Wakati Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania (TCRA) juzi iliamua kuingia rasmi katika Mfumo wa Mawasiliano ya Televisheni na Redio kwa kurushwa katika mfumo wa kisasa wa Dijitali kutoka ule mfumo wa Analojia, Shirika la Usambazaji Umeme TANESCO nao wameamua kuingia katika Mfumo wa Dijitali kwa staili ya kupandisha nguzo ya Umeme katika mti halisi ambao bado unamea kama jinsi taswira hizi zinavyoonesha. Hii ni Huko Mkoani Ruvuma, na TANESCO mkoani humo wameamua kutumia njia hii kurahisisha usambazaji umeme.
Pia baadhi ya wananchi wanahoji au shirika limeamua kufanya hivi baada ya udhibiti wa Nguzo hewa kutoka Afrika Kusini kufanyika? Ama ndo teknolojia yao Mpya 2013.
Jionee jinsi Tanesco walivo nateknolojia ya kisasa
Kweli huu ni mwaka mpya
Mambo hayo
Jiulize kwa hali kama hii Tanesco wako juu kwa mfumo huu au wanajaribu nao mfumo wao mpya:SOURCE:Demashonews Blog
0 comments:
Post a Comment