
MWANAFUNZI wa kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya St. Anthony Mbagala, mkoani Dar es Salaam, Franco Donald Kisongo (18),(pichani) aliyepotea jijini humo Machi 18 mwaka huu, amepatikana Mbinga mkoani Ruvuma.
Kijana huyo aliyekuwa mgeni jijini Dar es Salaam alipotea siku nne tu tangu ajiunge na shule hiyo kuanza masomo ya kidato cha tano.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika familia ya Franco, kijana huyo alifika kwao Mbinga mkoani Ruvuma Machi 23, akiwa peke yake.
Inadaiwa kuwa, baada ya kufika kwao, alisema kuwa hajui alifikaje huko akiwa ametumia takribani siku sita njiani kutoka Dar es Salaam.
Machi 18 asubuhi, Franco aliwaaga...