Naibu
Waziri wa Maji Mh. Amos Makalla akisalimiana na watumishi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya
Namtumbo Bi. Agnes Hokororo.
Naibu
Waziri wa Maji, Mh Amos Makalla amefanya ziara ya kikazi wilaya ya
Namtumbo pamoja na mambo mengine amezindua mradi mkubwa Maji kijiji cha
Mkongo Nakawale ambao watu zaidi ya 4000 wanapata Maji safi.
Aidha
amekagua mradi wa Maji Milonji na ametoa agizo hadi kufikia tarehe 12
mei mwaka huu mkandarasi awe amekamilisha kuchimba kisima kingine baada
kisima cha awali kuwa na Maji machache.
Pia
Mh Makalla amemwagiza Katibu mkuu wizara ya Maji kuunda kikosi kazi cha
watalaam kwenda Namtumbo kufuatilia matumizi ya Fedha kwa miradi ya
Maji wilaya ya Namtumbo.
Naibu
Waziri wa Maji Mh. Amos Makalla akisalimia watumishi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Namtumbo mara baada ya kuwasili Namtumbo kukagua na kuzindua
miradi ya maji wilayani Namtumbo. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa
Wilaya Bi. Agnes Hokororo.
Naibu
waziri wa Maji Mh. Amos Makalla akifungua maji katika moja ya vituo vya
kuchotea maji bara baada ya uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha
Nakawale kilichopo Namtumbo mkoani Ruvuma.
Naibu
Waziri wa Maji Mh. Amos Makalla akiwa na Mbunge wa Namtumbo Mh. Vitta
Kawawa wakiashiria kuzinduliwa kwa mradi wa maji wa kijiji cha Nakawale.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment