SHULE YA MSINGI SELOU.
WANAFUNZI WA MADARASA YA AWALI SHULE YA MSINGI RWINGA - WILAYANI NAMTUMBO
Mwalimu wa darasa la awali Fransis Ndunguru shule ya Rwinga Namtumbo
MOJAWAPO YA MDARASA YA SHULE YA MSINGI SELOUS ILIYOKO WILAYANI NAMTUMBO.
MWALIMU MKUU WA SHULE YA MSINGI KIDUGALO-Owini Mpangala (NAMTUMBO).
--
Uhaba wa vyumba vya madarasa ni moja ya changamoto kuu inayoikabili sekta ya elimu wilayani Namtumbo mkoani ruvuma hali inayopelekea kushuka kwa kiwango cha elimu wilayani humo.Baadhi ya walimu wanaofundisha katika shule za msingi wilayani namtumbo wamesema wanatamani kuacha kazi au kuhama kutoka shule hizo kutokana na changamoto nyingi ambazo hazijapatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu na kuchangia kushusha elimu katika shule nyingi ambazo zipo mjini.
Katika shule za msingi Rwinga,Selou,Mkapa na Kidugalo zote zikiwa kata ya Rwinga zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa vyumba vya madarasa hali inayowalazimu walimu kujenga vibanda vya nyasi ili kuwaepusha wanafunzi kutokukosa masomo yao kwa sababu ya uhaba wa madarasa.
Ukosefu wa madarasa pia umewapelekea walimu kuamua kutumia vyumba vichache vilivyopo kwa kuwachanganya wanafunzi wa madarasa mawili katika chumba kimoja hali inayotia shaka mazingira ya kujifunzia.
katika shule ya msingi Kidugalo, zaidi ya wanafunzi 200 kuanzia darasa la tatu mpaka la sita wanasoma katika vyumba viwili vya madarasa kwa kugeuziana migongo hali ambayo inachangia kushusha taaluma katika shule hiyo.Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo ina shule za msingi 107 kati ya hizo shule 105 zinamilikiwa na serikali na shule mbili ni za watu binafsi na mashirika ya dini.
0 comments:
Post a Comment