Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SERIKALI imesema katika siku zijazo haitoruhusu kampuni yoyote isiyosajiliwa katika Soko la Hisa kutolipa kodi na hata kutiliwa shaka kwamba shughuli zifanywazo haziko katika hali ya uwazi.
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema hayo Dar es Salaam na kuongeza kuwa ni vyema wamiliki wa kampuni mbalimbali nchini wakajiandaa kisaikolojia na kuhakikisha kampuni zao zinaandikishwa katika Soko la Hisa ili kuwezesha jamii kutambua kazi wazifanyazo kuwa ni za uwazi na zenye manufaa kwao.
“Kampuni mbalimbali…mtengeneze utaratibu wa kuingia katika Soko la Hisa Tanzania ili kuwezesha wananchi kiuchumi na pia kuondoa dhana kuwa mnaendesha shughuli zenu kwa usiri mkubwa,” alisema Nchemba.
Alisema Taifa linakokwenda si tu halitoruhusu kampuni kutolipa kodi bali hata kutiliwa shaka kwamba zinafanya shughuli zisizokuwa na uwazi. “Ni bora shughuli zenu mnazofanya ziweze kuungwa mkono na Watanzania wote.”
chanzo:Habari Leo
0 comments:
Post a Comment