TBA WATUNISHIANA MISULI NA HALMASHAURI YA NYASA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) waikatalia halmashauri ya wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma kukatisha mkataba wa ujenzi wa ofisi za halmashauri hiyo,Hii ni baada ya Baraza la madiwani la halmashauri hiyo kukubaliana kwa pamoja na kustisha mkataba. Wasema kama halmashauri itasitisha mkataba itabidi halmashauri iwalipe fidia TBA.

NAIBU SPIKA MH. DKT TULIA ACKSON AKABIDHI HUNDI YA TSH MIL.8 KUCHANGIA UJENZI WA HOSPITALI WILAYA YA NAMTUMBO.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mgeni rasmi Mh. Dkt Tulia Ackson akinadi korosho katika harambee yauchangiaji wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya Namtumbo iliyofanyika jijini Dar es salaam
   Mgeni rasmi Mh Dkt Tulia Ackson na baadhi ya viongozi wakitazama makala fupi ya Ujenzi wa Hospitali hiyo ilipoanza na baadhi yamajengo ya hospitali hiyo ya Wilaya ya Namtumbo

Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Mantra Bw. Fredy Kibodya akielezea jambo kwa mgeni rasmi katika harambee ya uchangiaji wa Hospitali ya Wilaya ya Namtumbo

Mgeni rasmi Mh Dkt Tulia Ackson akikabidhi mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi millioni  nane kuchangia ujenzi wa hospital ya Wilaya ya Namtumbo

Mkuu wa wilaya ya namtumbo Bi. Luckness Alima akilia kwa furaha baada ya kuchangiwa sehemu ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali hiyo.


RC RUVUMA AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUSIMAMIA VYEMA MAADILI YA WAUMINI WAO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme amewataka viongozi wa dini mkoa humo kusimamia vyema maadili ,unywaji pombe uliokithiri pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya amesema hayo wakati akizungumza na viongozi wa dini katika ikulu ndogo mjini songea

VIDEO:NAIBU WAZIRI WA UJENZI AMTAKA MKANDARASI KUMALIZA DARAJA KWA WAKATI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu waziri wa ujenzi ELIAS KWANDIKWA amemwagiza mkandarasi anayejenga daraja la RUHUHU liliopo lituhi wilayani nyasa mkaoni ruvuma ambalo pia linganisha mkoa wa LUDEWA kukamilisha kwa wakati ili kupisha shughuli za maendeleo zinazofanywa na wananchi katika maneneo hayo. Naibu waziri kwandikwa amesema hayo mara baada ya kukagua ujenzi wa daraja hilo na kuridhishwa na hali ya ujenzi unaofanya na kampuni ya lukolo HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE

VIDEO:RC RUVUMA AWAONYA WAFANYABIASHARA WA MBOLEA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma B CHRISTINA MNDEME amefanya ziara ya kushitukiza katika maghara ya SONAMCU ya kuhifadhia mbolea huku akikuta uchache wa mbolea katika maghara hayo habari kamili hii hapa video yake.

VIDEO:WAZIRI MKUU AWATAKA VIONGOZI WA HALIMASHAURI YA WILAYA YA NYASA KUMALIZA TOFAUTI ZAO.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Waziri mkuu wa Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania KASSIM MAJALIWA, amewaagiza viongozi wa halimashauri ya NYASA akiwemo mbunge wa jimbo hilo, mkuu wa wilaya na mkurugenzi, kumaliza tofauti zao na madala yake wawaletee wananchi maendeleo. Rai hiyo ameitoa wakati akizungumza na watumishi na wakuu wa idara mbalimbali wa halimashauri ya wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.

VIDEO:WAZIRI MKUU AMEIAGIZA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KUUNDA CHOMBO KITAKACHOSIMAMIA MASUALA YA FUKWE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Waziri mkuu KASSIM MAJALIWA ameiagiza wizara ya maliasili na utalii kuunda chombo kitakachomamia maeneo yenye fukwe, ili kulinda maeneo hayo yaweze kuvutiwa na watalii wakigeni wanaokuja katika maeneo hayo. Waziri mkuu ameyasema hayo wakati wa kufunga tamasha la utalii lililofanyika MABAMBA BAY wilayani ya NYASA mkoani Ruvuma.

UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA SONGEA MJINI WAZIDI KUIMALIZA KAMBI YA UPINZANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Moses Machali akimnadi Dkt Damas Ndumbaro
Wakati kampeni za kuelekea uchaguzi mdogo wa jimbo la Songea mjini mkoani Ruvuma zikiendelea katika kata mbalimbali za manisipaa ya Songea mkoani Ruvuma kwa ajili ya kumpata mbunge wa jimbo hilo ambaye chama cha mapinduzi kimemteua Dkt Damas Ndumbaro kupeperusha bendera ya chama hicho waliokuwa viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani nchini wamezidi kujitokeza kwenye kampeni hizo na kutangaza kuachana na vyama vyao vya awali.

Miongoni mwa viongozi hao wa vyama vya upinzani ni pamoja na waliokuwa wajumbe watatu wa serikali ya mtaa wa Majengo mjini Songea kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo ambao walitangaza uamuzi huo wa kukihama chao hicho na kujiunga na chama cha Mapinduzi baada ya hotuba ya siku mbili mfululizo kwenye kampeni hizo za kumnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya chama cha mapinduzi iliyotolewa na aliyewahi kuwa mwanachama wa chama na kingozi pia cha Demokrasia na maendeleo Moses Machali.

Katika hotuba yake ya kumnhadi mgombea huyo Machali alieleza sifa alizo nazo mgombea Dkt Damas Ndumbaro ambazo alizifahamu muda mrefu tangu akiwa kwenye kambi ya upinzani ambazo alisema hazina mashaka yoyote ya kumfanya asichaguliwe kuwa mwakilishi wa wananchi wa jimbo hilo na kuwataka wananchi wa jimbo la Songea mjini kwa ujumla kuitokeza kwa wingi siku ya Januari 13 mwaka huu kumpigia kura mgombea huyo na kuacha kuendelea kusikiliza na kufuata propaganda za wagombea wa vyama vya upinzani ambao walio wengi hawajui kilichoko kwenye vyama hivyo vya upinzani kwa sababu yeye alikuwepo huko na anajua kulivyo.

Viongozi wengine wa kambi ya upinzani waliopanda jukwaani katika viwanja vya mikutano vya Majengo na kutangaza kujiunga na chama cha mapinduzi ni pamoja na aliyekuwa katibu wa chama cha ACT Wazalendo mkoa wa Kigoma Sharon Msanya ambaye kabla ya kutangaza kujiunga na chama cha mapinduzi aliwataka wapiga kura wa jimbno la Songea mjini kutokuthubutu kulifanya jimbo hilo kuwa kambiya upinzani kwa sababu kufanya ni kurudisha nyuma jitihada za serikali za kuwaletea wananchi maendeleo ambayo wameyahityaji kwa muda mrefu kurtoka serikalini na serikali ya awamu ya tano inaendelea kuonesha dhamira ya dhati kuwafikishia wananchi maendeleo hayo.

Alisema yeye amekuwa kiongozi mkubwa wa chama cha ACT Wazalendo katika ngazi ya mkoa lwa Kigoma akini amefikia uamuzi huo wa kusafiri kutoka mkoani Kigoma mpaka mjini Songea ili aweze kupata fursa ya kuwaeleza wananchi wa Songea umuhimu wa kukiunga mkono chama cha mapinduzi na mgombea wake Dkt Dams Ndumbaro kwa ajili ya maendeleo yao na taifa kwa ujumla kwa sababu mgombea huyo amekuwa mpigania maendeleo ya taifa kwa muda mrefu hata kabla hajafikia uamuzi huo wa kugombea nafasi hiyo ya kuwawakilisha wananchi wa jimbo lake.

Huku naye Edna Sunga aliyekuwa katibu wa kamati ya maendeleo ya jamii taifa na mjumbe wa kamati kuu na halmashauri kuu taifa wa chama cha ACT Wazalendo akizungumza baada ya kukihama chama hico na kujijnga na chama cha mapinduzi amesema kwa sababu yeye ni muumini wa kuzingatia miiko na vita dhidi ya rushwa na kuwaletea maendeleo wananchi ameona hana sababu ya kuendelea kuwa kwenye upinzani badala ya kuongeza na kujnganisha nguvu ya kuwajhudumia wananchi walio wengi.

Amesema kiongozi au mwananchi yeyote mwenye dhamira ya dhati ya maendeleo ambayo wananchi walio wengi wanayahitajihana budi kukiunga mkopno chama cha mapinduzi na mgombea wake ambaye amevaa taswira ya chama hicho na taifa kwa ujumla huku naye mgombea wa jimbo hilo kwenye uchaguzi huo akiendelea kuwaomba wananchi wa mji wa Songea kujiktokeza kwa wingi siku hiyo ya uchaguzi kwa ajili ya kupiga kura kwa chama cha mapinduzi.

Na Nathan Mtega, Jamvi la habari - Songea

MHASIBU HALMASHAURI YA NAMTUMBO MKOANI RUVUMA AJISHINDIA KITITA CHA SHILINGI MILIONI 50 ZA TATUMZUKA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Mh.Luckiness Amlima akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 50 Mkazi wa wilaya ya namtumbo mwenye umri wa miaka 31,ambaye ni Mhasibu msaidizi wa halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoa wa Ruvuma,ndugu Jacob Ndee aliyejishindia kitita cha shilingi milioni 50 .
 
Akielezea kwa furaha za kushinda kitita cha milioni 50 za mchezo huo wa kubahatisha wa TatuMzuka,Jacob alisema kuwa ndoto yake kubwa siku akipata fedha za kutosha atazitumia kwa Kilimo,Anasema kwa sasa anaona ndoto yake imetimia baada kupata fedha hizo,hivyo atazitumia katika kilimo.
 Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Mh.Luckiness Amlima akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa Kitita cha Milioni 50 cha TatuMzuka Ndugu Jacob Ndee pamoja na baadhi ya Wadau wengine,ambapo pia walionekana kuuufurahia ushindi wa Jacob,ambaye ni Mhasibu msaidizi wa halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoa wa Ruvuma.

Dkt KALEMANI akagua maeneo ambayo Waziri Mkuu ataweka Jiwe la Msingi

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ametembelea maeneo mawili anayotarajiwa kuwekewa jiwe la msingi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa tarehe 7/01/2018 katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

Mradi wa kwanza aliotembelea ni wa jengo la Tanesco Mkoa wa Ruvuma lililoanza kujengwa mnamo mwaka 2014 ambao ulitarajiwa kukamilika mwishaoni mwa mwaka jana na kushindikana kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa Mkandarasi.

Aidha mradi wa jengo hilo unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili mwaka huu na kuanza kutumika rasmi.

Pamoja na kutembelea jengo hilo la Ofisi ya Tanesco Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Kalemani alitembelea eneo kunakojengwa mitambo ya kupoozea umeme katika mradi mkubwa wa kusafirisha umeme wa Makambako Songea uliopo wilayani Songea mkoani Ruvuma ambako alijadiliana na wataalamu na kuweka baadhi ya vitu sawa tayari kwa ajili ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kuweka jiwe la msingi. Meneja wa Mradi Mkubwa wa Usafirishaji wa Umeme wa Makambako - Songea Mhandisi Didas Lyamulya akitoa maelezo ya mradi kwa Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alipotembelea eneo la ujenzi wa mitambo ya kupoozea umeme unaoendelea kujengwa wilayani Songea mkoani Ruvuma.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirirka la Umeme Tanzania (Tanesco) akieleza jambo mbele ya wajumbe walioambatana na Waziri wa Nishati ili kukagua eneo litakalowekwa jiwe la msingi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika eneo la ujenzi wa Mitambo ya Kupoozea Umeme katika mradi wa Kusafirisha umeme wa Makambako Songea.Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (wa kwanza kushoto ) akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kupoozea umeme katika mradi wa Kusafirisha Umeme wa Makambako-Songea wilayani Songea tayari kwa ajili ya kuwekwa kwa jiwe la msingi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kesho Tarehe 7/01/2018.Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania Dkt. Tito Mwinuka akimweleza jambo walipotembelea eneo la uzinduzi wa mradi wa kusafirisha umeme wa Makambako-Songea ili kujionea maandalizi ya uzinduzi huo.

VIDEO:RAIS MAGUFUL ATOA BILIONI 210 KWA AJILI YA UJENZI WA MRADI WA UMEME SONGEA HADI MAKAMBAKO.

Serikali Kupitia Wizara Ya Nishati Imetoa Kiasi Cha Shilingi Bilioni 210 Kwa Ajili Ya Mradi Wa Umeme Kupitia Makambako Hadi Mkoani Ruvuma ambao utakuwa na uwezo wa kuhudumia wananchi zaidi ya 22,000 sawa na vijiji 120 kwa mikoa yote miwili RUVUMA na NJOMBE.HABARI KAMILI HII VIDEO YAKE

VIDEO:RC MNDEME MKANDARASI WATAKAYESHINDWA KUTIMIZA WAJIBU WAKE MWONDOENI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
mkuu wa mkoa wa ruvuma CHRISTINE MNDEME amemwagiza kurugenzi wa maji mjini songea SOWASA kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi huku wakandarasi watakao kiuka mikataba kwa kushindwa kutimiza majukumu yao basi waondolewe mara moja habari kamili hii hapa video yake

VIDEO:RC RUVUMA AMELITKA SHIRIKA LA UMEME MKOA WA RUVUMA KUTOWAFUMBIA MACHO WADAIWA SUGU.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
NA DITHA NYONI RUVUMATV
 Mkuu mkoa wa Ruvuma CHRISTINE MNDEME amelitaka shirika la umeme mkoa wa ruvuma kutowa fumbia macho wadaiwa sugu wa umeme kwani kufanya hivyo nikuitia hasara serikali kwani hizo ni pesa ni kodi za wananchi hivyo hata kama ofisi yake inadawa wanapaswa kukata umemee.

VIDEO:WANAFUNZI WA SHULE YA WASICHANA SONGEA WATOA WITO KWA VYOMBO VYA MOTO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Klabu ya usalama barabarani kutoka shule ya sekondari wasichana songea imeendesha mafunzo ya usalama barabarani kwa madereva pikipiki na magari katika manispaa ya songea habari kamili hii hapa video yake.

RC RUVUMA AKANUSHA TAATIFA ZIANAZOZAGAA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII KUWA MAPIGA MARAFUKU KUITA BABY

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
NA DITHA NYONI    WA RUVUMA TV
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amekanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amepinga marafuku wananchi wa mkoa wa Ruvuma wasiitane baby.
Tamko hilo amelitoa wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ikulu ndogo ya mkoa wa Ruvuma , hii inakuja baadaya ya taarifa kuzagaa na yenye picha inayoonesha mavazi tofauti na eneo alilokuwa anatoa ujumbe katika shule ya sekondari NASULI na MBAMBA BAY huku ujumbe ukisomeka “marukuku kuitana baby” mkuu wa  mkoa wa Ruvuma.
Inline image 2
Hii ni picha inaonyesha tofauti na mazingira 
Inline image 1Na hii ni picha inaonyesha eneo ambalo mkuu wa mkoa akizungumza na wanafunzi wa NASULI sekondari
Ikumbukwe Novemba 8 mwaka huu, mkuu wa mkoa wa Ruvuma alifanya ziara katika halimashauri ya natumbo katika shule ya sekondari nasuli na kuzungumza na wanafunzi hao, huku kampeni kubwa ili kuwa ni kueneza ujumbe wa kumtaka mwanafunzi wa kike kuvaa maguni manne ambayo ni sare ya shule,joho la maafari,gauni la harusi,na matreniti dress
“ili muweze kufanikisha masomo yenu watoto wakike lazima mvae magauni ili muweze kufanikisha malengo yenu”pia mkuu wa mkoa wa Ruvuma aliongeza kuwa ni marafuku watoto wa kiume na wakike kuitana baby
“msikubali kuitwa baby kwa sababu kukubali kuitwa baby ni chanzo cha kujiingiza kwenye mapenzi,mskubali kuitwa queen we ni mwanafunzi unatafuta maisha na wala usikubali kuitwa mrembo au mzuri alisema Rc MNDEME.
Lengo ya kampeni ni kumsaidia mwanafunzi wa kike aweze kufikia ndoto zake za kielimu na kuweza kufanikisha malengo yake.
Kufatia taarifa hizo mkuu wa mkoa alisema ilikuwa inawalenga wanafunzi wa kike na sio watu wazima kwani taarifa zinazoenezwa na makundi ya watu wachache zinalengo la kupotosha umma hivyo wakazi wa mkoa wa Ruvuma wapaswa kupuuzia
Aidha amewataka wazazi na jamii kwa ujumla kutumia kauli mbiu hiyo ya magauni manne ili iwe chachu kwa wanafunzi wa kike waweze kufanikisha ndoto zake,kwani wanaofanya hivyo hawana nia nzuri wa watoto wa kike 

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa