MSHUHUDIE MAMA HUYU ALIYE JIFUNGUA WATOTO WATANO , HUKO SONGEA , WATAZAME HAPA

Bi Jane Mlelwa aliyekaa kitandani akiwa amebeba mmoja wa  wawatoto watano aliowazaa kabla ya watototo hao kufa wote(Picha na maktaba)
Hawa ndio watoto aliojifungua katika hospital ya Mkoa wa Ruvuma na kesho wakafaliki dunia (Picha na maktaba)
..........................................................................
Na Nathan Mtega,Songea


 MWALIMU Sophia Mgaya(28) mkazi wa Ruhuwiko mjini Songea mkoani Ruvuma aliyejifungua watoto watano kwa wakati mmoja kwa njia ya upasuaji mnamo Mei 25 mwaka huu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma iliyopo mjini Songea na watoto hao kuishi kwa muda wa masaa kumi kabla hawajafariki dunia ameruhusiwa kutoka hospitalini hapo.

Akizungumza na Demashonews kwa njia ya simu Sophia Mgaya akiwa nyumbani kwake Ruhuwiko mjini Songea alisema alilazimika kuomba kutoka wodini kwa sababu alikuwa akijisikia uchungu anapowaona wanawake wenzake wodini humo wakiwakumbatia watoto wao baada ya kujifungua huku wa kwake wote wakiwa wamefariki dunia baada ya kuzaliwa. 

Alisema kuwa muda wote aliokuwa hospitalini hapo baada ya watoto wake kufariki huku akiwa bado anauguza kidonda cha upasuaji aliofanyiwa alikuwa akilia muda wote anapowaona wanawake wenzake waliojifungua wakiwakumbatia na kuwanyonyesha watoto wao hivyo akaamua kuomba aruhusiwe kutoka hospitalini hapo. 

 ‘’Niliomba kuruhusiwa kutoka hospitali na kwenda kujiuguza kidonda nyumbani kwa sababu ya uchungu na majonzi niiiyokuwa nikiyapata wodini hapo ninapowaona wanawake wenzangu waliojifungua wakiwakumbatia na kuwanyonyesha watoto wao huku wa kwangu wakiwa wameshazikwa”alisema Bi.Mgaya 

Aidha aliushukuru uongozi wa hospitali hiyo pamoja na wafanyakazi wote kwa namna walivyomuhudumia yeye pamoja na watoto wake watano waliozaliwa na kuishi kwa muda wa masaa ya kumi ambapo alisema kuwa yote yaliyotokea anaamini kuwa ni mapenzi ya Mungu.

Mganga Mkuu mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma Dkt.Benedict Ngaiza akizungumza na mwandishi wetu  kwa njia ya simu kuwa waliamua kuridhia ombi la mama huyo kuondoka hospitalini hapo baada ya kujiridhisha kuwa anaendelea vizuri kwa sababu walifanya kila walichoweza kukoa uhai wake na watoto lakini watoto walifariki baada ya masaa kumi. 

Wakizungumza baadhi ya wananchi waliomshuhudia mama huyo na watoto wake baada ya kuzaliwa na  kabla hawajafariki walisema kuwa kuna kila sababu kwa kila mwenye uwezo wa kumsaidia mama huyo kwa namna yoyote afanye hivyo
Bi.Marietha Ngonyani na Lusi Haule wakazi wa mjini Songea waliwaomba wananchi mbali mbali kujitolea kumsaidia mama huyo kwa sababu bado anauguza kidonda cha upasuaji aliofanyiwa na pia tukio hilo limemuathiri kisaikolojia pia hivyo anahitaji faraja. 
  KWA HISANI YA Demashonews

TANGAZO LA MAUZO YA NYUMBA ZA MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA (PSPF)


MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA
(PSPF)
 


MAUZO YA NYUMBA ZA PSPF
Mfuko unapenda kuwataarifu wananchi wote kwamba inauza nyumba zilizojengwa na Mfuko katika mikoa ya Dar es Salaam- Ilala (Buyuni), Morogoro (Lukobe), Tabora (Usule), Mtwara (Mang’amba) na Shinyanga (Ibadakuli).
Bei ya nyumba ni kati ya Tsh 59,000,000.00 hadi Tsh 80,000,000.00 (Bila ya VAT) kulingana na ukubwa wa nyumba na Mkoa nyumba ilipo.   Ukubwa wa nyumba ni kuanzia vyumba viwili hadi vinne. Fomu zinapatikana kwa gharama ya shilingi elfu tano (TShs. 5,000/=) kwenye ofisi za Mfuko zilizopo mikoa yote nchini.
Waombaji wanaohitaji kuona na kukagua nyumba wawasiliane na Mfuko kupitia namba 2120912/52 au 2127376.
“PSPF - Tulizo la Wastaafu”
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Mkurugenzi Mkuu,
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF),
Golden Jubilee Towers,
Front Tower – Ghorofa ya 6-13,
Mtaa wa Ohio/Kibo,
S. L. P. 4843,
DAR ES SALAAM.
Barua Pepe: pspf@pspf-tz.org          


 Tovuti: www.pspf-tz.org  

PSPF YAFUNGUA OFISI ZAO NJOMBE NA KATAVI

PSPF YAGUNGUA OFISI ZAO NJOMBE NA KATAVI





HII MBAYA SANA; UKATILI KWA WATOTO KAMA HUU UTAISHA LINI? shuhudia hapa




Mkono wa Fikiri Haus 13 
uliounguzwa unavyo onekana 
kwa karibu huo ni ukatiri ulio kithiri


Mtoto Fikili Hausi Mwanafunzi 
wa Darasa la Tatu Shule ya
 Msingi ya Majengo Mansipaa
 ya Songea akiwa amelazwa 
Hospitali ya Mkoa baada ya
 Kunguzwa Moto na Mama yake.



Jeshi la Police lina endelea 
kumtafuta mama yake Fikili Hausi

Msomaji hebu angalia Jamii ya
 watanzania kila siku inafanya
 makongamano ya kuzuia vitendo 
vya ukatili dhidi ya watoto na 
mama, je kitendo kama hiki
 watanzania tunaenda wapi 
na hikiwa watoto ndio Taifa la kesho?

Picha na hisia za Mwananchi Blog


MAKUBWA HAYA: MTOTO MCHANGA WA SIKU 4 AKAA SIKU SITA NDANI YA SHIMO AKIWA HAI



 Ndugu yangu ukishangaa ya Mussa basi shangaa na ya Filauni, Methali hiii methibitika Songea baada ya Mtoto Bahati Upendo mwenye siku 3 toka azaliwe alipo wekwa na mama yake kwenye mfuko wa mbolea na kutumbukizwa kwenye shimo, Ndani ya shimo hilo amekaa siku 6 bila kula wala kunywa hadi alipo okotwa na wasamalia wema, Hivi sasa yuko Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma akiwa Salama  Salimini Yeyote Mwenyenafasi ya kusaidia mtoto huyu anaweza kwenda moja kwa moja Hospitali au wasiliana na namba zifuatayo mchango  utafwatwa 0755061588 au 0755 731 234.
Dawati la Police Wanawake Mkoa wa Ruvuma wakiwa na Wauguzi kuangalia usalama wa Mtoto huyo aliye Tupwa. Kutoka kulia ni Muguzi Rukia Twahili anaye fuata Devota Umbela na aliye mshika mtoto Mwenyekiti wa Mtandao wa Police Wanawake Fadhila Chacha na wa mwisho kushoto ni A nna Chaima 
SOURCE  demashonews.blogspot.com
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa