Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Ruvuma zaendelea

Afisa Tawala wa Wilaya ya Nyasa,Hapiness Msanga (kushoto) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma,Idd Mponda kwa ajili ya kukimbizwa katika wilaya hiyo.
Mkulima maarufu wa kahawa Wilayani Mbinga,Gotam Haule (kushoto) akimuonesha mche wa zao hilo kiongozi wa mbio za mwenge,Kapt. Honest Mwanossa
Wakimbiza mwenge wa uhuru wakicheza baada ya kumaliza mbio za mwenge katika Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma katika viwanja vya michezo vya Mbambabay.kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbinga,Idd mponda.
Picha na Muhidin Amri.

MWENGE WA UHURU WAANZA MBIO ZAKE MKOANI RUVUMA


Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Severin Tossi(kushoto) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Njombe John Mahali .Mwenge wa Uhuru umepokelewa leo mkoani Ruvuma katika kijiji cha Ngelenge wilaya ya Ludewa kabla haujaanza mbio zake mkoani Ruvuma.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2012 Kapt.Honest E.Mwanossa akimsaidia kubeba ndoo ya maji Bi .Hilda Ngoya mkazi wa kijiji cha Nkaya wilaya ya Nyasa mara baada ya kiongozi huyo kuzindua kisima cha maji kilichoghalimu Tsh 14.9 milioni.Mwenge wa Uhuru utakuwepo mkoani Ruvuma kwa siku sita.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kapt.Honest E.Mwanossa akifungua jengo la hosteli ya wasichana katika shule ya sekondari ya Mbambabay wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.Picha na Muhidin Amri wa Globu Jamii,Ruvuma.
Picha na Blog ya Issa Michuzi

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma awaapisha wakuu wapya wa Wilaya mkoani humo

Mkuu wa Wilaya mpya ya Nyasa mkoani Ruvuma,Mh. Ernest Kahindi akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu wa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo katika viwanja vya Ikulu ndogo mjini Songea
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma,Mh. Abdul Lutavi akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu wa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo katika viwanja vya Ikulu ndogo mjini Songea.Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa huo,Sevelin Tossi.
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mh. Joseph Mkirikiti akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu wa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo katika viwanja vya Ikulu ndogo mjini Songea.Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa huo,Sevelin Tossi.
Mkuu wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma,Mh. Senyi Simon Ngaga akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu wa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo katika viwanja vya Ikulu ndogo mjini Songea.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu (kushoto) akimuongoza Mkuu mpya wa Wilaya ya Tunduru mkoani humo,Mh. Chande Bakari Nalicho kushika nafsi hiyo kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete kwa baadhi ya wakuu hao wa wilaya hapa nchini wiki iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wapya wa wilaya za mkoa huo baada ya kuwaapishwa katika viwanja vya ikulu ndogo mjini songea.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Mwambungu (kushoto) akiteta jambo na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbinga,Kanal mstaafu Edmund Mjengwa (katikati) na Mkuu Mpya wa Wilaya hiyo,Mh. Senyi Ngaga.
Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Shrika la Umeme nchini,Boniface Njombe (kushoto) akimsikiliza aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma,Kanal mstaafu Edmund Mjengwa, katika viwanja vya ikulu ndogo mjini Songea kabla ya kuanza kwa shughuli za kuwaapisha wakuu wapya wa wilaya.
Mwanasiasa mkongwe nchini,Alhaji Mustafa Songambele akizungumza na wakuu wa wapya wa wilaya za mkoa huo (hawapo pichani) baada ya kuapishwa katika viwanja vya ikulu ndogo mjini songea.
Picha ya Pamoja.Picha na Muhidin Amri wa Globu ya Jamii.
PICHA KWA HISANI YA MICHUZI BLOG

Uhaba wa Vyumba vya Madarasa ni Kero Kwa Wanafunzi na Walimu Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma


SHULE YA MSINGI SELOU.
WANAFUNZI WA MADARASA YA AWALI SHULE YA MSINGI RWINGA - WILAYANI NAMTUMBO
Mwalimu wa darasa la awali Fransis Ndunguru shule ya Rwinga Namtumbo
MOJAWAPO YA MDARASA YA SHULE YA MSINGI SELOUS ILIYOKO WILAYANI NAMTUMBO.

 MWALIMU MKUU WA SHULE YA MSINGI KIDUGALO-Owini Mpangala (NAMTUMBO).
--

Uhaba wa vyumba vya madarasa ni moja ya changamoto kuu inayoikabili sekta ya elimu wilayani Namtumbo mkoani ruvuma hali inayopelekea kushuka kwa kiwango cha elimu wilayani humo.Baadhi ya walimu wanaofundisha katika shule za msingi wilayani namtumbo wamesema wanatamani kuacha kazi au kuhama kutoka shule hizo kutokana na changamoto nyingi ambazo hazijapatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu na kuchangia kushusha elimu katika shule nyingi ambazo zipo mjini.



Katika shule za msingi Rwinga,Selou,Mkapa na Kidugalo zote zikiwa kata ya Rwinga zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa vyumba vya madarasa hali inayowalazimu walimu kujenga vibanda vya nyasi ili kuwaepusha wanafunzi kutokukosa masomo yao kwa sababu ya uhaba wa madarasa.



Ukosefu wa madarasa pia umewapelekea walimu kuamua kutumia vyumba vichache vilivyopo kwa kuwachanganya wanafunzi wa madarasa mawili katika chumba kimoja hali inayotia shaka mazingira ya kujifunzia.



katika shule ya msingi Kidugalo, zaidi ya wanafunzi 200 kuanzia darasa la tatu mpaka la sita wanasoma katika vyumba viwili vya madarasa kwa kugeuziana migongo hali ambayo inachangia kushusha taaluma katika shule hiyo.Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo ina shule za msingi 107 kati ya hizo shule 105 zinamilikiwa na serikali na shule mbili ni za watu binafsi na mashirika ya dini.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa