Home » » UKAWA WALALAMIKIA CCM KUTUMIA MALI ZA SERIKALI

UKAWA WALALAMIKIA CCM KUTUMIA MALI ZA SERIKALI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa
Umoja  wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umetishia  kukishtakiwa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  kwa Msajili wa Vyama vya Siasa  kuwa kinatumia rasilimali za serikali katika ziara zake za kichama.
Mpango wa kuishtaki CCM kwa Msajili ulitangazwa jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Musoma na viongozi wa Ukawa .

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa, alisema ni ukiukwaji wa sheria kwa chama cha siasa kutumia rasilimali za serikali.

“Hakuna chama cha daraja la pili, sheria inasema vyama visitumie rasilimali za serikali katika shughuli zake za kisiasa, lakini viongozi wa CCM katika ziara zake mikoani inatumia magari ya serikali,” alisema.

Alitoa mfano ziara ya viongozi wa CCM katika mkoa wa Tabora jimbo  la Urambo wakiongozwa na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana, walitumia magari ya serikali namba STK 667, STK 1627, STK 6826, SM 9284, STK 5144, STK 6929, DFP 6068, DFP 6110, DFP 9284 na STK 6929.

Alisema CCM haistahili kutumia rasilimali za serikali katika shughuli za chama wakati inafahamu kuwa nchi ipo katika mfumo wa vyama vingi

vya siasa na hivyo magari hayo ya serikali yametokana na kodi ya Watanzania wote na siyo ya wananchi ambao ni wanachama wa CCM pekee yake.

Alipoulizwa na NIPASHE, kuhusiana na tuhuma za Ukawa, Kinana alisema Ukawa wameishiwa hoja, wamedharauliwa na sasa wanatapatapa.
 
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa