Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Aidha, imeelezwa kuwa mkoa huo umezalisha tani 689,123 za mahindi
ambalo ni zao la chakula, katika msimu wa mwaka 2014/2015. Uzalishaji
huo ni sawa na ongezeko la asilimia 17.3 ikiwa ni ongezeko la asilimia
6.7 ya mavuno yaliyopatikana katika msimu wa kilimo wa mwaka 2013/2014.
Mkuu wa mkoa huo Said Mwambungu alisema hayo wakati akizungumza mjini
hapa na wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma.
Alihimiza wananchi kutobweteka kutokana na mafanikio hayo badala yake
waongeze juhudi katika uzalishaji hasa katika kilimo.
Aidha alisema kwamba wastani wa pato kwa mtu mmoja limezidi kukua
kutoka Sh 1,913,526 mwaka 2013/2014 hadi kufikia Sh 2,082,167 ambalo ni
ongezeko la asilimia nane kwa mwaka 2014/2015. Mwambungu alisema, kwa
takwimu hizo inaonesha mkoa wa Ruvuma ni mkoa wa tano ukitanguliwa na
mikoa ya Dar es Salaam, Iringa, Kilimanjaro na Arusha.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa alisema lengo ni kushika nafasi ya kwanza ifikapo mwaka 2018.
Alisema, mkoa unaendelea kupiga hatua nzuri katika ukuaji wa uchumi unaoendana na kuboresha maisha ya wananchi wake.
Mwambungu ametoa mwito kwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa
halmashauri kusimamia na kuchukua hatua dhidi ya watu wanaohujumu kazi
za kilimo ili usimamizi wake uende hadi katika ngazi ya kijiji. Alisema
serikali itaendelea kuhakikisha wananchi hususani wakulima wanapata soko
na bei nzuri ya mazao yao.
Chanzo: Gazeti la Habari leo
Chanzo: Gazeti la Habari leo
0 comments:
Post a Comment