WATU sita wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya
kupigwa na radi katika migahawa miwili inayohudumia wanafunzi wa Chuo
Cha Maendeleo na Mifugo (LITA).
Tukio tukio hilo lilitokea juzi jioni usiku wilayani hapa wakati
wanafunzi hao wakiwa kwenye mgahawa kwa ajili ya kupata mlo wa jioni
Kwa mujibu wa Ofisa Muuguzi Kiongozi wa Kituo cha Afya Madaba, Oraph
Pili, siku ya tukio kulikuwa na mvua iliyoambatana na radi ambayo
ilipiga eneo walilokuwapo wanafunzi hao
Alisema radi hiyo mara baada ya kupiga ilisababisha vifo hivyo sita na kuwajeruhi wengine wawili waliokuwapo eneo hilo.
Pili aliwataja waliofariki ni Chesko Luoga, mwanafunzi wa mwaka wa
pili, Lucas Mabula (mwanafunzi mwaka wa kwanza) Justin Ngonyani na Edwin
Funga, wakazi wa Madaba, Hosana Antony Mkazi wa Mbinga na Eva Chapile
mkazi wa Njombe ambao walikuwa wafanyakazi wa migahawa hiyo.
Muuguzi huyo aliwataja waliojeruhiwa ni Beatrice Mhagama mwanafunzi mwaka wa tatu na Leokadia Fusi mkazi wa Madaba
Alisema majeruhi hao mara baada ya kufikishwa kwenye kituo cha afya
Madaba na kuonekana wanahitaji matibabu zaidi walihamishwa kwenye
hospitali ya rufaa ya Songea wanakoendelea na matibabu.
Muuguzi huyo alisema hali za majeruhi hao zinaendelea vizuri huku
miili ya wanafunzi hao imehifadhiwa hospitali ya rufaa Songea na
inatarajiwa kusafirishwa kwenda nyumbani kwao kwa mazishi.
Naye Mkuu wa chuo hicho, Darlington Nkenwa, alisema wamesikitishwa na
vifo hivyo vilivyotokana radi iliyosababishwa na iliyoanza kunyesha saa
12 jioni hadi saa 5 usiku.
Chanzo;Tanzania daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment