Moses Machali akimnadi Dkt Damas Ndumbaro |
Wakati
kampeni za kuelekea uchaguzi mdogo wa jimbo la Songea mjini mkoani
Ruvuma zikiendelea katika kata mbalimbali za manisipaa ya Songea mkoani
Ruvuma kwa ajili ya kumpata mbunge wa jimbo hilo ambaye chama cha
mapinduzi kimemteua Dkt Damas Ndumbaro kupeperusha bendera ya chama
hicho waliokuwa viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani nchini
wamezidi kujitokeza kwenye kampeni hizo na kutangaza kuachana na vyama
vyao vya awali.
Miongoni
mwa viongozi hao wa vyama vya upinzani ni pamoja na waliokuwa wajumbe
watatu wa serikali ya mtaa wa Majengo mjini Songea kwa tiketi ya chama
cha demokrasia na maendeleo ambao walitangaza uamuzi huo wa kukihama
chao hicho na kujiunga na chama cha Mapinduzi baada ya hotuba ya siku
mbili mfululizo kwenye kampeni hizo za kumnadi mgombea ubunge wa jimbo
hilo kwa tiketi ya chama cha mapinduzi iliyotolewa na aliyewahi kuwa
mwanachama wa chama na kingozi pia cha Demokrasia na maendeleo Moses
Machali.
Katika
hotuba yake ya kumnhadi mgombea huyo Machali alieleza sifa alizo nazo
mgombea Dkt Damas Ndumbaro ambazo alizifahamu muda mrefu tangu akiwa
kwenye kambi ya upinzani ambazo alisema hazina mashaka yoyote ya
kumfanya asichaguliwe kuwa mwakilishi wa wananchi wa jimbo hilo na
kuwataka wananchi wa jimbo la Songea mjini kwa ujumla kuitokeza kwa
wingi siku ya Januari 13 mwaka huu kumpigia kura mgombea huyo na kuacha
kuendelea kusikiliza na kufuata propaganda za wagombea wa vyama vya
upinzani ambao walio wengi hawajui kilichoko kwenye vyama hivyo vya
upinzani kwa sababu yeye alikuwepo huko na anajua kulivyo.
Viongozi
wengine wa kambi ya upinzani waliopanda jukwaani katika viwanja vya
mikutano vya Majengo na kutangaza kujiunga na chama cha mapinduzi ni
pamoja na aliyekuwa katibu wa chama cha ACT Wazalendo mkoa wa Kigoma
Sharon Msanya ambaye kabla ya kutangaza kujiunga na chama cha mapinduzi
aliwataka wapiga kura wa jimbno la Songea mjini kutokuthubutu kulifanya
jimbo hilo kuwa kambiya upinzani kwa sababu kufanya ni kurudisha nyuma
jitihada za serikali za kuwaletea wananchi maendeleo ambayo
wameyahityaji kwa muda mrefu kurtoka serikalini na serikali ya awamu ya
tano inaendelea kuonesha dhamira ya dhati kuwafikishia wananchi
maendeleo hayo.
Alisema
yeye amekuwa kiongozi mkubwa wa chama cha ACT Wazalendo katika ngazi ya
mkoa lwa Kigoma akini amefikia uamuzi huo wa kusafiri kutoka mkoani
Kigoma mpaka mjini Songea ili aweze kupata fursa ya kuwaeleza wananchi
wa Songea umuhimu wa kukiunga mkono chama cha mapinduzi na mgombea wake
Dkt Dams Ndumbaro kwa ajili ya maendeleo yao na taifa kwa ujumla kwa
sababu mgombea huyo amekuwa mpigania maendeleo ya taifa kwa muda mrefu
hata kabla hajafikia uamuzi huo wa kugombea nafasi hiyo ya kuwawakilisha
wananchi wa jimbo lake.
Huku
naye Edna Sunga aliyekuwa katibu wa kamati ya maendeleo ya jamii taifa
na mjumbe wa kamati kuu na halmashauri kuu taifa wa chama cha ACT
Wazalendo akizungumza baada ya kukihama chama hico na kujijnga na chama
cha mapinduzi amesema kwa sababu yeye ni muumini wa kuzingatia miiko na
vita dhidi ya rushwa na kuwaletea maendeleo wananchi ameona hana sababu
ya kuendelea kuwa kwenye upinzani badala ya kuongeza na kujnganisha
nguvu ya kuwajhudumia wananchi walio wengi.
Amesema
kiongozi au mwananchi yeyote mwenye dhamira ya dhati ya maendeleo
ambayo wananchi walio wengi wanayahitajihana budi kukiunga mkopno chama
cha mapinduzi na mgombea wake ambaye amevaa taswira ya chama hicho na
taifa kwa ujumla huku naye mgombea wa jimbo hilo kwenye uchaguzi huo
akiendelea kuwaomba wananchi wa mji wa Songea kujiktokeza kwa wingi siku
hiyo ya uchaguzi kwa ajili ya kupiga kura kwa chama cha mapinduzi.
Na Nathan Mtega, Jamvi la habari - Songea
0 comments:
Post a Comment