MKOA WA RUVUMA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA KWA KUSOMESHA WANAFUNZI WA SAYANSI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Katika kuboresha huduma za afya mkoa wa ruvuma kupeleka wanafunzi wanaosomea masomo ya sayansi katika vyuo vya afya ili kuboresha huduma za afya mkoani hapo hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya songea POLOLETH MGEMA habri kamili hii hapa video yake ...

TUNDURU WAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS KWA VITENDO.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma Juma Homera .
Serikali ya Wilaya ya Tunduru imeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli la kujenga kituo cha Afya kila kata kwa nchi nzima, Ambapo wilaya hiyo tayari imenza ujenzi wa kituo cha Afya katika kata ya Nakayaya . Ujenzi wa kituo hicho cha Afya umefikia hatua ya kuezekwa na unatarajiwa kukamilika mwakani .Hii hapa video yenye habari hiyo.

DK. KIGWANGALLA AZINDUA ZOEZI LA UCHUNGUZI WA SARATANI YA MATITI NA SHINGO YA KIKZAZI MKOANI RUVUMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Hamisi Kigwangalla akipokea maelezo kutoka kwa wataalam wa MEWATA juu ya zoezi hilo.
Rais wa MEWATA, Dkt Serafina Baptist Mkuwa akimpa maelezo Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla wakati akizunguka kukagua maeneo ya ukaguzi wa upimaji huo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Hamisi Kigwangalla akipokea maelezo kutoka kwa wataalam wa MEWATA juu ya zoezi hilo.
Zoezi hilo likiendelea
Dk. Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Ruvuma pamoja na Madaktari wa MEWATA katika tukio hilo.
Dk. Kigwangalla akikagua kituo cha zoezi hilo la upimaji wa Afya bure linaloendelea katika Hospitali ya Peramiho.
Dk. Kigwangalla akitoa maelezo wakati wa ukaguzi wa zoezi hilo kwa kituo cha Hospitali ya Paramio.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Hamisi Kigwangalla mapema jana Agosti 24,2017, amezindua rasmi zoezi la upimaji wa Afya bure kwa akina mama linalofanyika kwa siku tatu kwenye uwanja wa Majimaji na maeneo mengine ya Songea Mkoani Ruvuma.

Zoezi hilo linaratibiwa na Chama Cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) kwa ushirikiano na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Serikali ya Mkoa wa Ruvuma. Kampeni itahusisha upimaji wa Saratani ya Matiti, Saratani ya Shingo ya Kizazi, Kisukari, Shinikizo la damu (Hypertension), Magonjwa mengine yasiyo ya kuambukiza na Ugonjwa mengine yakiwemo ya kuambukiza (Kifua Kikuu).

Dk. Kigwangalla aliwashukuru MEWATA, kwakuwezesha zoezi hilola upimaji Afya bure ambapo zoezi hilo linaonyesha dhamira ya kuhakikisha kwamba jamii ya Kitanzania inahamasika katika kupunguza tatizo la saratani kwa ujumla, hususani saratani ya matiti na mlango wa kizazi na matiti.

“Nilipopata mwaliko huu wa kuwa mgeni rasmi katika zoezi hili wala sikusita kabisa, nilikubali kwa vile ninafahamu tatizo la saratani kwa wanawake nchini, na mimi pamoja na Waziri wangu Mhe. Ummy Mwalimu ni wakereketwa wakubwa wa Afya ya mama na mtoto, hivi hatutasita kushirikiana na mtu yeyote mwenye nia njema hususan kwenye eneo hili, hapa Nchini kwetu, kwa ajili ya kupunguza vifo vya mama na mtoto na vitokanavyo na saratani.” Alieleza Dk. Kigwangalla.

Dk. Kigwangalla amebainisha magonjwa yasiyo ya kuambukiza yakiwamo saratani, kisukari, magonjwa ya moyo, magonjwa sugu ya mfumo wa hewa, magonjwa ya figo, seli mundu, na magonjwa ya akili, kwa sasa yamekuwa yakiongezeka kwa kasi kubwa duniani kote na hapa nchini pia. Magonjwa haya huchangia zaidi ya asilimia hamsini ya mzigo wa magonjwa duniani kwa vile husababisha gharama kubwa za matibabu, ulemavu na hata vifo.

“ Tanzania na nchi nyingine kusini mwa Jangwa la Sahara zina viwango vya juu vya saratani ya matiti na mlango wa kizazi. Nchini Tanzania, katika saratani zinazo wapata zaidi wakina mama, saratani ya mlango wa kizazi inaongoza ikifuatiwa na saratani ya matiti. Saratani hizi mbili kwa pamoja husababisha zaidi ya asilimia 50 ya vifo vyote vya wakina mama vitokanavyo na saratani.

Takwimu katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road zinaonyesha kuwa saratani ya mlango wa kizazi ndiyo inayoongoza kwa asilimia 36% (zaidi ya theluthi moja) ya wagonjwa wote wanaohudhuria katika taasisi. Aidha, mnamo mwaka 2005, kulikuwa na wagonjwa wapya 2500, ukilinganisha na wagonjwa wapya 5200 mwaka 2016. Hii inaonyesha dhahiri kuwa wagonjwa wameongezeka kwa asilimia 100% kwa kipindi cha miaka 10. Idadi hii ni kubwa sana, hivyo juhudi na ushirikiano zaidi zinahitajika katika kupunguza vifo hivi kwa kushirikiana na taasisi na mashirika binafsi kama MEWATA na wengine katika kutoa huduma za uchunguzi wa awali na matibabu.” Alieleza Dk. Kigwangalla wakati akihutibia wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye uzinduzi huo.

Akielezea kuhusiana na tatizo la kisukari, Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, tafiti za ugonjwa wa kisukari zinaonyesha kuwa mwaka 2007 kulikuwa na wagonjwa 246 milioni duniani. Takwimu za mwaka 2015 kutoka kwenye Atlas ya kimataifa ya Kisukari, zinaonyesha kuwa kulikuwa na wagonjwa milioni 415 duniani kote. Ifikapo mwaka 2040 inatarajiwa kuwa na wagonjwa milioni 642.

“Katika bara la Afrika kulikuwa na wagonjwa wa kisukari milioni 14.2 mwaka 2015 na idadi hii itaongezeka na kufikia milioni 34.2. Kwa Tanzania mpaka mwaka 2015 kulikuwa na jumla ya wagonjwa 822,880 wa kisukari. Utafiti uliofanyika mwaka 2012 na kuhusisha wilaya 50 nchini Tanzania ulionyesha ya kuwa asilimia 9.1 ya Watanzania wenye umri wa miaka 25-64 wana ugonjwa wa kisukari. Hii inaonyesha ni jinsi gani ugonjwa wa kisukari unavyoongezeka, na namna amabvyo mazoezi haya yatasaidia kwenye juhudi za Serikali za kupambana na magonjwa haya.” Alieleza Dk. Kigwangalla.

Kwa upande wake, Rais wa MEWATA, Dkt Serafina Baptist Mkuwa, amewataka wanawake mkoa wa Ruvuma kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi hilo ili kubaini tatizo mapema ili kuweza kuchukua hatua.

“Wananchi wa mkoa wa Ruvuma na mikoa yote ya jirani, ni wakati mzuri wa kuitumia vyema fursa hii muhimu, kuja kujichunguza afya zenu, na zoezi hili ni bure kwa watu wote” alieleza Dk. Mkuwa.

Katika tukio hilo pia lilishuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dkt Gosbert Mutayabarwa Wakuu wa Wilaya za Songea Mjini na vijijini, Waganga Wakuu wa Wilaya, Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwemo Mbunge wa Songea Mh, Gama, pamoja na madiwani wote.

VIDEO - MATUKIO YA WIKI YALIYOJILI MKOANI RUVUMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

WAZIRI JENISTA, NAIBU WAZIRI DKT. KALEMANI WAZINDUA MRADI WA USAMBAZAJI UMEME VIJINI REA III KWA KUGAWA VIFAA VYA UMEME TAYARI (READY BOARD MKOANI RUVUMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe.Jenista Mhagama, akikabidhi kifaa kijulikanacho kama umeme tayari(Ready Board) kikichobuniwa na Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO),  kwa mwanakijiji wa kijiji cha Litapwasi, Peramiho, Mkoani Ruvuma wakati wa uzinduzi wa mradi wa Usambazaji umeme vijijini unaoratibiwa kwa pamoja na Wakala wa Umeme Vijijini REA na Shirika la Umeem Tanzania , (TANESCO), ambapo uzinduzi huo ni awamu ya tatu. Uzinduzi huo ni mwendelezo wa kazi kama hiyo ulioanzishwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medad Kalemani(aliyeshika vipaaza sauti) kwenye mikoa mbalimbali nchini


NA MWANDISHI WETU SONGEA.
KAMPENI ya kuhakikisha vijiji vyote nchini vinapatiwa umeme, imeendelea jana (Agosti 16, 2017), mkoani Ruvuma, ambapo Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, amezindua  mradi huo kwenye kijiji cha Litapaswi, wilaya ya Songea vijijini mkoani Ruvuma, kwa kugawa vifaa vijulikanavyo kama umeme tayari (Ready Board) kwa wanakijiji.
Katika hafla ya uzinduzi huo, uliofanywa kwa pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Watu Wenye Ulemavu), Mheshimiwa Jenista Mhagama, Wanakijiji walipatiwa vifaa hivyo vinavyowezesha umeme kuwaka mara moja bila ya kuhitaji (mtandao wa waya kwenye nyumba- (Wiring).
“Kifaa hiki ni maalum kwa matumizi ya nyumba isiyozidi vyumba viwili na mwanakijiji analipia shilingi elfu 36,000 tu kupata kifaa hiki.” Amefafanua Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji ambaye anafuatana na Naibu Waziri kwenye ziara hiyo.
Hali kadhalika alisema, kifaa hicho kwa sasa kinapatikana kwenye ofisi zote za TANESCO za Mikoa na Wilaya kwenye mikoa ambayop tayari mradi huo umezinduliwa.
Alisema, tayari Naibu Waziri amekwishazindua mradi kama huo kwenye mikoa yote ya Tanzania bara isipokuwa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Kigoma, na Katavi.
“Jambo la kufurahisha sana ni kwamba mradi huu wa REA III, unafadhiliwa na Serikali yetu kupitia Wakala wa Nishati Vijijini na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO)” alifafanua Bi. Muhaji.




MATUKIO MBALIMBALI YALIYO JIRI MKOANI RUVUMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Wakwanza kutoka kushoto ni Ditha Nyoni na Nancy Mbogoro watangazaji wa RUVUMA TV, Kama ulipitwa na matkio ya wiki yaliyo jili mkoani ruvuma kuanzia tarehe 07-13 August 2017 basi tumekusogezea matukio hayo kama ilivyo kawaida yetu.

VIDEO:JESHI LA POLISI USALAMA BARABARANI MKOA WA RUVUMA KUFUNGUA KLABU MIA MOJA ZA USALAMA KWA SHULE ZA MSINGI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa ruvuma ABEL SWAI apania kupunguza ajali za barabarani kwa wanafunzi kwa kufungua klabu za usalama ili kusaidia wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

MALI ZA MIL 300/- ZANADIWA KULIPA MADENI YA USHIRIKA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

VIDEO – MATUKIO 12 YALIYO MAKE HEADLINES MKOANI RUVUMA KUANZIA 07 -13 AUGUST 2017

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wakwanza kutoka kushoto ni Ditha Nyoni na Nancy Mbogoro watangazaji wa RUVUMA TV, Kama ulipitwa na matkio ya wiki yaliyo jili mkoani ruvuma kuanzia tarehe 07-13 August 2017 basi tumekusogezea matukio hayo kama ilivyo kawaida yetu.

WILAYA YA NEWALA INAHITAJI TEKNOLOJIA YA KISASA KUINUA KILIMO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Mkuu wa Wilaya ya Newala, Aziza Mangosongo, akizungumza na maofisa ugani wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya jinsi ya kutumia sayansi na teknolojia katika kuboresha kilimo kwa maofisa ugani kutoka  Halmashauri ya Wilaya ya Newala ambayo yameandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB). Kutoka kushoto ni Mtafiti, Bestina Daniel kutoka COSTECH na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya hiyo, Ally Lilama. 

WILAYA SONGEA HATARINI KUGEUKA JANGWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Imeandikwa na Muhidin Amri, Songea
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Polole Mgema
WILAYA ya Songea mkoani Ruvuma inakabiliwa na tishio la kugeuka jangwa kutokana na wananchi kukata miti, kuchoma misitu moto na baadhi ya watumishi wasiokuwa waadilifu kuruhusu wafugaji kutoka mikoa mbalimbali nchini kuingiza idadi kubwa ya mifugo bila kufuata sheria.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea, Polole Mgema wakati akitoa salamu za serikali katika kikao cha Baraza la Madiwani cha Halmashauri ya Wilaya ya Songea kilichofanyika katika Kijiji cha Lundusi katika Kata ya Maposeni.
“Kuna uharibifu mkubwa katika mlima Lihanje na nimekuwa nikitoa maagizo kwa watendaji wetu mara kwa mara kusitisha shughuli za kilimo katika mlima ule, hata hivyo bado imeonekana baadhi ya wananchi wanaendelea kukata miti na kufanya shughuli zao za kibinadamu,” alisema Mgema na kuongeza: “Kuna watumishi ambao ni wagumu sana kutekeleza maagizo ya serikali sasa mimi mwenyewe nitaanza operesheni ya kuwaondoa ndugu zenu, lakini msije kunilaumu kwa hatua nitakayochukua.”
Kwa mujibu wake, ataanza kupita kijiji hadi kijiji kwa ajili ya kuwatangazia wananchi kuhusu mpango wa serikali kutunza mlima Lihanje kutokana na umuhimu wake baada ya kuona watumishi waliopewa dhamana ya kusimamia uhifadhi wa mazingira katika mlima huo kushindwa kutimiza wajibu wao kwa sababu wanazozijua. Aidha, amewataka watumishi na madiwani kusimamia vema agizo la serikali la kutoruhusu uingizaji mifugo kutoka mikoa mingine na kuzuia biashara ya mkaa kwenda nje ya Wilaya ya Songea.
CHANZO HABARI LEO

SHUGHULI MBALIMBALI ZA KILELE CHA SIKU YA WAKULIMA NANE NANE MKOANI RUVUMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 Katibu tawala msaidizi utumishi na utawala katika sekretarieti ya mkoa wa Ruvuma  Bw. Biseko Bwai (kushoto) akiangalia maziwa yaliyosindikwa na mjasilimali mdogo aliyefahamika kwa jina moja la mama Tarimo wakati wa kilele cha siku ya wakulima nane nane mkoani Ruvuma jana.

 Afisa kilimo kutoka halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Bw. Jibinza Masaba (kushoto)  akiwaeleza baadhi ya wananchi waliofika katika maonesha ya siku ya wakulima nane nane nyanya ambazo zinaweza kuishi na kuzaa kwa muda wa miezi sita tofauti na nyanya nyingine ambazo zinaishi kwa miezi miwili.
 Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Songea wakiangalia kibao kinachoonesha aina ya mbegu ya ngano na mahindi yenye uwezo wa kutoa gunia 40 kwa ekari moja katika viwanja vya nanenane  wakati wa kilele cha mnaadhimisho ya siku ya wakulima mkoani Ruvuma. Picha na Muhidin Amri

UNAJUA?: ANGALIA PICHA YA JIWE LA AJABU NCHINI TANZANIA NA HAIRUHUSIWI KULIPANDA WALA KULISOGELEA!! KWANI NI HATARII

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Haya ndio maajabu ya Jiwe la Mbuji Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma
Maana ya neno Mbuji ni "Kitu kikubwa"

1. Ni jiwe pekee kubwa Mkoani Ruvuma,

2. lina vyanzo vingi vya maji chini yake, 
3. Ni ngumu kulipanda na ukithubutu yatakayokukuta ni
juu yako na tayari Mzungu mmoja kapoteza maisha'
4. Ni ngumu kulizunguka,

5. Hutumika kwa matambiko kwa baadhi ya koo,

6. Kuna watu maalumu wanaotoa maelekezo kwa yeyote
anayetaka kulifikia ama kupanda,

7. Ni kivutio kikubwa kwa wageni wachache ambao
hutembelea Litembo, Maguu, Hagati nk huko Mbinga,
8. Linaheshimika sana na wakazi wanaolizunguka jiwe
hilo,
9. Sehemu kubwa ya watu wananchi wanaolizunguka
hawajawahi kulipanda wala kulisogelea kwa hofu,
10. Jina la jiwe hilo ndilo jina la Tarafa ya Mbuji wilayani
Mbinga.

VIDEO - KIJANA AELEZEA MKASA WA BABA YAKE MZAZI PAMOJA NA BIBI YAKE WALIVYOLIWA NA MAMBA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Kijana Emidio Nkoma mkazi wa kijiji cha Londo kilichopo Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma, Aelezea mkasa wa baba yake mzazi pamoja na bibi yake walivyoliwa na mamba katika Daraja la mto Rwika ambalo linaunganisha kijiji cha Londo na Ngido .

WAKULIMA RUVUMA WATAKIWA KULIMA MAZAO YENYE TIJA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Wakulima mkoani RUVUMA wametakiwa kuzalisha mazao yeye tija ili kukuza sekta ya kilimo na kupanua uzalishaji ili kuifanya nchi ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ambapo mkoa wa ruvuma ni kati ya mikoa inayozalisha chakula kwa wingi hapa nchini Tanzania.

HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE

WAUMINI WA KANISA LA EFATHA MJINI SONGEA WACHANGIA DAMU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


Waumini wa kanisa la EFATHA MINISTRY lililopo katika manispaa ya SONGEA mkoani RUVUMA wamejitokeza kwa wingi kuchangia damu kwa watu wenye uhitaji wa damu, ambapo zoezi hilo la kuchangia limefanyika kanisani hapo. PHILIPO GUNI ni baba wa kiroho katika kanisa hilo anasema kutokana na mateso mengi wanayoyapata ndugu zetu hususani akina mama wajawazito na watu wanaopata ajali ndicho kilicho wasukuma zaidi.habari kamili hii hapa video yake
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa