Home » » TUANGALIE FURSA KUTOKA MKOANI RUVUMA: UJUE MTO RUVUMA AMBAO NI CHANZO KIKUBWA CHA MAPATO KWA JAMII INAYOISHI KANDO KANDO YA MTO HUO

TUANGALIE FURSA KUTOKA MKOANI RUVUMA: UJUE MTO RUVUMA AMBAO NI CHANZO KIKUBWA CHA MAPATO KWA JAMII INAYOISHI KANDO KANDO YA MTO HUO


Mto Ruvuma unavyo onekana kwa juu 

 Hawa ni Vijana wa Ruvuma maarufu kwa WAYAO  wakijitifautia ridhiki  katika mto Ruvuma , Kila pikipiki moja huoshwa kwa Shilingi Elfu moja(1000) wanapokuwa wanaosha mafuta husambaa katika maji . Je kwa hali hii kuna matumizi mazuri ya vyanzo vya mto Ruvuma ikiwa  mbele yake watu hutumia maji haya kwa matumizi ya nyumbani(kupikia na kunywa)   Pia mto huu huumwaga maji yake katika Mto RUVUMA
 
Hawa ni akina mama wakifua nguo katika mto huu wa Ruvuma na pembeni kukiwa na mtoto anayechezea maji ,pengine mtoto huyu uwenda akawa anachota kwa mikono yake na kunywa
 Hii ndiyo hali halisi ya chanzo cha  mto Ruvuma ulipo Ruvuma kwa WAYAO ukiwa umeanza kukauka maji kutokana na matumizi mabaya ya vyanzo vya maji kwa kupitisha mifugo kiholela na ulimaji pembezoni mwa mto,

 Bibi(MBUYA) akisuuza nguo baada ya kufua katika mto Ruvuma huku mjukuu wake akitelemka kumfuata ndani ya maji
 Vijana wakiwa kazini kuelekea katika kuvua samaki

Baadhi ya watalii pamoja na watu mbalimbali ambao ni wakazi wa pembezoni mwa mto huo wakitazama mambo mbalimbali pamoja na kununua Samaki

Hapo mwaka 1886, Askofu wa Kanisa la Anglikana, Charles Alan Smythies, alikuwa MZUNGU sio mtu wa Kwanza kuona chanzo cha mto RUVUMA. Inaelezwa kuwa Askofu huyu alifika katika chanzo cha mto Lujenda, naodaiwa kuwa chanzo muhimu cha mto Ruvuma.
Inasemekana kwamba wakati askofu huyo alipokiona chanzo hicho, uvumi ulienea miongoni mwa wenyeji kwamba kwa vile chanzo hicho kilikuwa na MASHETANI basi Askofu Smithies angekufa. Hata hivyo askofu huyo hakufa kama ilivyohofiwa.

Vile vile yafaa kukumbushana hapa kwamba Askofu Charles Allan Smithies ndiye alikuwa askofu wa kwanza wa UMCA (University Mission to Central Africa) – ya Anglikana visiwani ZANZIBAR hapo mwaka 1892
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa