Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wahandisi
wa Shirika la umeem nchini TANESCO na mkandarasi kutoka kampuni ya m/s
Isolux, wakijadiliana jambo pembezoni mwa moja ya transofa mpya
zilizofungwa kwenye mji wa Madaba Oktoba 11, 2017.
Meneja
wa TANESCO mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Patrick Lwesya, akizungumza na
wahariri kwenye eneo la ujenzi wa kituo kipya cha kupoza na kusambaza
umeme wa kilovolti 220kV/33kV, eneo la Madaba.
Nyumba
zikiwa na madishi ya tv kwenye Halmashauri ya mji wa Madaba mkoani
Ruvuma ambazo bila shaka kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia fedha nyingi
kutokana na matumizi ya jenereta kupata umeme lakini ujio wa umeme wa
TANESCO utapunguza gharama za uendeshaji.
Maendeleo ya ujenzi wa msingi wa kufungia mashine kituo cha Madaba, ukiendelea Oktoba 11, 2017.
Maendeleo ya ujenzi wa msingi wa kufungia mashine kituo cha Madaba, ukiendelea Oktoba 11, 2017.
Mafundi
wa TANESCO kwa kushirikiana na mkandarasi kutoka kampuni ya India ya
Kalpataru, wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa minara ya kupitisha laini za
umeme wa 220kV huko Iboya, Njombe.
Mafundi
wa TANESCO kwa kushirikiana na mkandarasi kutoka kampuni ya India ya
Kalpataru, wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa minara ya kupitisha laini za
umeme wa 220kV huko Iboya, Njombe.
Mafundi
wa TANESCO kwa kushirikiana na mkandarasi kutoka kampuni ya India ya
Kalpataru, wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa minara ya kupitisha laini za
umeme wa 220kV huko Iboya, Njombe.
Mhandisi
kutoka kampuni ya Kalpataru, (kulia), akifafanua jambo kwa wahariri
kwenye eneo la ujenzi wa minara ya kupitisha nyaya za umeme wa 220kV
eneo la Iboya.
Wajariri wakiwa kazini eneo la ujenzi wa kituo kipya cha Madaba.
Mhandisi kutoka kampuni ya Kalpataru, (kulia), akiwatembeza wahariri kwenye eneo la ujenzi wa minara huko Iboya.
Kaimu
Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi, Leila Muhaji, (kulia), na baadhi ya
wahariri wakitembelea eneo la ujenzi wa minara huko Iboya.
Meneja
Mradi wa Makambako-Songea, Mhandisi Didas Lyamuya, akifafanua jambo kwa
waharri kwenye eneo al ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Madaba mkoani
Ruvuma Oktoba 11, 2017.
Mradi
wa Makambako-Songea, umehamasisha ujenzi wa viwanda na ujenzi wa
kiwanda cha kuchakata chai kinachomilikiwa na kampuni ya Uniliver huko
Njombe.
Tayari
eneo la ujenzi wa kiwanda hicho limefikishiwa umeme na TANESCO kama
ambavyo transfoma pozo mpya iliyofungwa na Shirika hilo inavyoonekana
jirani na eneo la ujenzi.
Meneja
Mradi wa Makambako-Songea, Mhandisi Didas Lyamuya, akifafanua jambo kwa
waharri kwenye eneo al ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Madaba mkoani
Ruvuma Oktoba 11, 2017.
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MADABA
WANANCHI
wa Halmashauri ya mji wa Madaba, mkoani Ruvuma, wameipongeza serikali
kwa kuwafikishia umeme kwenye eneo lao ambapo wamesema utabadilisha
maisha yao.
Pongezi
hizo zimetolewa Oktoba 11, 2017, kufuatia kukamilika kwa kazi ya
kujenga njia ya kusafirisha umeme kwenye eneo hilo ikiwa ni pamoja na
kuweka mtandao wa nyaya (wiring), kwenye eneo hilo na kwenye nyumba za wananchi kazi iliyokwenda sambamba na ufungaji wa transofoma pozo.
Kwa
sasa Serikali kupitia Shirika lake la Umeme, TANESCO inatekeleza mradi
mkubwa wa umeme wa Makambako-Songea ambao unahusisha ujenzi wa njia ya
kusafirisha umeme wa msongo wa
kilovolti 220Kv Transmision Lines na usambazaji umeme vijijini (Rural
electrification), katika vijiji vya mkoa wa Njombe na Ruvuma ikiwa ni
pamoja na kujenga vituo viwili vipya vya kupoza umeme, huko Madaba na
Songea na upanuzi wa kituo kingine mjini Makambako.
“Nimefurahi
sana eneo letu kupata umeme, kwa muda mrefu sana tumekuwa tukitegemea
umeme wa solar, sasa nina matumaini makubwa nimeona kazi zinavyoendelea
hapa za kuweka nguzo za umeme, kutandaza nyaya majumbani na kuweka
transofa, na tumeambiwa tukae mkao wa kula kwani umeem utawaka muda
wowote kuanzia hivi sasa.” Anasema Rehema Maluwa, (pichani juu).
Bi
Maluwa, amesema, yeye ni mjasiriamali kwa hivyo ujio wa umeme
utamuwezesha walau kutengeneza askrimu, na hivyo anatatarajia
kujiongezea kipato kwa njia hiyo.Mwananchi
mwingine Bw. Eliudi Msigwa, yeye anategeema umeme huo sio tu
utawaharakishia maendeleo, pia utainua hadhi ya mji wao ambao kwa muda
mrefu umekuwa hauna umeme.
Akizungumzia
hatua iliyofikia hadi sasa katika kuhakikisha umeme unawaka kwenye
Halmashauri hiyo, Meneja wa Mradi wa umeme wa Makambako-Songea, Mhandisi
Didas Lyamuya, amesema, kilichobaki kwa sasa ni kuunganisha umeme
majumbani.
Mwananchi
mwingine Bi.Theresia Justin yeye amefurahishwa na taarifa za ujio wa
umeme kwenye Hamlamshauri yao kwani tangu wapate uhuru hawajawahi kuwa
na umeme, zaidi ya watu wenye uwezo kutumia majenereta na wengine umeme
wa Solar.
“Niwahakikishie
wananchi mwishoni mwa Novemba au mwanzoni mwa Desemba mwaka huu wa
2017, umeme utawaka kwenye Halmashauri ya Mji wa Madaba na wananchi
watasherehekea Krismas wakiwa na umeme, alisema.
Kwa
upande mwingine, kazi ya kujenga minara ya njia ya kusafirisha umeme,
inaendelea kwa kasi ambapo hadi hivi sasa jumla ya minara, (nguzo kubwa)
266 imejengwa kati ya nguzo 710 ambazo zinatarajiwa kujengwa chini ya
mradi huo.
Kwa upande wake Meneja wa TANESCO mkoani Ruvuma, Mhandisi Patrick Lwesya, amewataka
wawekezaji kujenga viwanda vidogo, vya kati na vikubwa kwani
upatikanaji wa umeme kwenye mkoa wake utakuwa wa uhakika na wa kutosha
kutokana na utekeelzaji wa mradi huu unavyokwenda kwa kasi.
"Mradi huu ifikapo Septemba mwakani kwa asilimia 100 utakuwa umekamilika kwa hivyo wananchi wa Halmashauri ya Madaba, Songea, Mbinga na Namtumbo watakuwa na huduma ya umeme wa uhakika na wa kutosha na hivyo niwaombe tu kujiandaa kwa kuanzisha miradi midogo na mikubwa ya viwanda ili kuongeza pato lao na la taifa kwa ujumla." Alsiema Mhandisi Lwesya.
"Mradi huu ifikapo Septemba mwakani kwa asilimia 100 utakuwa umekamilika kwa hivyo wananchi wa Halmashauri ya Madaba, Songea, Mbinga na Namtumbo watakuwa na huduma ya umeme wa uhakika na wa kutosha na hivyo niwaombe tu kujiandaa kwa kuanzisha miradi midogo na mikubwa ya viwanda ili kuongeza pato lao na la taifa kwa ujumla." Alsiema Mhandisi Lwesya.
0 comments:
Post a Comment