KAMPUNI YA MSAMA PROMOTIONS KUPELEKA MATAMASHA MENGINE MJINI SONGEA, NI KUTOKANA NA MWITIKIO WA WANASONGEA‏

  Mwimbaji wa Muziki wa injili Upendo Nkone akiimba mbele ya mashabiki wa muziki huo kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea ambapo tamasha kubwa la Krismas limefanyika na kushirikisha waimbaji mbalimbali kutoka nchini na nje ya Tanzania, onesha la leo lilikuwa ni hitimisho la matamasha ya Krismas yaliyofanyika katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Ruvuma yakishirikisha waimbaji kama Upendo Nkone, Faraja Ntaboba kutoka nchini DRC Congo , Edson Mwasabwite. Wngine ni Ambwene Mwasongwe, Bonny Mwaiteje, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa Kutoka nchini DRC Congo , Tumaini Njole, Titha Mutinda kutoka nchini Kenya Joshua Mlelwa na wengine wengi.Tamasha...

UKAWA WAAMBULIA VITI 38 TUNDURU

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilani Tunduru, kimeibuka kidedea kwa kupata viti katika vijiji 105 katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyia jana nchi nzima. Kwa mujibu wa takwimu hizo, vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimepata viti 38 kati ya vijiji vyote 153 vilivyopo wilayani hapa. Aidha, takwimu hizo zinaonesha kuwa hadi sasa bado matokeo ya vijiji 10 hayajapatikana, kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za baadhi yake kutopiga kura kwa kukosekana vifaa vya kupigia kura. Sababu nyingine ambazo zimekwamisha kupatikana kwa takwimu kutoka katika vijiji hivyo, ni pamoja na kutokamilika kwa zoezi la kuhesabu kura na pia kuwepo kwa pingamizi. Akizungumzia zoezi hilo msimamizi wa Uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru,...

RADI YAUA SITA, YAJERUHI WAWILI

WATU sita wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi katika migahawa miwili inayohudumia wanafunzi wa Chuo Cha Maendeleo na Mifugo (LITA). Tukio tukio hilo lilitokea juzi jioni usiku wilayani hapa wakati wanafunzi hao wakiwa kwenye mgahawa kwa ajili ya kupata mlo wa jioni Kwa mujibu wa Ofisa Muuguzi Kiongozi wa Kituo cha Afya Madaba, Oraph Pili, siku ya tukio kulikuwa na mvua iliyoambatana na radi ambayo ilipiga eneo walilokuwapo wanafunzi hao Alisema radi hiyo mara baada ya kupiga ilisababisha vifo hivyo sita na kuwajeruhi wengine wawili waliokuwapo eneo hilo. Pili aliwataja waliofariki ni Chesko Luoga, mwanafunzi wa mwaka wa pili, Lucas Mabula (mwanafunzi mwaka wa kwanza) Justin Ngonyani na Edwin Funga, wakazi wa Madaba, Hosana Antony...

WALIMU WALIOGOMA WATISHWA

WALIMU wa Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, walioshiriki kwenye mgomo uliolitikisa taifa, wametishiwa kuchukuliwa hatua za kisheria na hata kuwajibishwa endapo itabainika walishiriki. Ofisa Elimu wa Wilaya ya Tunduru, Rashid Mandoa, aliiambia Tanzania Daima juzi kuwa walimu hao watachukuliwa hatua za kuwajibishwa kutokana na kukiuka taratibu za kufanya mgomo na watahesabiwa kama watoro katika siku walizoshiriki mgomo huo. Akifafanua tukio hilo, alisema walimu hao watatakiwa kujutia kitendo hicho kutokana na kupotoshwa na uongozi wa Chama cha Walimu (CWT). Mandoa alisema tayari wamekwishatuma timu ya waratibu elimu kata na makatibu kata kutembelea shule zote wilayani humo, ili kubaini walimu walioshiriki mgomo huo. Chanzo;Tanzania Daima Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote...
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Ruvuma Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa