kuhusu ‘Uhusiano kati ya Vyombo vya habari na Wanasiasa, alisema uhusiano kati yao ni muhimu, lakini hautakiwa kuzidi sana.

Alisema uhusiano ukizidi sana unaweza kuathiri upatikanaji wa habari kwa jamii, kwa kupewa habari ambazo wanasiasa wanazitaka.

Alisema habari za rushwa ni moja kati nyingi ambazo zinapendwa kuandikwa au kutangazwa kwenye vyombo vya habari, hivyo zinaweza kuwachafua wanasiasa kwa haraka zaidi.

“Kazi kubwa ya vyombo vya habari pamoja na suala la kuelimisha lakini wanataka kufichua maovu na wanapofanya hivyo wanatarajia hatua zitachukuliwa haraka dhidi ya wahusika,” alisema.
 
SOURCE: NIPASHE
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa