Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa
(Mb) anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Ruvuma kuanzia tarehe 23 -
25 Novemba, 2017.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 22 Novemba 2017 na Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma Christina Mndeme amesema Mheshimiwa Waziri Mkuu atawasili mjini Songea
siku ya Alhamisi tarehe 23 Novemba, 2017 na kupokelewa na viongozi wa Chama na
Serikali katika Uwanja wa ndege Songea majira ya 7.00 mchana.
Baada ya kuwasili atapokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa na ile ya Chama Tawala
Uwanja wa Ndege Songea. Kisha ataelekea Wilaya ya Namtumbo ambapo atafungua
ghala la MIVARF, kuongea na Madiwani na watumishi wa Umma na baadaye
ataongea na wananchi wa Namtumbo kwenye mkutano wa hadhara.
Ijumaa tarehe 24 Novemba, 2017 Mheshimiwa Waziri Mkuu ataendelea na ziara yake
kwa kuongea na wananchi wa kijiji cha Mchomoro kisha ataelekea Wilaya ya Tunduru
ambapo atasalimia na wananchi wa vijiji vya Rahaleo,Milonde na Matemanga akiwa
njiani kuelekea mjini Tunduru.
Aidha, Mheshimiwa Waziri Mkuu atatembelea kituo cha Afya cha Nakayaya, ghala la
kuhifadhia Korosho na kupata taarifa ya Chama Kikuu Cha Ushirika TAMCU.
Jioni Mheshimiwa Waziri Mkuu ataongea na wananchi kwenye mkutano wa hadhara
utakaofanyika mjini Tunduru katika uwanja wa michezo.
Jumamosi tarehe 25 Novemba, 2017 Mheshimiwa Waziri Mkuu atahitimisha ziara yake
mkoani Ruvuma na kurejea Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa Mndeme ametoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Ruvuma
kujitokeza kwa wingi katika mapokezi kuanzia uwanja wa Ndege Songea atakapowasili
Aidha amewaomba wananchi kujitokeza kwenye maeneo yote ambayo Waziri Mkuu
atapita na kwenye mikutano ya hadhara ili wapate fursa nzuri ya kumsikiliza
Mheshimiwa Waziri Mkuu na kupokea maelekezo atakayoyatoa.
0 comments:
Post a Comment