RTO RUVUMA ABEL SWAI “DEREVA BODABODA VAENI KOFIA NGUMU,ZINGATIENI SHERIA ZA BARABARABI”

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Ruvuma ABEL SWAI amewataka madereva pikipiki maarufu kama bodaboda kuvaa kofia ngumu katika kujinga na ajali za mara kwa mara wawapo barabarani kwa undani wa habari hii , Hii hapa video yake.

DC JUMA HOMERA AFANIKIWA KUANZA UJENZI WA KITUO CHA AFYA NAKAYAYA, TUNDURU.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
AOMBA WANANCHI PAMOJA NA WADAU MBALIMBALI WAMUUNGE MKONO KUFANIKISHA AZMA YAKE

Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mhe. Juma Zuberi Homera ameazisha ujenzi wa kituo cha Afya Nakayaya, lengo la kuanzisha kituo hiki ni kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya wilaya Tunduru huzidiwa na wagonjwa kushindwa kupata matibabu kwa wakati.

Kata ya Nakayaya ipo umbali wa kilomita tano toka Tunduru mjini, kituo hiki kinatarajiwa kuhudumia kata ya Nakayaya, Masonya, Mlingoti na Nandembo/ Tarafa ya Mlingoti na Nampungu pamoja na maeneo ya jirani.

DC Homera alianzisha mchakato huo kwa kutafuta eneo la kujenga kituo na mara baada ya kupata eneo alimtafuta mchora ramani wa kituo cha afya na mara baada ya kupata ramani alitafuta vijana wa kusafisha eneo na hivi sasa mchanga wa kuanzia ujenzi upo eneo la ujenzi.

Jumla ya mifuko mia tatu ya saruji imepatikana, fedha bado zinakusanywa toka kwa wananchi, wafanyabiashara, makundi ya Vijana mbalimbali wa wilaya ya Tunduru,hivyo anawaomba wadau wengine wamuunge mkono.

Jumla ya matofali elfu thelathini zina hitajika ili kukamilisha ujenzi wa kituo hiki cha afya na zoezi la ufyetuaji utaanza hivi karibuni, vikundi mbalimbali vya vijana vinatarajia kuweka kambi ili kufanikisha zoezi hili.

Aidha, Dc Homera amewaomba wananchi wote waungane kufanikishe ujenzi wa kituo cha afya Nakayaya na hivi karibuni atatoa utaratibu wa kujitolea.

"Tunduru Mpya itajengwa na wenye moyo, wananchi wenzangu wa Tunduru nawaomba tuungane kujenga kituo hiki cha afya na hivi karibuni nitatoa utaratibu wa kujitolea kila mmoja Wetu, tumtangulize Mungu mbele tutafanikiwa kwa ushauri namna ya kufanikisha namba zangu ni +255759814088. Tumuuge mkono Rais wetu Mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli katika kuwaletea maendeleo Watanzania nasi kwa upande Wa wana Tunduru tuna wajibika"
Mchoro wa kituo hicho kitakavyoonekana mara baada ya kukamilika.


Muonekano kwa nje itakavyokuwa.

Sehemu mbalimbali ndani ya kituo hicho kitakavyoonekana



VIDEO – WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MRUSHA ,HATARINI KUDONDOKEWA NA KUTA ZA MADARASA TUNDURU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera akimkabidhi mwanafunzi wa Shule ya msingi Mrusha Anna Nathan kwa niaba ya wanafunzi wenzake pesa kiasi cha shilingi elfu hamsini (50,000) kwa ajili ya kununua sukari ya kuweka katika uje wa wanafunzi. (Picha habari na Ruvuma TV ). Wanafunzi wa shule ya msingi Mrusha wilaya ya Tunduru mkoani Tuvuma wapo hatari kudondokewa na kuta za madarasa wanayoseomea kutona na madarasa hayo kuwa na nyufa za muda mrefu, Habari kamili hii hapa video yake.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa