Bi. Samia Suluhu Ahaidi Umeme Kila Kijiji Ruvuma, Viwanda vya Mahindi, Kahawa

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu (katikati) akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini, Martin Mtonda (kushoto) na mgombea udiwani wa CCM.


MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu ameanza ziara yake mkoani Ruvuma akiinadi ilani ya chama hicho huku akiahidi neema kwa wakulima wa kahawa na mahindi wa mkoa huo.

Bi. Samia Suluhu ambaye amehutubia mikutano mitatu katika majimbo mawili ya mkoa wa Ruvuma yaani Jimbo la Nyasa na Mbiga Vijijini, akizungumza katika mikutano yake amesema serikali itakayoundwa na CCM endapo itashinda itahakikisha inashusha umeme katika vijiji vyote vya mkoa huo kwa awamu ili kuchochea maendeleo ya wananchi.

Alisema kwa kuwa mkoa huo unazalisha mazao ya mahindi na kahawa serikali itahakikisha inaanzisha viwanda eneo hilo vya kusaga na kuandaa unga wa mahindi kwa wakulima na kuwawezesha ili wauze unga na kunufaika zaidi tofauti na ilivyo kwa sasa ambapo wamekuwa wakilanguliwa.

Alisema viwanda vingine ambavyo Serikali ya CCM itavianzisha ni pamoja na viwanda vya kubangua kahawa na kuiandaa kikamilifu tayari kwa kutumika, jambo ambalo alisema licha ya kuongeza thamani ya zao hilo itaongeza ajira kwa vijana na kuchochea uchumi wa wakulima eneo hilo.
Akizungumzia miundombinu ya barabara ambayo bado ni changamoto kwa mkoa huo hasa vijijini alisema serikali itakayoundwa na CCM chini ya uongozi wa Dk. John Pombe Magufuli pamoja na yeye watahakikisha wanajenga na kuboresha barabara za maeneo hayo ili ziweze kupitika kwa uhakika.

Hata hivyo kiongozi huyo amesema Serikali itakayoundwa na CCM endapo itashinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2015 imejipanga kuboresha vizuri huduma za afya kuondoa ukiritimba na rushwa, elimu kwa kutoa elimu bure toka darasa la kwanza hadi kidato cha nne pamoja na ujenzi wa mabweni na uwezeshaji vijana na akinamama kiuchumi popote walipo mjini na vijijini.

Ziara ya mikutano ya kampeni ya mgombea mwenza huyo wa urais tiketi ya CCM, inaendelea leo katika Mkoa wa Ruvuma na ataingia Jimbo la Tunduru kuendelea kuinadi ilaya ya chama hicho kuomba ridhaa kwa wananchi ili waweze kurejeshwa madarakani na kuunda dola.

Pichani juu ni baadhi ya wananchi na wanaCCM wakiwa wamefurika katika kiwanja cha Kijiji cha Maguu Wilaya ya Mbinga kumsikiliza mgombea mwenza wa urais kupitia tiketi ya CCM alipokuwa akiinadi ilani ya chama hicho.


Pichani juu ni baadhi ya wananchi na wanaCCM wakiwa wamefurika katika kiwanja cha Kijiji cha Maguu Wilaya ya Mbinga kumsikiliza mgombea mwenza wa urais kupitia tiketi ya CCM alipokuwa akiinadi ilani ya chama hicho.
Baadhi ya wananchi na wanaCCM wa Kijiji cha Maguu wilayani Mbinga wakimsubiri mgombea mwenza wa urais, CCM, Bi. Samia Suluhu. 


Pichani juu ni baadhi ya pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda zilizompokea mgombea mwenza wa CCM urais, Bi. Samia Suluhu mara baada ya kuingia Wilaya ya Mbinga zikiwa zimeegeshwa pembeni huku mkutano wa hadhara ukiendelea. 

Mmoja wa wajumbe wa kamati ya kampeni ya mgombea mwenza, Bi. Asumpta Mshama akizungumza na wanaCCM na wananchi (hawapo pichani) katika Kijiji cha Maguu, Wilaya ya Mbinga. 
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu (kulia) akizungumza na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu, kabla ya kuanza kuhutubia katika mikutano wake wa kampeni.  

Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu (katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi wa CCM ambao ni wenyeji wake mkoa wa Ruvuma.

Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu (katikati) akizungumza na mmoja wa vijana walemavu waliohudhuria mkutano wake wa hadhara Kijiji cha Maguu. Bi. Suluhu alimsaidia fedha kijana huyo. 

*Imeandaliwa na www.thehabari.com

LOWASSA AENDELEA "KUTISHA" MAELFU WAFURIKA KUMSIKILIZA HUKO RUVUMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

MGOMBEA kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, akiwapungia maelfu ya wananchi akiwa kwenye gari, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Matarawe, Songea Mjini, Mkoani Ruvuma leo Septemba 1, 2015 ambapo alihutubia mkutano wa kampeni ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni akiwa kwenye mkoa watatu baada ya kuzindua rasmi kampeni zake jijini Dar es Salaam. Mh. Lowassa ameendelea kuonyesha "nguvu" zake kisiasa kutokana na maelfu ya wananchi wanaojitokeza kwenye mikutano yake. (Picha zote na Othman Michuzi)

DK MAGUFULI AKISHINDA URAIS AAHIDI SERIKALI KUJENGA RELI KUTOKA MTWARA HADI MBAMBA BAY RUVUMA, KUPUNGUZA BEI YA VIFAA VYA UJENZI‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
 Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni wa CCM kumnadi mgombea urais Dk John Magufuli  wilayani Masasi leo. Dk Magufuli amesema kuwa CCM ikishinda Serikali  itajenga Reli kuanzia Mtwara hadi Mbamba Bay Ruvuma
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akijinadi katika mkutano wa kampeni mjini Masasi, mkoani Mtwara leo.
 Mfuasi wa CCM  akiwa amejichora usoni huku kidevuni akiwa aqmeandika jina la Mgombea Urais wa Tanzania kuptia CCM, Dk Magufuli.
 Wananchi wakishangilia wakati Dk Magufuli akitoa ahadi mbalimbali za maendeleo endaqpo akichaguliwa
 Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika leo wilayani Namtumbo, Ruvuma. Dk Magufuli alitangaza kwamba akichaguliwa atahakikisha vifaa vya ujenzi bei yake inashuka kupunguza kodik.
 Dk Magufuli akionesha  Ilani ya Uchaguzi kabla ya kumkabidhi Mgombea ubunge jimbo la Namtumbo. Injinia Edwin Ngonyani
 Mama mkazi wa Kijiji cha Chomolo, wilayani Namtumbo, mkoani, akishangilia baada ya Dk Magufuli kutangaza kwamba akishinda urais kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne hawatolipa ada
 Dk Magufuli akihutubia baada ya kuzuiwa  na wananchi katika Kijiji cha Kilimasela wilayani Namtumbo, alipokuwa akienda kufanya kampeni Masasi mkoani Mtwara
  Dk Magufuli akihutubia baada ya kuzuiwa  na wananchi katika Kijiji cha Kilimasela wilayani Namtumbo, alipokuwa akienda kufanya kampeni Masasi mkoani Mtwara
  Dk Magufuli akihutubia baada ya kuzuiwa  na wananchi katika Kijiji cha Nandembo  wilayani Tunduru, alipokuwa akienda kufanya kampeni Masasi mkoani Mtwara
  Dk Magufuli akihutubia baada ya kuzuiwa  na wananchi katika Kijiji cha Matemanga wilayani Tunduru.
 Akina mama wakiwa karibu na mti wenye picha ya Mgombea urais kupitia CCM, Dk John Magufuli
 WAFUASI WA ccm wakishangilia wakati Dk Magufuli akijinadi
 Ni furaha iliyoje kwa Bibi kizee huyu baada ya kumuona Dk Magufuli wakati wa mkutano wa hadhara mjini Tunduru leo
 Dk Magufuli akijinadi katika mkutano wa kampeni mjini Tunduru
 Mrembo akiwa amejiremba ki ccm katika mkutano huo wa kampeni mjini Tunduru
 Baadhi ya wananchi wakiwa juu ya ukuta ili wapate kumuona Dk Magufuli akihutubia mjini Tunduru
 Dk Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Tunduru Kaskazini, Ramo Makani
 Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya Dk Magufuli
 Dk Magufuli akiwapongeza wafuasi wa CUF  waliokihama chama hicho na kujiunga na CCM KATIKA MKUTANO WA HADHARA ULIOFANYIKA MJINI TUNDURU
 Mambo ya warembo wa ccm
 Msafara wa Dk Magufuli ukiwasili  katika Kijiji cha Ligunga, wilayani Nanyumbu, Mkoa wa Mtwara

 Mwanafunzi  akiwa akiparamia mti ili aweze kumuona Dk Magufuli
Dk Magufuli akihutubia wananchi waliomzuia katika Kijiji cha Michiga, wilayani Nanyumbu alipokuwa akienda Masasi kuendelea na kampeni
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa