Home » » JESHI LA POLISI SONGEA LAKAMATA MENO 18 TEMBO NA NOTI BANDIA

JESHI LA POLISI SONGEA LAKAMATA MENO 18 TEMBO NA NOTI BANDIA



Kamanda wa Polisi Mkoa wa 
Ruvuma Deudedit Nsimeki
 akiwa ameshika noti za bandia 
ambazo zilikamatwa wakati wa 
kuuza mahindi katika soko la 
Sodeko Manispaa ya Songea
Haya  ndio meno ya tembo 
ambayo yamekamatwa katika 
kijijicha Hanga yakiwa meno
 18 ambayo yalikuwa 
yakisafirishwa kwenda Dar es salaam
Kweli watu  hawana huruma
 hayo ni meno ya tembo
 wadogo ambao walikuwa 
wakitegemewa kuwa watakuwa
 rasilimali ya taifa lakini
 masikini wawindaji haramu
 wamekatisha maisha ya tembo hao
Noti bandia zilizokamatwa 
Manispaa ya Songea katika
 soko la Sodeko, kwa mujibu wa
 kamanda wa Police Mkoa wa Ruvuma 
Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma 
limefanikiwa kukamata Vipande
18 vya Meno ya Tembo vikiwa 
kwenye Mfuko wa Salfeti. 
Kamanda wa Polisi Mkoa 
wa Ruvuma Deusdedit Nsmeki 
amefanikisha kukamatwa kwa meno
 ya Tembo vipande 18 vikiwa 
kwenye Mfuko wa Salfeti maeneo 
ya Hanga Misheni wilaya ya Namtumbo


PICHA NA SONGEA HABARI

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa