
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Jimbo la Peramiho ni eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Songea, maarufu kwa jina la Songea Vijijini. Halmashauri hii inaundwa na kata 19, vijiji 74 na vitongoji 617 na kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 hapa Peramiho kuna wakazi 173,821 wanaume wakiwa 86,548, wanawake 87,273 na kuna wastani wa watu wanne katika kila kaya.
Peramiho ni kati ya majimbo ambayo yalikuwa na vuguvugu la mabadiliko mwaka 1995 kwenye uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi, japokuwa lilikuwa chini ukilinganisha na baadhi...