Ripoti: Wazee hawapati huduma za afya bure
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mwandishi wa vitabu, Pearl Buck aliwahi kuandika “jamii lazima
ihakikishe inatengeneza mazingira mazuri kwa wazee ili kila anayefikia
hatua hiyo ya maisha asijione tofauti na watu wa rika jingine, kwa
sababu ni hatua ambayo kila mwanadamu ataifikia iwapo hatafariki dunia
mapema”.
Fikra kama hizo ndizo zimefanya nchi nyingi
kutengeneza mifumo ambayo inawawezesha wazee waishi maisha mazuri ambayo
yanawafanya kutojisikia kunyanyapaliwa.
Hivi karibuni taasisi isiyo ya kiserikali nchini,
Twaweza ilifanya utafiti ambao ulibainisha kuwa ni mtu mmoja tu kati ya
watu 20 wenye umri zaidi ya miaka 60 ambaye hupata huduma za afya na
matibabu bila kulipa gharama zozote kwenye vituo vya afya nchini.
Siyo kwamba hawaitaki huduma hiyo, bali mazingira
ya upatikanaji wa huduma hizo siyo rafiki na hivyo kuwafanya wazee wenye
uwezo kidogo wakimbilie katika hospitali za binafsi na wale wengine
kubaki wakisubiri miujiza itokee.
Jitihada za serikali kuimarisha sekta ya afya
zimeendelea kupambana na vikwazo baada ya kubainika kuwa kuna baadhi ya
vituo vya afya ambavyo vinatoza fedha kwa wazee na watoto wakati wa
kutoa huduma hizo jambo ambalo ni kinyume na sera ya afya ya wazee na
watoto.
Idadi hiyo ni sawa na asilimia 6 tu ya watu wanaozidi umri huo, kwa maana ya wazee wanaofadika na huduma za bure.
Mbali na kundi hilo kuonekana kunyimwa haki yao ya
msingi, utafiti huo pia ulifanywa kwa kundi jingine ambalo ni la watoto
walio na umri chini ya miaka mitano. Kwenye kundi hilo imebainika kuwa
ni mtoto mmoja kati ya watano mwenye umri chini ya miaka hiyo, ambaye
hupata huduma za afya na matibabu bure. Idadi hiyo ni sawa na asilimia
18 tu ya watoto wanaofaidika na huduma hizo.
Mtafiti kutoka taasisi hiyo, Elvis Mushi anasema
kuwa kutokana na mambo yanayotendeka kwenye vituo hivyo vya afya na
matokeo waliyoyapata, ni dhahiri kuwa makundi hayo mawili yanayotakiwa
kupata haki yao ya msingi hayatendewi haki.
“Wagonjwa wananyimwa haki zao za kupata huduma za
afya kikamilifu kama inavyotakiwa. Inafahamika fika kuwa wanatakiwa
kupewa huduma hizo bila malipo, halafu bado wanatozwa fedha. Hiyo si
sawa,” anasema Mushi.
Mtafiti huyo anasema kuwa huenda wagonjwa wengine
wakawa wanateseka kwa kuugulia nyumbani kutokana na ukweli kwamba hawana
fedha za kulipia huduma za afya.
Hata hivyo, Mushi anatoa tahadhari kuwa kutokana
na usimaminzi mbovu wa Serikali juu ya huduma zinazotolewa kwenye vituo
vingi vya afya vilivyopo chini yake, huenda ikawa sababu kubwa
inayochangia wananchi wengi kuvisusia vituo hivyo.
“Kutoridhika na usimamizi wa Serikali kwenye
huduma za afya kunaweza pia kusababisha wananchi kutopendelea kwenda
kupata matibabu na huduma katika vituo vya afya,” anasema Mushi.
Utafiti huo uliofanywa kati ya Mei na Juni 2013 ukiwa na lengo
la kubaini iwapo vituo vya afya vipo kwa ajili ya kuwahudumia watu na
uliojumuisha zaidi ya nusu ya watu (asilimia 57) waliotembelea vituo vya
afya kwa dhumuni la kutibiwa au kumsindikiza mgonjwa, ulibaini kuwa
wagonjwa kutoka kwenye makundi hayo mawili huwa wanatozwa fedha kinyume
na mpango uliowekwa na Serikali.
Mpango wa Serikali ni kutoa bure huduma za afya
kwa makundi hayo mawili, lakini dhumuni hilo linaonekana kuendeshwa
kinyume na baadhi ya vituo vya afya vinavyotoa huduma hizo nchini.
Mratibu wa mradi wa wazee wa shirika la Helpage
International, Juliana Bernard anasema zipo sababu nyingi zinazowafanya
wazee wasipate huduma stahili pamoja na Serikali kuweka sera inayotoa
mwongozo.
Anasema kama kweli Serikali ina nia ya kuhakikisha
wazee wanapata huduma hizo bila usumbufu wowote, iweke vipaumbele
ikiwemo kuwawekea waangalizi maalumu angalau katika kila hospitali
kadhaa nchi nzima.
“Ni kweli Serikali inaonekana kuwa na nia ya
kuwasaidia wazee, lakini kwa hali halisi ya hospitali zetu, siyo rahisi
kwa sababu wauguzi na madaktari wengi hawana weledi. Wanadharau wazee.
Kama wangekuwa na madaktari wao au na wodi zao maalumu pengine hali
ingekuwa tofauti,” anasema Juliana.
Anaongeza kuwa Serikali iongeze bajeti katika
huduma za afya ambayo itawezesha wazee kupata huduma zao ikiwemo hiyo ya
kuwawekea wauguzi na madaktari wao.
“Wakati mwingine hata daktari hampimi mzee
akijiaminisha kuwa haumwi bali uzee unamsumbua. Watoa dawa nao huwanyima
dawa wazee, hali ambayo imewavunja moyo na kuwafanya wengine waamue
kufia majumbani mwao,” anasema Juliana.
Sera ya Afya inasemaje?
Sera rasmi ya Afya ilitayarishwa na kupitishwa
mwaka 1990 inasema kuwa msisitizo wa sera hiyo ulikuwa ni kuinua hali ya
afya kwa wananchi wote na kipaumbele kilitolewa kwa makundi yaliyo
katika hatari zaidi ya kuugua. Sera hiyo inafafanua kati ya makundi
ambayo yamepewa kipaumbele ni watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Watoto wanatakiwa kupewa huduma ya afya bila malipo.
Sera hiyo ya mwaka 2003 inaweka wazi kuwa umri wa
miaka 60 ndio unaozingatiwa kuwa kigezo cha uzee ni umri wa miaka 60 na
kuendelea.
Katika kipengele cha huduma ya afya kwa wazee,
sera inasema kuwa kutokana na umri huo wengi wao huwa na magonjwa ya
mara kwa mara na ya muda mrefu, hali ambayo ni ya kawaida katika kipindi
hicho cha maisha ya biandamu.
Hali hiyo inahitaji uangalizi na matunzo maalum ya
kitaalamu hivyo kutokana na hilo huduma za afya kwa wazee zitakuwa
zikitolewa bure.
Pamoja na ukweli huo, huduma za afya hazipatikani kwa urahisi
kwa wazee walio wengi na mara nyingi ni ghali na kuwa utaratibu wa kutoa
huduma bure kwa wazee, bado una upungufu, inasema sera hiyo.
Pia inaeleza kuwa kutakuwa na utaratibu wa kutoa
mafunzo kwa watumishi ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wazee na namna
ambavyo wanapaswa kuhudumiwa tofauti na makundi mengine.
Jambo hilo linaungwa mkono na mkuu wa Twaweza,
Rakesh Rajani ambaye anasema kuwa licha ya kuwa na sera hizo, bado kuna
changamoto lukuki zinazozikabili.
Rajani anasema hakuna utekelezaji mzuri wa sera
hizo ambazo malengo yake ni mazuri kwa kuwa wagonjwa kutoka kwenye
makundi hayo mawili wanaendelea kuteseka bila sababu za msingi.
“Wazee na watoto wanaumia kwa sababu hizo sera
zilizowekwa hazitekelezwi. Kungekuwa kuna ufualiliaji na usimamizi
mzuri, labda haya yote yasingetokea,” anasema Rajani.
Mkuu huyo anasema kuwa sera hizo zimebaki kuwa
maneno yaliyoko kwenye maandishi tu, lakini ufuatiliaji wake ni
hafifu.“Serikali inahitaji kutimiza ahadi zake za kufuatilia
utekelezaji, kuwatunuku wanaotoa huduma nzuri, na kuwawajibisha wale
wanaotoa huduma duni. Vinginevyo Serikali itapoteza uaminifu wake na
watu maskini wataendelea kuteseka,” anasema Rajani.
Wizara ya Afya yakemea
Naibu Waziri wa Afya, Dk Kebwe Steven anasema kuwa
sera ya afya inaweka wazi kuwa kuna makundi maalum yanayotakiwa kupewa
huduma za afya bure kutokana na mahitaji yao, likiwamo kundi la watoto
wenye umri chini ya miaka mitano na wazee walio na umri wa kuanzia miaka
60.
Steven anafafanua kuwa mbali na makundi hayo
mawili ya watoto na wazee kuna makundi mengine pia yanayopaswa kupata
huduma za afya bila kutozwa gharama za matibabu. “Magonjwa ya kudumu
kama pumu, kifua kikuu, Ukimwi na magonjwa mengine yaliyoainishwa kwenye
sera pamoja na wale wasiona na wasio na uwezo kwa maana ya wenye kipato
kidogo, wanatakiwa kupata huduma za afya bure,” anabainisha Waziri
Kebwe.
Anasisitiza kuwa hivyo ndivyo sera inavyoeleza na
kwamba kinyume na hapo ni ukiukwaji wa matakwa yaliyowekwa na serikali
chini ya sera hiyo.
“Tuliweka sera kwa madhumuni maalum lakini
ikitokea kwenye badhi ya vituo vya umma wanatoza fedha kwa wagonjwa
kutoka kwenye makundi hayo, tutachukua hatua kali dhidi yao,”
anasisitiza Waziri Kebwe.
“Tunafahamu kuwa wako baadhi ya watumishi wa umma
ambao si waaminifu na si waadilifu hivyo na ninaahidi kuwa tutakula nao
sahani moja. Kama wizara kamwe hatuwezi kukubaliana na hilo.”
Vilevile Kebwe amekemea vikali kuhusiana na hilo hivyo amewataka viongozi wote kuanzia ngazi ya wilaya hadi taifa wanaohusika na wizara hiyo kushirikiana na wadau wangine wa afya nchi kutoa taarifa juu ya suala hilo ili wizara iweze kuchukua hatua stahiki dhidi ya wahusika.
Chanzo;Mwananchi
Vilevile Kebwe amekemea vikali kuhusiana na hilo hivyo amewataka viongozi wote kuanzia ngazi ya wilaya hadi taifa wanaohusika na wizara hiyo kushirikiana na wadau wangine wa afya nchi kutoa taarifa juu ya suala hilo ili wizara iweze kuchukua hatua stahiki dhidi ya wahusika.
Chanzo;Mwananchi
UKAWA WALALAMIKIA CCM KUTUMIA MALI ZA SERIKALI
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa
Mpango wa kuishtaki CCM kwa Msajili ulitangazwa jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Musoma na viongozi wa Ukawa .
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa, alisema ni ukiukwaji wa sheria kwa chama cha siasa kutumia rasilimali za serikali.
“Hakuna chama cha daraja la pili, sheria inasema vyama visitumie rasilimali za serikali katika shughuli zake za kisiasa, lakini viongozi wa CCM katika ziara zake mikoani inatumia magari ya serikali,” alisema.
Alitoa mfano ziara ya viongozi wa CCM katika mkoa wa Tabora jimbo la Urambo wakiongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana, walitumia magari ya serikali namba STK 667, STK 1627, STK 6826, SM 9284, STK 5144, STK 6929, DFP 6068, DFP 6110, DFP 9284 na STK 6929.
Alisema CCM haistahili kutumia rasilimali za serikali katika shughuli za chama wakati inafahamu kuwa nchi ipo katika mfumo wa vyama vingi
vya siasa na hivyo magari hayo ya serikali yametokana na kodi ya Watanzania wote na siyo ya wananchi ambao ni wanachama wa CCM pekee yake.
Alipoulizwa na NIPASHE, kuhusiana na tuhuma za Ukawa, Kinana alisema Ukawa wameishiwa hoja, wamedharauliwa na sasa wanatapatapa.
SOURCE:
NIPASHE
ASKOFU:HOFU YA MUNGU ITATUPA KATIBA
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu akiongoza watu mbalimbali
kumpongeza Askofu Mkuu mpya wa Jimbo la Songea, Damian Dallu katika
Kanisa la Mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba mjini Songea jana
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea, Damian Dallu
amesema Katiba Mpya itapatikana iwapo wajumbe wa Bunge la Katiba
watakuwa na maadili ya kiroho kwa kufuata maagizo ya Mwenyezi Mungu bila
kupindisha ukweli wa mchakato wa maoni ya Katiba.
Amesema kupotosha ukweli wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba unaweza kuipeleka nchi kubaya.
Hayo aliyasema jana katika Ibada maalumu ya
kumsimika rasmi iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Mtakatifu
Mathias Mulumba lililopo Mjini Songea ambayo ilihudhuriwa na maelfu ya
waumini, viongozi wa chama na Serikali, viongozi wa madhehebu ya dini
pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne
Makinda.
Askofu Dallu alisema wapo watu wanaodhani kuwa
iwapo Katiba Mpya itapatikana matatizo yao yatakwisha kitu ambacho
hakina ukweli kwa madai kuwa hata Katiba iliyopo imeongoza nchi kwa
miaka 50 na watu waliungana kiroho na siyo kwa kupitia makaratasi ambayo
yanaweza kuchakachuliwa.
Alisema Watanzania hawana budi kumwomba Mungu
asaidie kupata viongozi watakaoweza kuliongoza taifa kuanzia ngazi za
chini hadi juu kwa kufuata maadili ili nchi isije ikaiingia kwenye
machafuko.
Akitoa salamu za Mkoa wa Ruvuma Mkuu wa Mkoa, Said
Mwambungu alisema kuwa Serikali itatoa ushirikiano kwa askofu huyo
katika kuunga mkono juhudi na mafanikio yanayofanywa na Kanisa Katoliki
katika kutoa huduma zake kwenye Sekta ya afya, elimu, kilimo na maji.
Alisema mafanikio hayo yamechangiwa na viongozi wa
dini ambao walikuwa wakijituma kwa bidii kusaidia wananchi bila kujali
madhehebu wanayotoka kitu ambacho kimeipa Serikali faraja na inaomba
ushirikiano huo kuendelea.
Spika Makinda akitoa salamu kwa niaba ya Serikali
amewataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii badala ya kuitegemea
Serikali au kanisa kuwaletea maendeleo jambo ambalo linarudisha nyuma
maendeleo binafsi.
Naye Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania,
Tarcisius Ngalalekumtwa amempongeza Askofu Dalu kwa kukubali kushika
nafasi hiyo na kukemea tabia za wizi na mauaji kuwa ni kinyume cha
matendo ambayo hayampendezi Mungu.
Alisema dhamira safi, upendo na wema, upole, ukarimu na rehema ndiyo matunda na zabibu za kumtolea Mwenyezi Mungu
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
MAOMBI YA MIKOPO ELIMU YA JUU 2014/2015 YAFUNGULIWA
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkurugenzi wa Habari,Elimu na Mawasiliano wa HESLB,Cosmas Mwaisobwa
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Cosmas Mwaisobwa, alisema maombi ya mikopo ambayo yanafanyika kwa njia ya mtandao (Olas) yamefunguliwa kuanzia Aprili 23 na yatafungwa rasmi Juni 30, mwaka huu.
Mwaisobwa alisema kuwa Bodi inatarajia kupokea maombi ya mikopo kutoka kwa waombaji wenye sifa zilizoainishwa kwenye mwongozo na vigezo vya utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2014/2015 ambao ulitolewa na Bodi na kutangazwa kupitia magazeti na tovuti yake mwanzoni mwa Aprili, 2014.
Mwongozo huo unataja sifa za msingi za waombaji mikopo kuwa wawe ni wahitimu wa kidato cha sita, Stashahda na cheti cha elimu ya ufundi ((Tvet) hatua ya sita, waliohitimu masomo yao kati ya mwaka 2012 na mwaka 2014 wanaotarajia kujiunga na elimu ya juu na wanaotarajia kuomba mikopo toka Bodi ya Mikopo wanafahamishwa kuwa wanapaswa kutuma maombi yao ndani ya kipindi kilichotajwa hapo juu.
Bodi inatarajia kutoa mikopo kwa wanafunzi takriban 35,000 wa mwaka wa kwanza watakaodahiliwa kujiunga na masomo katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu.
“Pamoja na kupewa fursa ya kuomba mikopo, waombaji wa mikopo wanapaswa kuzingatia masuala ya msingi yanayoambatana na mchakato mzima ikiwa ni pamoja na kusoma kwa umakini mwongozo na vigezo vya utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2014/2015 kabla ya kulipa ada ya maombi na kujaza fomu, kusoma kwa umakini na kujaza vipengele vyote vya fomu kulingana na maelekezo ili kuiwezesha Bodi kupata taarifa sahihi za mwombaji,” alifafanua Mwaisobwa.
Aliongeza kuwa ni muhimu kwa mwombaji mkopo kuambatanisha nyaraka zinazohitajika kama vile cheti cha kuzaliwa, vyeti vya taaluma, vielelezo vya mdhamini na uthibitisho wa nyaraka kutoka kwa mamlaka husika na mwisho kutuma fomu kamili na viambatanisho kwenye Bodi ya Mikopo ili ziweze kupitia kwenye mchakato wa uchambuzi na upangaji wa mikopo kwa wakati.
Aidha, Mwaisobwa alieleza kuwa kuna mabadiliko machache yamefanyika ambapo wanufaika wa mikopo wanaoendelea na masomo hawatakiwi kujaza tena fomu kuthibitisha uhitaji wao wa mikopo kwa mwaka unaofuatia.
CHANZO:
NIPASHE
FAHAMU VIVUTIO VYA UTALII NDANI YA MKOA WA RUVUMA
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wildlife
Ruvuma region has nine game reserves and one game controlled area.
A wide variety of wildlife can be found within these game conservation areas such as hippos, Lions, Zebra, Buffaloes, Wild dogs, Bushbucks and Baboons. The fairly large wildlife areas in the
Wild Animals.
region with a diversity of wildlife species already attract a fair number of tourists. However, these wildlife attractions are yet to be developed in terms of tourist accommodation, camping sites for tourist hunting. Exploration and investing in this sector for tourist development undertakings will be of great importance
Ruvuma region has nine game reserves and one game controlled area.
A wide variety of wildlife can be found within these game conservation areas such as hippos, Lions, Zebra, Buffaloes, Wild dogs, Bushbucks and Baboons. The fairly large wildlife areas in the
Wild Animals.
region with a diversity of wildlife species already attract a fair number of tourists. However, these wildlife attractions are yet to be developed in terms of tourist accommodation, camping sites for tourist hunting. Exploration and investing in this sector for tourist development undertakings will be of great importance