Waziri
wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ametembelea maeneo mawili
anayotarajiwa kuwekewa jiwe la msingi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa tarehe 7/01/2018 katika wilaya
ya Songea mkoani Ruvuma.
Mradi wa kwanza aliotembelea ni wa jengo la Tanesco Mkoa wa Ruvuma lililoanza kujengwa mnamo mwaka 2014 ambao ulitarajiwa kukamilika mwishaoni mwa mwaka jana na kushindikana kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa Mkandarasi.
Aidha mradi wa jengo hilo unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili mwaka huu na kuanza kutumika rasmi.
Pamoja na kutembelea jengo hilo la Ofisi ya Tanesco Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Kalemani alitembelea eneo kunakojengwa mitambo ya kupoozea umeme katika mradi mkubwa wa kusafirisha umeme wa Makambako Songea uliopo wilayani Songea mkoani Ruvuma ambako alijadiliana na wataalamu na kuweka baadhi ya vitu sawa tayari kwa ajili ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kuweka jiwe la msingi.
Meneja wa Mradi Mkubwa wa Usafirishaji wa Umeme wa Makambako - Songea
Mhandisi Didas Lyamulya akitoa maelezo ya mradi kwa Waziri wa Nishati
Dkt. Medard Kalemani alipotembelea eneo la ujenzi wa mitambo ya kupoozea
umeme unaoendelea kujengwa wilayani Songea mkoani Ruvuma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirirka la Umeme Tanzania (Tanesco) akieleza
jambo mbele ya wajumbe walioambatana na Waziri wa Nishati ili kukagua
eneo litakalowekwa jiwe la msingi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika
eneo la ujenzi wa Mitambo ya Kupoozea Umeme katika mradi wa Kusafirisha
umeme wa Makambako Songea.
Waziri
wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (wa kwanza kushoto ) akikagua maendeleo
ya ujenzi wa kituo cha kupoozea umeme katika mradi wa Kusafirisha Umeme
wa Makambako-Songea wilayani Songea tayari kwa ajili ya kuwekwa kwa
jiwe la msingi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kesho Tarehe 7/01/2018.
Waziri
wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Umeme Tanzania Dkt. Tito Mwinuka akimweleza jambo
walipotembelea eneo la uzinduzi wa mradi wa kusafirisha umeme wa
Makambako-Songea ili kujionea maandalizi ya uzinduzi huo.
Mradi wa kwanza aliotembelea ni wa jengo la Tanesco Mkoa wa Ruvuma lililoanza kujengwa mnamo mwaka 2014 ambao ulitarajiwa kukamilika mwishaoni mwa mwaka jana na kushindikana kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa Mkandarasi.
Aidha mradi wa jengo hilo unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili mwaka huu na kuanza kutumika rasmi.
Pamoja na kutembelea jengo hilo la Ofisi ya Tanesco Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Kalemani alitembelea eneo kunakojengwa mitambo ya kupoozea umeme katika mradi mkubwa wa kusafirisha umeme wa Makambako Songea uliopo wilayani Songea mkoani Ruvuma ambako alijadiliana na wataalamu na kuweka baadhi ya vitu sawa tayari kwa ajili ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kuweka jiwe la msingi.
0 comments:
Post a Comment