Home » » SIMBA YA POKELEWA KAMA MFALME USIKU KATIKA WILAYA YA TUNDURU MKOANI RUVUMA, IKIELEKEA SONGEA MKOANI HUMO KUCHEZA NA MAJI MAJI

SIMBA YA POKELEWA KAMA MFALME USIKU KATIKA WILAYA YA TUNDURU MKOANI RUVUMA, IKIELEKEA SONGEA MKOANI HUMO KUCHEZA NA MAJI MAJI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mashabiki wa Timu ya SIMBA SC wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wakiwa wamejitokeza kwa wingi kuipokea timu yao ikitokea Dar , Mashabiki wa Simba hawakujali kuwa ni usiku walichokiona wao ni kuipokea timu yao kwa furaha , shangwe huku wengine wakiimba aungurumapo simba hucheza nani .....? pamoja na kuiombea ushindi wa nguvu.

Simba inakuja kucheza na Maji Maji ( Wanalizombe) tarehe 04 katika uwanja wa MAJI MAJI uliopo mjini Songea mkoani Ruvuma.

Utakuwa mchezo mkali na wa hatari sana maana simba inahitaji ushindi iweze kurudi juu na kushika msukani huku Maji Maji wakipambana kuhakikisha wanapanda juu zaidi ili waweze kunusurika na kushuka daraja ,

Umati wa mashabiki wa Simba katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma.

Tumekusogezea na VIDEO ya mapokezi ya Simba usiku huo huo katika wilaya ya Tunduru .HABARI KWA HISANI YA www.ruvumatv.com

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa