CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilani Tunduru, kimeibuka kidedea kwa kupata viti katika vijiji 105 katika matokeo ya awali ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyia jana nchi nzima.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimepata viti 38 kati ya vijiji vyote 153 vilivyopo wilayani hapa.
Aidha, takwimu hizo zinaonesha kuwa hadi sasa bado matokeo ya vijiji 10 hayajapatikana, kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za baadhi yake kutopiga kura kwa kukosekana vifaa vya kupigia kura.
Sababu nyingine ambazo zimekwamisha kupatikana kwa takwimu kutoka katika vijiji hivyo, ni pamoja na kutokamilika kwa zoezi la kuhesabu kura na pia kuwepo kwa pingamizi.
Akizungumzia zoezi hilo msimamizi wa Uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Tinna Sekambo, alisema kuwa takwimu kamili za uchaguzi huo zikiwemo za wenyeviti wa vitongoji na wajumbe, zitatolewa kesho baada ya kukamilika kwa zoezi la kuunganisha matokeo hayo.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Chande Nalicho pamoja na mambo mengine, alisema kuwa zoezi hilo limefanyika katika hali ya usalama wa hali ya juu.
Chanzo:Habari Leo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment