
Sophia Abdul (14)
Na Amon Mtega – Songea
MTOTO Sophia Abdul (14) anayesoma shule ya msingi Lilahi darasa la tano iliyopo kata ya Mhukulu wilaya ya Songea vijijini mkoani Ruvuma amekumbwa na ugonjwa usiofahamika ambao umejitokeza kwenye jicho lake la kulia lililo vimba na kutokezea nje hali inayomletea maumivu makali na kushindwa kwenda shule huku akiomba msaada kwa wasamaria wema.
Akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za elimu za wilaya hiyo mama wa mtoto huyo Joyce Nyoni alisema kuwa mwanae alianza kupatwa na ugonjwa huo toka Aprili mwaka jana lilianza kuwasha kisha kujitokeza uvumbe...