Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amempa mwezi mmoja Ofisa Ardhi wa wilaya ya
Namtumbo Bw. Maurus Yera awe ametafuta ardhi ya kuwafidia wakazi wa
kijiji cha Lwinga wilayani Namtumbo.
Wakazi
hao 21 mwaka 2008 eneo lao lenye ukubwa wa ekari 101 lilitwaliwa na
Serikali kupitia halmashauri ya wilaya hiyo kwa ajili ya kupisha ujenzi
wa shule ya sekondari ya mkoa wa Ruvuma na waliahidiwa kulipwa
fidia.Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana jioni (Alhamisi, Novemba 23,
2017) alipozungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye uwanja wa michezo wa Lwinga akiwa katika ziara yake ya kikazi
mkoani Ruvuma.
Alitoa
agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi hao kupitia
mabango, ambapo walimuomba awatatulie kero hiyo ya madai ya fidia ya
ardhi iliyodumu kwa miaka 10 bila kupatiwa ufumbuzi.Waziri Mkuu alisema
haoni sababu ya Halmashauri hiyo kushindwa kuwafidia wananchi hao sehemu
ya ardhi kwa muda wote huo ukizingatia wilaya hiyo ina hifadhi ya
ardhi.“Nataka wananchi hawa wawe wamelipwa fidia yao ya ardhi kabla ya
siku kuu ya Krismasi ya mwaka huu. Serikali haiko tayari kuona wananchi
wake waliotoa ardhi kupisha maendeleo wakisumbuliwa.”
Waziri
Mkuu alisema Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli
inataka kila mtumishi ahakikishe anatumia taaluma yake vizuri kwa
kuwahudumia wananchi ikiwa ni pamoja na kutatua kero zinazowakabili kwa
wakati.Pia Waziri Mkuu alitoa wito kwa wananchi hao kuhakikisha
hawakubali kutoa rushwa pale wanapohitaji kupata huduma mbalimbali
kutoka kwa watumishi kwa kuwa ni haki yao kuhudumiwa.
Aliwataka
wananchi kuwa na imani na Serikali yao na kuiunga mkono katika
mapambano dhidi ya rushwa kwani vitendo hivyo vinakwamisha shughuli za
maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.Katika hatua nyingine, Waziri
Mkuu amewataka watendaji kuhakikisha miradi wanayosimamia inakuwa na
thamani inayolingana na kiasi cha fedha kilichotolewa na iwapo
watabainika kwenda kinyume hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
“Lazima
kiasi cha fedha kinachotolewa kugharamia mradhi kilingane na thamani ya
mradi husika. Mfano tumetoa sh. milioni 70 kugharamia mradi na kukuta
mradi uliojendwa ni wa sh. milioni 30 aliyeshughulikia ujenzi huo nasi
tutamshughulikia hatutamuacha salama.”Awali, Waziri Mkuu alifungua ghala
la kuhifadhiia mpunga na mchele katika wilaya ya Namtumbo lililojengwa
na MIVARF na kisha alizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo na
kuwataka wafanye kazi kwa bidii na kuzingatia maadili ya utumishi wa
umma.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bibi Christine Mndeme alisema mkoa
huo unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa masoko
kwa mazao ya mahindi na mbaazi, ambapo Waziri Waziri Mkuu alisema sula
hilo linashughulikiwa hivyo wananchi waendelee kuwa na subira.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
iJUMAA, NOVEMBA 24, 2017.
0 comments:
Post a Comment