
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Muhidin Amri, Songea.
MFUKO wa taifa wa Bima ya Afya(NHIF) umewahimiza wana michezo nchini kuchangamkia fursa ya kujiunga na mpango wa matibabu kupitia mfuko wa afya ya jamii(CHF) na mfuko wa taifa wa Bima ya Afya(NHIF) kwa ajili ya kupata huduma bora za matibabu pindi wanapoumia wakiwa michezoni.
Rai hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF)mkoani Ruvuma Abdiel Mkaro wakati wa Bonanza maalum la kuhamasisha jamii hususana wana michezo kujiunga na mfuko huo...